Home

KIGOMA ALL STARS waingia mkoani KIGOMA kwa kishindo.

Leave a comment


Wasanii wale wa bongo fleva waliotokea Kigoma hivi sasa wapo jijini tayari kwa show yao ya tarehe 17/07/2012. Wasanii hao ni kama Linex, Abdu Kiba, Mwasiti, Recho, Banana Zoro, Diamond, Ommy Dimpoz, Queen Dlyn, Macomandor..etc..Show hiyo itakuwa free katika uwanja wa Lake Tanganyika…
Don’t miss..

source:djchoka.

Matarajio ya kupata mshindi kutoka Tanzania katika mashindano ya Tusker Project Fame msimu wa tano jana yafikia ukingoni

Leave a comment


Matarajio ya kupata mshindi kutoka Tanzania katika mashindano ya Tusker Project Fame msimu wa tano jana yamefutika rasmi baada ya mshiriki aliyekuwa amesalia kutoka Tanzania kutoka.
Damiani Innocent Mihayo alifungasha virago jana baada ya jitihada zake za kuonesha kuwa aliingia kwenye probation kwa bahati mbaya kugonga mwamba. “Damian is Good…Bad choice ya nyimbo aliyoimba,he also lacks star quality,” aliandika mfuatiliaji mmoja wa mashindano hayo.
“Huyu jamaa (Damian) like two weeks ago alichemka mistari ya Ali Kiba, shame! Aaaa project fame alikua Lina, Msechu na kidoooogo Aneth, yaani hata Hemedi namsifu, he knew how to play the game. Ndo makosa tunafanya hata BBA. Watu kama Hemedi au hata Wema ni watu wanajua kucheza na ni rahisi watanzania kutoa support. Hilda na Julio ppphhheeeew,” aliandika mwingine aitwaye Yvonne kupitia Facebook.
Kutokana na kutolewa kwa Damian sasa watanzania watabakia kuwashuhudia tu washiriki kutoka Uganda, Kenya, Sudan Kusini, Rwanda na Burundi katika shindano hilo. Katika hatua nyingine wiki hii Universal Music Group (UMG) imeingia mkataba na shindano hilo ambapo itamsimamia mshindi wa mwaka huu. Pia itasimamia kurekodi albam ya pamoja ya washiriki kumi bora wa mwaka huu.

Single Boy ya Alikiba: Namba tatu kwenye radio maarufu ya Lagos

1 Comment


ALIKIBA NA LADYJAYDEE


Kama unadhani kuwa nyimbo za Nigeria zina umaarufu nchini kuliko nyimbo za Tanzania zinavyojulikana nchini Nigeria, unaweza kuwa wrong!
Ngoma ya Alikiba– Single Boy inabang kinoma nchini Nigeria.
Infact kituo cha radio kinachosikilizwa zaidi kwenye mji mkuu wa kibiashara nchini Nigeria, Lagos, The Beat 99.9 FM kimeuingiza wimbo huo kwenye chart zake.
Wiki hii radio hiyo kupitia ukurasa wake imetweet. “ #AfricanTop10 At number 3, we have “Single Boy” Ft. Lady Jay Dee (@JideJaydee) – Ali Kiba (@AlikibaTZ4Real).”
Kwa taarifa yako tu ni kuwa Beat 99.9 FM – Lagos #1 Hit Music Station! inasikilizwa na asilimia 49 ya ya wakazi wa Lagos wanaofikia milioni 15.
Kwenye page yake ya Facebook ina zaidi ya mashabiki 300,000 na Twitter ina zaidi ya followers 21,600. Hivyo kwa resume hiyo, hii si radio ndogo.
Katika hatua nyingine jana kupitia Twitter, Alikiba amesema yuko mbioni kuachia ngoma nyingine, “Get ready for my new track .its a sexy song in another feelings.”

source:bongoflavortz

%d bloggers like this: