Home

RAIS WA ZAMANI WA MISRI HOSNI MUBARAK AREJESHWA GEREZANI.

Leave a commentRais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak amerejeshwa gerezani baada ya kupata matibabu hospitalini.
Mwendesha mashitaka wa umma nchini humo ameamuru kuwa afya ya Mubarak mwenye umri wa miaka 84 imeimarika na kwamba hapaswi tena kuendelea kuwa katika hospitali ya kijeshi.
Mubarak anatumikia kifungo cha maisha gerezani kutokana na mauaji ya waandamanaji wakati wa wimbi la mageuzi katika ulimwengu wa kiarabu ambalo lilianza mwezi wa Januari mwaka wa 2011.
Hosni Mubarak aliondolewa madarakani wakati wa vuguvugu hilo la umma na kuumaliza utawala wake wa miaka 30 nchini Misri.

AFANDE SELE AKIFUNGUKA KUHUSU SHOW YA ZANZIBAR MUSIC AWARD

Leave a comment


Salaam Ndugu zangu wote mashabiki na wadau wa muziki wetu!!
Tamko langu kuhusiana na lugha zilizotolewa na Twent Percent kuhusiana na show yetu ya Zanzibar Music Award.
“Tulialikwa kwenye ZANZIBAR MUSIC AWARD, na kabla ya kazi makubaliano yote ya kazi kwa mujibu wa mkataba yalifuatwa, makubaliano hayo yalihusisha sisi kujigharamia gharama zote za nauli na Malazi (accomodation).
Tulifika Zanzibar salama, tulipokua Zanzibar twenty alitaka agharamiwe huduma zote ambazo ni nje ya mkataba wetu, nikamuomba na kumsihi sana Ndugu yangu aheshimu mkataba, asitafute matatizo kwani tayari mpaka wakati huu tuna kesi na Halmashauri ya Manispaa ya Moro ambayo kimsingi sikuhusika (nilishatolea ufafanuzi siku za nyuma).
Lakini yeye alipingana na mimi, akanibishia na kunisukuma Mbele ya wageni na wenyeji wetu, wakiwemo Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seiph Ali Idi, Waziri Seiph Khatibu.
Walikuwepo waadishi wa habari wa siku Nyingi Akiwemo Abubakari Liongo (idhaa ya kiswahili radio Ujerumani), Mkurugenzi wa ZENJI FM ndugu Tua Saidi Tua.
Mimi Selemani Abdallah Juma Msindi sihusiki kwa namna yoyote, na tabia zisizo za kuridhisha zinazoonyeshwa na Ndugu yangu Twenty Percent, ambae nimekua nae nyumbani kwangu hata kabla ya Tuzo zake Tano (Kili Music Award) ambazo kazi hizo zote hizo kaandikia nyumbani kwangu siwezi kuwa na tatizo nae ni ndugu yangu kiimani na kikazi, hata kazi yangu niliyofanya nae kabla siku za nyuma “MBELE YAKO NYUMA YANGU” .. Kuna mstari Nilisema ” ..Kuandika Rhyme kwenda Gym kimtindo kuonyesha Ugum, bado unatakiwa uwe na nidhamu ya kweli, sio ya kumzuga Mwalimu, utajihukumu”.
Nimekua nikisisitiza nidhamu kwa Ndugu zangu woote toka enzi za Ghetto BoyZ, Watupori na Mabwasha’Kingdom, ambao wengine hawafanyi sanaa, ila nipo nao kwenye Familia yetu kubwa hapa Tanzania. Nimesikitishwa na kitendo hicho. Siku zote nimekua mwenye kuhitaji suluhu kwa namna ya Amani.
Verry sorry kwa wote ambao mumefadhaika kwa hilo. Tuendelee kuwa pamoja na msisite kutoa ushauri wenu, maoni ili Game letu lisonge. MUNGU ATUBARIKI.
Asanteni sana.
Selemani Juma Abdallah Mutabhazi Msindi.
a.k.a Afande Sele (King of Rhymes)

source:

Lissu sasa matatani

Leave a comment


MNADHIMU wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu ameingia matatani kutokana na kauli yake kwamba Rais Jakaya Kikwete amekuwa akiteua majaji wa Mahakama Kuu wasiopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Kutokana na kauli hiyo aliyoitoa wakati akiwasilisha maoni ya kambi yake, kuhusu hotuba ya makadirio ya matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria, Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) atajadiliwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Wakati akisoma hotuba yake, mbunge hiyo alisema majaji wanaoteuliwa na Rais hawafanyiwi ‘vetting’ (uchunguzi) na tume hiyo kuona kama uwezo na ujuzi wao unafaa kukabidhiwa madaraka ya ujaji.

Mwenyekiti wa Bunge, Jenista Mhagama ndiye aliyeamuru suala la Lissu kupelekwa katika kamati hiyo baada ya mbunge huyo kukataa kufuta kauli yake ambayo kwa mtazamo wa Serikali iliwadhalilisha majaji.

Hata hivyo, jana alipotakiwa kueleza kama ana taarifa rasmi za kuitwa kwenye kamati hiyo Lissu alisema: “Sijaitwa, lakini nina taarifa kuwa naweza kuitwa.’’

Alisema, hata wakimwita hatakuwa na jambo lolote la kuzungumza kwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge aliyeongoza kikao hicho juzi (Jenista Mhagama), alikosea kwa kuwa ndiye aliyepaswa kumpa adhabu.

Mbunge huyo alisema juzi aligoma kufuta kauli yake kama alivyotakiwa na Mwenyekiti kwani aliamini kuwa hata Mwanasheria Mkuu alikuwa amekosea.

Alibainisha kuwa endapo ataitwa katika kamati hiyo, atahoji kama waliomwita wamegeuka kuwa wenyeviti wa Bunge na kama si hivyo, anaamini watakosa neno la kumhoji.

Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kwa nyakati tofauti wakati wakijibu hoja za wabunge juzi jioni walisema: “Lissu aliwakashifu majaji bungeni, hivyo alipaswa kuomba radhi.”

Kwa upande wake Werema alimtaka Lissu kufuta kauli yake na kwamba ikiwa hatafanya hivyo basi awasilishe vielelezo vinavyothibitisha madai kwamba majaji huteuliwa bila kufanyiwa uchunguzi.

“Lissu ni mtaalamu wa sheria, lakini kauli yake imewafedhehesha majaji na inashangaza inapotolewa na wakili machachari kama yeye,” alisema Werema.

Werema pia alimtaka Lissu kuondoa kauli yake kwa kuwataja watu ambao sio wabunge kwa kunukuu gazeti la Mwanahalisi lililowataja watu watatu kuwa wamehusika na mauaji ya Dk Steven Ulimboka.

Werema alisema iwapo Lissu hataondoa maneno yake suala hilo lipelekwe katika Kamati ya Maadili.

Kwa upande wake, Chikawe alimwombea radhi Lissu kwa majaji akisema anajua hakutoa kauli ya kuwadhalilisha majaji kwa kukusudia.

“Lissu amemtuhumu hadi Rais katika uteuzi wa majaji, hili siyo sahihi, uteuzi wa majaji hupendekezwa na tume maalumu inayohusisha majaji wazoefu ambao ndio wanapendekeza majina kwa Rais,” alisema Chikawe.

Baada ya maelezo hayo, Mhagama aliamuru Lissu kuondoa kauli yake hiyo baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Werema wakati akifanya majumuisho ya mjadala wa wizara hiyo.

Hata hivyo, Lissu alipopewa nafasi alisema hawezi kuondoa kauli yake kwa kuwa mchakato mzima wa kumtaka afanye hivyo haukufuata Kanuni za Bunge.

Lissu alinukuu kanuni ya 63 (1) ambayo inasema: “Bila kuathiri masharti ya Ibara ya 100 ya Katiba yanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika Bunge, ni marufuku kabisa kusema uongo bungeni kwa sababu hiyo, mbunge yeyote anapokuwa akisema bungeni ana wajibu wa kuhakikisha kwamba anatoa kauli au maelezo kuhusu jambo au suala ambalo yeye mwenyewe anaamini kuwa ni kweli na siyo jambo la kubuni au la kubabaisha tu”.

Lissu aliongeza kuwa, Jaji Werema na Mhagama walivunja Kanuni za Bunge kwa kumtaka kuondoa kauli inayodaiwa kuwa ya uongo kinyume bila kufuata utaratibu.

Alipoulizwa kuhusu utekelezaji wa hatua hiyo jana, Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema alisema kuwa siyo lazima kwa Watanzania kufahamu hilo.

“Nilipozungumza jana (juzi) sikuzungumza na Watanzania bali nilizungumza na Bunge, hivyo siyo lazima Watanzania kufahamu jambo hilo na wala sioni sababu za kwa nini liandikwe magazetini,’’ alisema Jaji Werema.

source:mwananchi.

SIMBA SC YAIBUKA MABINGWA WA KOMBE LA URAFIKI.

Leave a comment


Waziri asiye na Wizara maalum Zanzibar Mh. Machano Othman Said akimkabidhi kombe la ubingwa wa michuano ya Urafiki nahodha wa timu ya Simba Juma K. Juma mara baada ya timu ya Simba kuifunga timu ya Azam FC magoli 5-3 kwa penati, baada ya kutoka suluhu magoli 2-2 katika kipindi cha dakika tisini, kwenye mchezo mzuri na wa kuvutia kwa timu zote na hivyo kuifanya Simba kuibuka mabingwa wa kombe hilo.(Picha na Fullshangwe Blog).

Mabingwa wa Tanzania Bara klabu ya Simba SC imeibuka bingwa wa kombe la Urafiki (ujirani mwema) baada ya kuifunga timu ngumu ya Azam FC kwa bao 4 – 3 kwa njia ya mikwaju ya penati.
Mchezo huo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ulikuwa wa vuta nikuvute ambapo hadi timu hizo zinakwenda mapumziko mabao yalikuwa ni 1-1, ambapo kwa upande wa Simba goli lilifungwa na Felix Sunzu na Khamis Mcha aliisawazishia Azam FC.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu hizo kushambuliana ambapo mchezaji John Boko aliipatia Azam FC goli la pili kabla ya ksawazishwa na kiungo bora wa Simba Mwinyi Kazimoto.
Baada ya mechi hiyo kumalizika timu hizo zikiwa sare ya bao 2-2 ndipo ilipotumika mikwaju ya penati kuamua nani atakuwa bingwa wa Kombe la Urafiki, ambapo Simba ilitawazwa kuwa bingwa kwa kupata penati 4 dhidi ya 3 za Azam.

source:/dewjiblog.

Vox Media: Utendaji mbovu umemuondoa Dr. Asher Rose Migiro UN

Leave a comment


Wiki hii aliyekuwa naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa Dr.Asha Rose Migiro amerejea nchini baada ya kuutumikia kwa miaka mitano.
Hata hivyo shirika la habari la Vox Media limebaini sababu za kwanini Dr. Migiro hakuongezewa muda wa kufanya kazi kwenye umoja huo.
Limesema vyanzo vya ndani ya UN vimesnitch kuwa utendaji dhaifu na kushindwa kufit kwenye chombo hicho kigumu ni baadhi ya sababu ya kushindwa kuongezewa mkataba wa kufanya kazi humo.
“Nafasi ya Unaibu katibu mkuu ni ngumu mno; inahitaji mtu mzoefu kuongoza vema Secretariat. Changamoto yake kubwa ilikuwa ni kuelewa siasa katika chombo hicho cha kimataifa na kuunda muungano,” chanzo kimoja kiliiambia Vox Media.
Inadaiwa kuwa Dr. Migiro alizungumza na kundi la waafrika lenye asilimia 28 ya wajumbe wa umoja wa mataifa ili achaguliwe tena lakini walimtosa.
“Hakuwa maarufu miongoni wa wanadiplomasia. Hakuna aliyemsikiliza. Unaweza kukumbuka pia kuwa uteuzi wake ulikosolewa sana,” kilisema chanzo hicho.
Katika hatua nyingine Dr. Migiro alisema hana mpango wa kuwania urais wa Tanzania na huenda akarejea kwenye kazi yake ya zamani ya uhadhiri wa chuo kikuu.

Washington D.C:Polisi atishia kumuua Michelle Obama

Leave a comment


Afisa wa polisi wa jijini Washington D.C. anayehusika na kulinda maafisa wa ikulu ya White House nchini Marekani, amejikuta akipumzishwa kazi baada ya kudaiwa kutishia maisha ya First Lady, Michelle Obama.
Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post, ofisa huyo anafanya kazi ya escort ya pikipiki na anadaiwa kusema kuwa angempiga risasi First Lady huyo.
Inasemekana aliwaonesha polisi wenzake picha ya bunduki ambayo angeitumia kumuulia.
Hata hivyo idara ya polisi ya jijini Washington imesema haina maelezo mengi kuhusiana na tukio lakini msemaji wake Gwendolyn Crump amesema kwenye maelezo:
“We received an allegation that inappropriate comments were made. We are currently investigating the nature of those comments.”
Idara hiyo pia iliwasiliana na ‘Secret Service’ kuhusiana na kitisho hicho.
Msemaji wa Secret Service Ed Donovan amesema mamlaka hiyo inalifahamu tukio hilo na inachukua hatua zinazotakiwa kwa uchunguzi maalum.

source:bongo5

WAJANJA WA BUSH WAMLIZA TIMBULO DOLA 800

Leave a comment


Nyota wa muziki wa kizazi kipya Bongo, ALLY Timbulo ‘Timbulo’ amepatwa na tukio la aina yake baada ya wajanja wa Bush kumliza kamera kubwa aina ya sonny wakati wa paty maalumu aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita kijijini kwao Riuwa, Wilayani Mbalali jijini Mbeya.

Akizunguma na Teentz mapema leo Timbulo amesema kuwa aligundua kupotea ghafla kwa kamera yake hiyo mara baada ya kumalizika kwa paty hiyo iliyokuwa imechangamka kupita kiasi huku vijana wengi aliokuwa wamefurika wakiwa hoi kwa mitungi.
“Nilipomaliza kuimba nikawa nimechili sehemu napumzika, lakini baada ya party kuisha nianza kukusanya vitu vyangu na baadae nikagundua kuwa kamera yangu haipo, kwa kweli nilichanganyikiwa kwa kuwa bado ni mpya kabisa na niliinunua kiasi cha dola 800 za Marekani” alisema Timbulo
Akiendelea zaidi timbulo amesema kuwa juhudi za kumsaka mtu aliyesepa na kamera hiyo ya kisa bado zinaendelea kwa kuwa sehemu kubwa ya watu waliofika siku hiyo wanafahamiana hivyo anaamini ndani ya siku chache zijazo atakuwa ameipata.
katika shoo hiyo Timbulo amerifu kuwa jukwaa alilokuwa analitumia kuwaburudisha mashabiki wake lilishindwa kuhimili vishondo na kuvunjika kufuatia watu kushindwa kuvumilia na kupanda juu alipokuwa yeye na hatimaye jukwaa hilo likasalimu amri.
“Hakika ilikuwa siku mbaya kwani kuna mambo mengi yalijitokeza ikiwamo shughuli yangu kucheleweshwa baada ya mchana na kuwa ucku kutokana na mtendaji wa kata kuzuia mpaka diwani alipoingilia kati na kuniruhusu” alimaliza

source:teentz

Older Entries

%d bloggers like this: