Home

Happy Birthday Mandiba “NELSON MANDELA”

Leave a comment


Nelson Rolihlahla Mandela alizaliwa tarehe 18 Julai, mwaka 1918. Ni rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini Afrika Kusini. Alikuwa mwanasheria na mwanachama wa ANC aliyepinga siasa ya Apartheid katika Afrika Kusini. Mandela alitumikia kifungo cha maisha kwa miaka 27 kutokana na harakati zake za kuupinga ubaguzi wa rangi. Alifungwa katika kisiwa cha Robben. Baada ya kuachiliwa huru mwaka 1990 alianzisha sera ya maridhiano. Mwaka wa 1993, pamoja na Frederik Willem de Klerk alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani.
Jumanne hii rais wa zamani Bill Clinton alienda nyumbani kwa Nelson Mandela Kumtakia kila la heri katika kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa. hata hivyo
Rais Barack Obama na Mke wake Michelle Obama, jana pia walimtumia salamu za pongezi kwa Mandiba kwa heshima ya juu zaidi. “ kwa niaba ya watu wa Marekani, Tungependa Kutoa pongezi zetu za dhati kwa siku ya kuzaliwa ya miaka 94 na mwaka wan ne wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya nelson Mandela’s day”. Alisema Obama

Tamko Maalum Kutoka CHADEMA Kuhusu Yaliyojiri Katika Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA Uliofanyika Kata ya Ndago Siku ya Jumamosi Tarehe 14 Julai 2012

Leave a comment


Ofisa wa Sera na Utafiti CHADEMA Makao Makuu Bw. Waitara Mwita Mwikwabe


CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

Tamko Kuhusu Yaliyojiri Katika Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA  Uliofanyika Kata ya Ndago Siku ya Jumamosi Tarehe 14 Julai 2012

1. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliandaa mikutano ya  hadhara katika Jimbo la Iramba Magharibi. Mikutano hiyo ilitolewa taarifa polisi na jeshi hilo lilitoa baraka zake kama utaratibu wa sheria unavyotaka kwa barua yake ya tarehe 12 Julai 2012 Kumb. Na. KIO/ B1/1/VOL.V/268

2. Mkutano wa kwanza ulipangwa kufanyika katika Kata ya Ndago katika  viwanja vilivyo karibu na kituo cha mabasi ambapo pia ni hatua chache karibu kabisa na Kituo cha Polisi Ndago. Mkutano huu ulipangwa kuanza saa nane mchana.

3. Msafara wa kitaifa unaofanya ziara ya ukaguzi wa chama, katika mkoa  wa Singida chini ya uratibu wa Ofisa wa Sera na Utafiti Makao Makuu, Mwita Mwikwambe Waitara, (ikiwa ni maandalizi ya operesheni nyingine kubwa mkoani humo itakayofanyika baadae), uliwasili katika eneo la  Mkutano majira ya saa tisa na nusu alasiri. Tulikuta wananchi wengi
wakiwa wanatusubiri. Kabla ya Mkutano kuanza tulipewa taarifa kwamba kuna kikundi cha vijana kimeandaliwa kuvuruga mkutano wa CHADEMA kwa kufanya fujo, ikiwemo kurusha mawe ili mkutano huo usifanyike. Suala hilo lilielezwa mkutanoni mapema na Mheshimiwa Waitara, mbele ya askari polisi.

4. Wakati tukijiandaa kuanza hotuba, vijana wapatao wanane walianza chokochoko kwa kutoa matusi na punde mawe yakaanza kurushwa kutoka sehemu mbalimbali. Wakati fujo zinaanzishwa na kile kikundi, Mheshimiwa Waitara alikuwa bado anazungumza na wananchi kuwaandaa kusikiliza wazungumzaji wengine. Vurumai hiyo ilizimwa na wananchi
wenyewe wa Ndago waliokuwa na hamu ya kusikiliza ujumbe wa viongozi wa kitaifa wa CHADEMA.

5. Kwa kweli tunawashukuru wananchi wengi wa Ndago walioonesha ujasiri  mkubwa kuweza kuwaondoa vijana wale eneo la mkutano, kisha mkutano ukaendelea, huku wananchi wakionesha kila hamasa ya kufurahia hoja kutoka kwa wazungumzaji, akiwemo Mheshimiwa John Mnyika, ambaye aliombwa ahudhurie ziara hiyo kwa nafasi yake ya Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA.

6. Mpaka tunamaliza mkutano huo ambao wananchi waliufurahia sana kwa  namna ulivyohutubiwa kwa amani na utulivu huku wazungumzaji wakijenga hoja juu ya mstakabali wa jimbo na taifa lao kwa ujumla, mamia ya wananchi waliohudhuria walitaka tuendelea kuhutubia, lakini tulibanwa na ratiba ya kuwahi mkutano wa pili, eneo la Kinampanda.

7. Lakini kutokana na vurugu hizo zilizokuwa zikisababishwa na kikundi  cha vijana ambao tayari ilishatolewa taarifa yao kwenye mkutano huo, lakini askari waliokuwepo hawakuthubutu kuchukua hatua, tulilazimika kuomba msaada kutoka kwa OCD na R.P.C, ambapo baadae wakati mkutano unakaribia kuisha tuliona gari la polisi kutoka Mjini Singida likiwa na askari waliojipanga rasmi kwa ajili ya kuzuia vurugu likifika pale
eneo la mkutano, lakini wakati huo hali ilishatulia na hotuba zimetolewa vizuri.

8. Kutokana na hali hiyo ya vurugu, zilitolewa taarifa Kituo cha  Polisi cha Ndago, ambapo lilifunguliwa jalada NDG/RB/190/2012. Katika jalada hilo tulitaja baadhi ya majina ya watuhumiwa waliokuwa vinara wa kundi lililokuwa likifanya fujo kwenye mkutano mbele ya askari polisi. Majina hayo ni; 1. Daniel Sima, 2. Tito Nitwa, 3. Bakili Ayubu, 4. Yohana Makala Mpande, 5. Ernest Kadege, 6. Abel John, 7. Athuman Ntimbu, 8. Martin Manase, 9. James Ernest, 10. Simion Makacha, 11. Anton John, 12. Frank Yesaya

9. Kwa hakika askari polisi wa Ndago waliokuwepo mkutanoni mbali ya  kutochukua hatua yoyote dhidi ya fujo tulizofanyiwa ikiwemo kupondwa mawe na kikundi kidogo cha wahuni, fujo zilipozidi askari wote walikimbia eneo la mkutano, akabaki OCS pekee ambaye naye alionekana dhahiri kutotaka kuchukua hatua stahili. Hakuonekana kufanya juhudi zozote za kuhakikisha amani inalindwa na ulinzi unaimarishwa katika eneo la mkutano na hatua zinachukuliwa dhidi ya watu walioonekana kudhamiria kufanya fujo.

 Mtu yeyote makini angeweza kuona kuwa askari wale walikuwepo pale mkutanoni ‘almuradi’ tu lakini kama vile walikuwa na maelekezo maalum ya kuhakikisha hawachukui hatua yoyote katika kuzuia mpango wowote wa kusababisha vurugu na kuvunja amani.

10. Baada ya kumaliza mkutano wa Ndago kwa amani, tulikwenda  Kinampanda ambako tulifanya mkutano mwingine mzuri kwa amani kabisa, ambapo mbali ya wananchi kuwa wametusubiri kwa hamu kubwa na kutusikiliza kwa makini hoja zetu, polisi katika eneo hilo walitupatia ushirikiano mzuri tangu wakati tunafika mpaka tulipomaliza mkutano
huo.

11. Jioni wakati tumerudi hotelini, tukasikia kuna taarifa  zinasambazaa kuwa kuna mtu/watu wamekufa katika eneo la Ndago. Habari hizo zilikuwa zinakanganya kwa sababu zilikuwa zikitaja idadi tofauti tofauti. Lakini kwa vyovyote vile kama ni kweli kuna tukio la mtu
kufariki, CHADEMA tunasikitika sana kwa tukio hilo la uhai wa mtu.

12. Tunalaani taarifa zinazozidi kusambazwa ambazo zinawataja polisi  kuwa wanatuhusisha CHADEMA na tukio la mtu aliyefariki. Hii ni ajabu kubwa kwamba tumetoka kwenye mkutano ule kwa amani kabisa mpaka tumemaliza mkutano wa pili kwa amani na polisi wakiwepo sehemu zote mbili, kisha tunasingiziwa masuala ambayo wenyewe hatukuwa na habari nayo tangu mkutano wa kwanza ukiwa unaendelea mpaka mkutano wa mwisho
ulipomalizika.

13. Kutokana na habari hiyo ya kifo cha mtu inavyoenezwa kwa  kuihusisha CHADEMA, tumebaini kuwepo kwa mbinu na mikakati ya chama tawala pia vyombo vya dola vikihusika kutaka kuwatisha wananchi waSingida, Watanzania wote wapenda mabadiliko na viongozi wa CHADEMA katika mkoa huu, wasifanye kazi ya kisiasa kwa kuwabambikizia tuhuma
na kesi na pia kuwafanya waonekane ni watu wa vurugu.

14. Tunapenda kusema hapa kuwa njama hizo hazitafanikiwa. Zitashindwa  kama zilivyoshindwa njama zingine zote ambazo zimekuwa zikifanywa na vyombo vya dola, viongozi wa serikali na chama tawala dhidi ya CHADEMA na vuguvugu la mabadiliko nchini.

15. Tunawataarifu wananchi kuwa ratiba ya kufanya Operesheni nyingine  kubwa katika Mkoa wa Singida, ikiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa, itafanyika baadae kama ilivyoazimiwa na kikao cha Kamati Kuu.


Imetolewa leo Singida, Julai 15, 2012 na;
Waitara Mwita Mwikwabe
Ofisa wa Sera na Utafiti CHADEMA Makao Makuu

source:fatherkidevu

RAIS WA MADAKTARI WA ALIEFIKISHWA MAHAKAMANI JULY10 NDIO HUYU.

Leave a comment


Rais wa chama cha Madaktari Tanzania MAT Namala Mkopi amefikishwa kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es salaam kujibu mashitaka mawili yanayomkabili kuhusiana na mgomo wa madaktari Tanzania.

Akimsomea mashtaka hayo mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya Kisutu Faisal Kahamba, Mwendesha mashtaka wakili mwandamizi wa Serikali Tumaini Kweka amesema kosa la kwanza Dr Mkopi anashitakiwa kwa kutotii amri halali ya mahakama kuu kitengo cha kazi iliyomtaka atangaze kusitisha mgomo wa madaktari.

Wakili Kweka amesema kosa hilo ni kinyume cha kanuni ya adhabu namba 124 ambapo kosa la pili linalomkabili Dr Mkopi ni kuhamasisha mgomo wa Madaktari kinyume na kanuni na adhabu ya kifungu cha 390 na kifungu cha 35.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo Dr Mkopi aliyakana yote ambapo mawakili wake wanne wanaomtetea wakiongozwa na Kikondo Maulid wameomba mteja wao apatiwe dhamana ambapo hakimu mkazi Faisal Kahamba amesema dhamana ipo wazi na kutaja masharti ya dhamana hiyo ambayo yalipingwa na mawakili wa upande wa utetezi.

Masharti ya dhamana yaliyotajwa yalikua ni wadhamini wawili waajiriwa wa serikali au taasisi zinazotambulika kisheria wakiwa na vitambulisho vyao na hati ya mali isiyopungua thamani ya shilingi laki tano ambapo mawakili wa upande wa mashitaka walitaka masharti ya kukabidhi hati ya kusafiria na kuzuiwa kusafiri nje ya Dar es salaam ndio yaingizwe kwenye masharti ya dhamana.

Hali hiyo ya mvutano wa kisheria ilimlazimu hakimu huyo jana Mahakamani kuomba muda wa dakika kumi ili apitie sheria husika na baada ya hapo mahakama iliamua kumuachia Dr Mkopi kwa masharti yaliyotajwa awali ambapo hakimu alitangaza kwamba kama kuna mtu hajaridhia dhamana hiyo anaweza kukata rufaa mahakama kuu hivyo akaiahirisha kesi hiyo mpaka mwezi wa nane tarehe 6 mwaka huu.

source:millardayo.

Kocha Roberto Mancini wa Manchester City asaini mkataba Mpya

Leave a comment


Roberto Mancini, Kocha wa sasa wa timu ya Manchester City, alichukua nafasi ya Mark Hughes kama kocha, Desemba mwaka 2009,ambapo anasifika kwa kuiongoza timu hiyo hadi kutwaa kombe la FA mwaka 2011.
Mwaka mmoja baada ya hapo, City ilitwaa taji lake la kwanza la Ligi Kuu tangu mwaka 1968,Mancini amesain mkataba mpya wa kuendelea kufunda timu hiyo hadi mwaka wa 2017.

Producer Ally Baucha afiwa na baba yake mzazi

Leave a comment


Producer mkongwe nchini wa studio za Baucha Records, Ally Baucha, amefiwa na baba yake mzazi usiku wa kuamkia leo.
Leo usiku muda wa saa 6:26, ametutumia ujumbe wa simu unaosema, “Mambo vp…? Nimefiwa na baba mzazi leo usiku huu. Najua wewe ni mtu muhimu kukutaarifu kwanza, nasubiri kuelekea Zanzibar kwa mazishi… Baucha.”
Baucha amesema kifo cha baba yake Mzee Mohamed Yussuf kimetokana na ugonjwa wa ini.
Mzee Yussuf aliyefariki akiwa na umri wa miaka 69,aliwahi kuwa mkuu wa polisi wa wanamaji mkoa wa Mwanza miaka ya 1980 kabla ya kuhamishiwa Zanzibar.

source:bongo5

Irene Uwoya amgeuzia kibao Flora Mvungi

Leave a comment


Vita vya maneno kati ya waigizaji wa filamu nchini Flora Mvungi na Irene Uwoya jana vimechukua sura mpya.
Wiki iliyopita tuliandika habari kuhusiana na Flora kutofurahishwa na kitendo cha Irene kuongea na vyombo vya habari na kusambaza shutuma kuwa mpenzi wake wa zamani H.Baba hajui mapenzi.
Jana Irene Uwoya aliongea na Clouds Fm na kusema Flora na H.Baba wamemchokoza.
Alisema yeye pia anamshangaa Flora kwa kupakaza maneno kuwa aliongea na magazeti ‘kumvua nguo mpenzi wake wa zamani H’Baba kuwa ni zezeta kitandani kitu ambacho alikanusha kukisema.
Irene alisema kwanza anamuona Flora ni mshamba na kumfananisha na ‘vocha’ na kamwe sio saizi yake.
Aliongeza kuwa yeye si mtu wa kutembea na H.Baba na kudai kuwa wako pamoja na Flora kwakuwa wote ni washamba na wote amewafananisha na vocha.
‘Sasa leo nasema kuwa kweli H.Baba hajui mapenzi, hana lolote, ni tegemezi na simtaki,alisema.
Akiongea kwa jaziba, Irene aliongeza kuwa yeye yupo level zingine na anawadharau wapenzi hao.

Adele: Kupata ujauzito wa Simon Konecki!!

Leave a comment


Adele na Simon Konecki wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza. Ijumaa hii Adele mwenyewe alikiri kuwa wanatarajia kupata mtoto wao wakwanza na Simon Konecki, dada huyo ambaye ni mshindi wa Grammy aliwaambia mashabiki wake kwenye website yake kwa kuwa andikia habari kuhusu ujauzito huo na kutumia kichwa cha habari kinacho sema “I’ve Got Some News”
Simon Konecki ambaye ana umri wamiaka 38, ambaye ana mtoto wakike na vilevile yeye na mkewe wazamani walitalakiana January. Febuary Simon alimsindikiza Adele kwenye tuzo za Grammys ambapo kipindi hicho adele Mwenye umri wa miaka 24 alisema malengo yake nikuwa na watoto wa kiume watatu kabla hajafikia umri wa miaka 30. Na ujauzito huu unaonyesha kweli kuwa yupo tayari kutimiza malengo yake.
Adele “I really want to be a mum,” she said. “I better start getting on with it!”

source:thehollywoodgossip

Older Entries

%d bloggers like this: