Home

AFUMANIWA AKIFANYA MAPENZI NA NG’OMBE

Leave a comment


hii sio picha halisi ya aliyefumaniwa

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Tumsifu Mwambusi (20),mkazi na mkulima wa Kijiji cha Mwela,Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya amefumaniwa akimbaka ng’ombe.

Tukio hilo la ajabu yake limetokea Julai 15 mwaka huu majira ya saa mbili za usiku ambapo jamaa huyo alikwenda kwenye makazi ya Bwana Leonard Mwangwemba,kisha kuingia ndani ya zizi na kuanza kumbaka ng’ombe huyo hali iliyopelekea ng’ombe huyo kuanza kupiga kelele kwa kuomba msaada.

Ndipo wakazi wa eneo hilo walielekea eneo la tukio na kumkuta kijana huyo akiendelea na kitendo hicho na kumshushia kipigo cha mbwa mwizi mara baada ya kuvunja amri ya sita ya kuzini na ng’ombe huyo.

Aidha,kufuatia hali hiyo Kijana Mwambusi aliomba msamaha kwa kitendo hicho lakini wananchi hao hawakujali na mara akajikuta akimwagiwa maji ya baridi na kipigo kikiwa kinaendelea na kusababishiwa maumivu sehemu mbalimbali ya mwili wake.

Hata hivyo wazazi wa kijana huyo walijaribu kutoa kiasi cha shilingi 100,000 kwa wananchi hao ili waweze kumwachia kijana wao kufuatia kipigo alichokuwa akipewa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Andongwisye Mwakalinga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amewasihi wananchi hususani vijana kumwomba mungu muda wote ili kuondokana na majaribu yasiyompendeza Mwenyezi Mungu.
Imeandikwa na Bosco Nyambege, Mbeya

source:jaizmelaleo

MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA CCM (UVCCM) AUAWA SINGIDA.

Leave a comment


Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,Linus Vicent Sinzumwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya mauaji yaliyofanywa na wafuasi wa CHADEMA. (Picha na Nathaniel Limu).

Jeshi la polisi mkoa wa Singida, linawashikilia wakazi 18 wa kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi,kwa tuhuma ya kumuua mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM (UVCCM),Yohana Mpinga (30) baada ya kumpiga kwa kutumia silaha za jadi.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Singida, Linus Vicent Sinzumwa alisema tukio hilo la kusikitisha limetokea julai 14 mwaka huu saa kumi alasiri huko katika kijiji cha Ndago.

Alisema siku ya tukio,Chama Cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) kilikuwa na kibali halali cha kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji hicho cha Ndago na mgeni rasmi katika mkutano huo,alikuwa mbunge wa jimbo la Ubungo jijini Dar-es-salaam.

Sinzumwa alisema mara baada ya CHADEMA kuanza mkutano huo,viongozi wake walianza kuporomosha mvua ya kashifa mbalimbali dhidi ya mbunge wa jimbo hilo Mwingullu Nchemba, kitendo ambacho kiliudhi baadha ya watu waliokuwa wamehudhuria mkutano huo.

“Wananchi hao ambao walichukizwa na kitendo cha kukashifiwa mbunge wao,walianza kupiga kelele kuwa hawataki mbunge wao akashifiwe na badala yake wanataka kusikia sera za CHADEMA tu na si vinginevyo.Hata hivyo,viongozi hao waliendelea tu kuporomosha kashifa dhidi ya Mwingullu na kusababisha kuanza kwa vurugu”,alisema.

Kamanda huyo alisema kuwa vurugu hizo zilihusisha kundi la wanachama wa CHADEMA na wa CCM na zilisambaa.Wanachama hao walianza kurusha mawe ovyo na askari wachache wa polisi waliokuwepo,walizidiwa nguvu na makundi hayo.

“Huyu mwenyekiti wa vijana CCM Yohana,yeye akikimbilia kwenye nyumba ya mwalimu Shume Manase Mpinga ili kuokoa maisha yake,lakini kundi la wananchama wa CHADEMA wakiwa wamebeba fimbo na mawe,walimpiga sehemu mbalimbali za mwili wake na kusbabisha kifo chake papo hapo”,alisema kamanda Sinzumwa kwa masikitiko makubwa.

source:dewjiblog.

Lissu sasa matatani

Leave a comment


MNADHIMU wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu ameingia matatani kutokana na kauli yake kwamba Rais Jakaya Kikwete amekuwa akiteua majaji wa Mahakama Kuu wasiopendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama.

Kutokana na kauli hiyo aliyoitoa wakati akiwasilisha maoni ya kambi yake, kuhusu hotuba ya makadirio ya matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria, Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) atajadiliwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Wakati akisoma hotuba yake, mbunge hiyo alisema majaji wanaoteuliwa na Rais hawafanyiwi ‘vetting’ (uchunguzi) na tume hiyo kuona kama uwezo na ujuzi wao unafaa kukabidhiwa madaraka ya ujaji.

Mwenyekiti wa Bunge, Jenista Mhagama ndiye aliyeamuru suala la Lissu kupelekwa katika kamati hiyo baada ya mbunge huyo kukataa kufuta kauli yake ambayo kwa mtazamo wa Serikali iliwadhalilisha majaji.

Hata hivyo, jana alipotakiwa kueleza kama ana taarifa rasmi za kuitwa kwenye kamati hiyo Lissu alisema: “Sijaitwa, lakini nina taarifa kuwa naweza kuitwa.’’

Alisema, hata wakimwita hatakuwa na jambo lolote la kuzungumza kwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge aliyeongoza kikao hicho juzi (Jenista Mhagama), alikosea kwa kuwa ndiye aliyepaswa kumpa adhabu.

Mbunge huyo alisema juzi aligoma kufuta kauli yake kama alivyotakiwa na Mwenyekiti kwani aliamini kuwa hata Mwanasheria Mkuu alikuwa amekosea.

Alibainisha kuwa endapo ataitwa katika kamati hiyo, atahoji kama waliomwita wamegeuka kuwa wenyeviti wa Bunge na kama si hivyo, anaamini watakosa neno la kumhoji.

Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kwa nyakati tofauti wakati wakijibu hoja za wabunge juzi jioni walisema: “Lissu aliwakashifu majaji bungeni, hivyo alipaswa kuomba radhi.”

Kwa upande wake Werema alimtaka Lissu kufuta kauli yake na kwamba ikiwa hatafanya hivyo basi awasilishe vielelezo vinavyothibitisha madai kwamba majaji huteuliwa bila kufanyiwa uchunguzi.

“Lissu ni mtaalamu wa sheria, lakini kauli yake imewafedhehesha majaji na inashangaza inapotolewa na wakili machachari kama yeye,” alisema Werema.

Werema pia alimtaka Lissu kuondoa kauli yake kwa kuwataja watu ambao sio wabunge kwa kunukuu gazeti la Mwanahalisi lililowataja watu watatu kuwa wamehusika na mauaji ya Dk Steven Ulimboka.

Werema alisema iwapo Lissu hataondoa maneno yake suala hilo lipelekwe katika Kamati ya Maadili.

Kwa upande wake, Chikawe alimwombea radhi Lissu kwa majaji akisema anajua hakutoa kauli ya kuwadhalilisha majaji kwa kukusudia.

“Lissu amemtuhumu hadi Rais katika uteuzi wa majaji, hili siyo sahihi, uteuzi wa majaji hupendekezwa na tume maalumu inayohusisha majaji wazoefu ambao ndio wanapendekeza majina kwa Rais,” alisema Chikawe.

Baada ya maelezo hayo, Mhagama aliamuru Lissu kuondoa kauli yake hiyo baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Werema wakati akifanya majumuisho ya mjadala wa wizara hiyo.

Hata hivyo, Lissu alipopewa nafasi alisema hawezi kuondoa kauli yake kwa kuwa mchakato mzima wa kumtaka afanye hivyo haukufuata Kanuni za Bunge.

Lissu alinukuu kanuni ya 63 (1) ambayo inasema: “Bila kuathiri masharti ya Ibara ya 100 ya Katiba yanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika Bunge, ni marufuku kabisa kusema uongo bungeni kwa sababu hiyo, mbunge yeyote anapokuwa akisema bungeni ana wajibu wa kuhakikisha kwamba anatoa kauli au maelezo kuhusu jambo au suala ambalo yeye mwenyewe anaamini kuwa ni kweli na siyo jambo la kubuni au la kubabaisha tu”.

Lissu aliongeza kuwa, Jaji Werema na Mhagama walivunja Kanuni za Bunge kwa kumtaka kuondoa kauli inayodaiwa kuwa ya uongo kinyume bila kufuata utaratibu.

Alipoulizwa kuhusu utekelezaji wa hatua hiyo jana, Mkuu wa Serikali Jaji Fredrick Werema alisema kuwa siyo lazima kwa Watanzania kufahamu hilo.

“Nilipozungumza jana (juzi) sikuzungumza na Watanzania bali nilizungumza na Bunge, hivyo siyo lazima Watanzania kufahamu jambo hilo na wala sioni sababu za kwa nini liandikwe magazetini,’’ alisema Jaji Werema.

source:mwananchi.

Vox Media: Utendaji mbovu umemuondoa Dr. Asher Rose Migiro UN

Leave a comment


Wiki hii aliyekuwa naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa Dr.Asha Rose Migiro amerejea nchini baada ya kuutumikia kwa miaka mitano.
Hata hivyo shirika la habari la Vox Media limebaini sababu za kwanini Dr. Migiro hakuongezewa muda wa kufanya kazi kwenye umoja huo.
Limesema vyanzo vya ndani ya UN vimesnitch kuwa utendaji dhaifu na kushindwa kufit kwenye chombo hicho kigumu ni baadhi ya sababu ya kushindwa kuongezewa mkataba wa kufanya kazi humo.
“Nafasi ya Unaibu katibu mkuu ni ngumu mno; inahitaji mtu mzoefu kuongoza vema Secretariat. Changamoto yake kubwa ilikuwa ni kuelewa siasa katika chombo hicho cha kimataifa na kuunda muungano,” chanzo kimoja kiliiambia Vox Media.
Inadaiwa kuwa Dr. Migiro alizungumza na kundi la waafrika lenye asilimia 28 ya wajumbe wa umoja wa mataifa ili achaguliwe tena lakini walimtosa.
“Hakuwa maarufu miongoni wa wanadiplomasia. Hakuna aliyemsikiliza. Unaweza kukumbuka pia kuwa uteuzi wake ulikosolewa sana,” kilisema chanzo hicho.
Katika hatua nyingine Dr. Migiro alisema hana mpango wa kuwania urais wa Tanzania na huenda akarejea kwenye kazi yake ya zamani ya uhadhiri wa chuo kikuu.

CHARLIE SHEEN: Kuwa Jaji wa American Idol Season 12

Leave a comment


Charlie Sheen ameiambia blog ya TMZ, kuwa yupo 100% katika bodi ya najaji kwenye msimu ujao wa “American Idol”>> lakini kuna masharti machache wanatakiwa kuyafanya kabla hajatia saini ya kuku bali kuwa jaji.

Kama TMZ walivyo Sema  kuwa Executive Producer Nigel Lythgoe, aliwaambia kuwa angependa kuwa Charlie Sheen na Jerry Lewis kama majaji kwenye Msimu ujao wa “American Idol season 12”. Nigel asingesema kama angekuwa anatania, inasemekana alikuwa anarudi rudi katika mazungumzo na TMZ kuwa angependa watu hao wawepo msimu ujao

Na haya ndio masharti yake Charlie Sheen

CONDITION #1.  Charlie says FX — the network that airs his show “Anger Management” — must sign off on an “Idol” deal … but Jennifer Lopez proved, being on A.I. can be good for business.

CONDITION #2.  Charlie says the money has to be right:  “If the numbers move the needle AND ‘Idol’ matches 20% of my weekly salary for Autism Speaks, JDRF, and the Boys and Girls Club … then the hell with it. As we say, pour the smoke.”

That’s Charlie-speak for “Why the hell not?”

As for Jerry Lewis, he’s in Nashville directing a stage play of “The Nutty Professor” and was not available for comment.

sourcetmz.

SIMBA, AZAM FC SASA KUKIPIGA UWANJA WA TAIFA

Leave a comment


MECHI ya fainali ya kombe la Urafiki baina ya Simba na Azam Fc sasa litapigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, imefahamika.
Awali mechi hiyo ilipangwa kufanyika siku ya Alhamis kiwenye uwanja wa Aman Visiwani Zanzibar lakini baada ya majadiliano ya uongozi wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) na uongozi wa Simba na Azam wamekubaliana kulihamishia jijini Dar es Salaam.
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema mchana huu kwamba kikosi chao kipo tayari kwa mchezo huo na kitahakikisha kinashinda mchezo huo na kutwaa yubingwa.
Kamwaga alisema, kupitia michuano hiyo, Kikosi cha Suimba kimeweza kuimarika ipasavyo kadiri siku zinavyosonga hivyo ni wazi kwamba ubingwa utabaki Msimbazi.
ALisema mchezo huo unatarajiwa kuanza kupigwa saa moja usiku.

source:dinaismail.

BAADA YA RAIS JOYCE BANDA KUSAMEHE WAFUNGWA 400, WALIOBAKI GEREZANI WAFANYA GHASIA.

Leave a comment


Wafungwa kwenye gereza moja ya Malawi wamefanya ghasia kupinga msamaha waliopewa baadhi ya wafungwa wenzao, ambao wanaona haukuwa wa haki.
Rais Joyce Banda (Pichani), siku ya Ijumaa aliwasamehe wafungwa karibu 400, lakini siyo wale waliofungwa kwa sababu ya mauaji au ubakaji.
Wafungwa katika gereza la Zomba walitoroka na kuwabughudhi wasimamizi, wakisema wafungwa wawili waliosamehewa ni wahalifu wa mauaji na ubakaji.
Bibi Banda alisema wabakaji wanafaa kufa jela, hasa wale waliowabaka watoto.
Ubakaji wa aina hiyo unatokea mara kadha Malawi, kwa sababu kuna wanaoamini kuwa kufanya mapenzi na msichana bikira kunaleta mali na kunatibu HIV na UKIMWI.

Older Entries

%d bloggers like this: