Home

KUTANA NA BINADAMU WA KWANZA ANAYEISHI BILA MOYO WALA KUWA NA MAPIGO YA MOYO.

Leave a comment


Mwaka jana mwezi wa tatu, Bwana Cgraig Lewis, 55.  Alikuwa anatarajia kufa kwa matatizo ya moyo, yaliosababishwa na kuwa na uwingi wa protein mwilini, ambapo hata hospital kuwa huko ugaibuni hazikuweza kuja na utatuzi wa tatizo lake.

Ndipo madaktari wawili kutoka Texas Heart Institute walipendekeza na ufumbuzi wa tatitizo lake, waliutoa moyo wake na kumwekea kifaa mfano wa pump ambacho kitamsaidia kusukuma damu mwilini mwake.

 

Kifaa hicho kwa mujibu wa madaktari na mashahidi waliopata kuzundumza na Bwana Craig Lewis, ni kwamba ukisikiliza kwa karibu au kwa kifaa cha kusikilizia mapigo ya moyo ulikuwa unasikia sauiti mfano wa pump ndogo…

Picha ya moyo mpya wa Bwana Craig Lewis

Picha ya X-ray Baada ya kufanikiwa kwa Operesheni. hapo chini.

Video ya jinsi maisha ya Bwana Craig Lewis yalivyoweza kunusuriwa na Madaktari hawa watata.

Photo source

MNYIKA: Msimamo wangu wa sasa juu ya Kauli yangu!

Leave a comment


John Mnyika akisindikizwa na askari wa bunge. (picha kutoka issamichuzi.blogspot.com)

Mbunge wa jimbo la Ubungo kupitia tiketi ya CHADEMA, John Mnyika ametolewa Bungeni na Naibu Spika, Job Ndugai kwa kile kilichodaiwa kushindwa kufuta kauli yake ya kumuita Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa ni mtu dhaifu.
Msimamo wangu wa sasa juu ya Kauli yangu!

Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.

Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!

source:mrokim.blogspot

Miss Dar Intercollege 2012 ,kusugua kisigino na Twanga kesho Club Billcanas

Leave a comment


WAREMBO wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss dar Intercollege 2012 jumatano ya keshjo wanatarajiwa kujivinjari katika ukumbi wa kimataifa wa Club Bilicanas iliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Shindano hilo limepangwa kufanyika Ijumaa ya Juni 22 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambapo msanii wa bongo Fleva Nasib Abdul ‘Diamond’ anatarajiwa kutumbuiza.
Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail amesema leo kwamba, warembo hao watapata kuhudhuria onyesho maalum la bendi ya African Stars “twanga Pepeta’ kupitia usiku wa Mwafrika unaorindima kila jumatano katika klabu hiyo.
Dina alisema uongozi wa Bilicanas Group umewaalika warembo hao ili kuweza kuburudika pamoja na mashabiki wa muziki wa dansi nchini kwa lengo la kujipoza baada ya mazoezi yao.
“Warembo wetu wamealikwa kesho pale Bilicanas ambapo bendi ya Twanga Pepeta hutumbhuiza kila Jumatano kupitia usiku wa Mwafrika, hivyo tunaoomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwashuhudia kabla ya kuja tena Ijumaa katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa,”Alisema
Alisema maandalizi ya shindano hilo yanakwenda vema ambapo warembo 14 watakaoshiriki wanaendelea na mazoezi katika hoteli ya The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam
“Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina.
Warembo watakaoshiriki shindano hilo wanatoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss Tanzania.
Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Shindano hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s,Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band,Lamada Hotel, Screen Masters,Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada Hotel,Grand Villa Hotel, Sporti Kizaa zaa, Clouds Fm na blog za Michuzi, Dinaismail(zamani Mamapipiro), Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaa na Fullshangwe.

BBA7 Stargame: Goldie amwokoa Prezzo dhidi ya Nomination ya kutolewa

Leave a commentWiki hii kwenye Jumba la Big Brother Africa, Goldie alishinda zoezi la mwanzo wa wiki na kumfanya awe mkuu wa nyumba (HoH) kwa wiki moja. Hiyo ina maana kuwa unapokuja muda wa nomination , atakuwa na nafasi ya kumwokoa mtu mmoja na kumbadilisha na mwingine.
Bahati mbaya ni kuwa washiriki wengine wa shindano hilo wameanza kumwekea mtimanyongo mfalme wa viwalo wa Kenya, Prezzo kwa kumtaja zaidi atoke wiki hii.
Asilimia 41 za kura zote zilimwangukia yeye na hivyo kuhatarisha ukaaji wake kwenye mjengo huo wa BBA.
Biggie aliposoma majina ya wale watakaokuwa hatarini kutoka, Goldie alishangaa na kuvuta pumzi na kuitoa nje kwa mshtuko baada ya kusikia jina la mpenzi wake Prezzo limo. “Oh my God,” alisikika akisema.
Licha ya huzuni iliyojidhihirisha kwenye sauti yake, muda ulipofika wa kumtaja atakayemwokoa, hakufikiria mara mbili zaidi ya kumtaja Prezzo.
Reaction yake baada ya kusikia jina la Prezzo kuwa limo kwenye orodha ya watakaokabiliwa na eviction week hii na kitendo cha kumwokoa, kinaashiria kuwa kweli mrembo huyu wa Nigeria amekufa na kuoza kwa mnyamwezi Prezzo.
Huu ni wakati sasa wa Prezzo kuacha kumchukulia poa kama alivyofanya wiki kadhaa zilizopita kiasi cha kumfanya Goldie akatae kula na kuhofiwa huenda akataka kujuia.

Diamond kununua Gari lake Aina ya LandCruse Prado

1 Comment


Picture source:thisisdiamond

MWIGIZAJI JACKLINE WOLPER AONGELEA KUHUSU KUNYANGA’NYWA GARI AINA YA BMW X6

Leave a commentkatika stori za town sasa hivi ni kwamba Mwigizaji Jackline Wolper amenyanga’nywa gari ambalo ameonekana nalo kwenye misele mbalimbali Dar es salaam.

Kupitia blog yake J ameamua kujibu hizo stori ambazo zinadai kanyanga’nywa gari na mwanaume aliempatia. Kasema “Uvumi unaonea kwenye mitandao kuwa nimenyang’annywa gari sio kweli. wakati naendesha Noah watu kimya, Lexus hakuna aliyesema nimenyang’anywa, inakuaje X6? Kuna ajabu gani mimi kuendesha X6? Wanawake tusijishushe kuonekana vitu fulani hatuwezi kumiliki”

“Nasikitika sana kusikia watu wanavumisha maneno kama hayo. Hivi inakuaje mtu unanyang’anywa gari yako mwenyewe? Nina kila uthibitisho wa kuonesha hii X6 ni yangu na hakuna atakayeweza kuninyang’anya” – J Wolper

Source:millardayo.com

ZAMARADI MKETEMA AONGELEA KUHUSU ISHU YA NYUMBA YA WEMA SEPETU.

Leave a comment


Muda mfupi baada ya mwigizaji Wema Sepetu kuonyesha nyumba yake mpya ya milioni 400 kwenye kipindi cha Take One Clouds Tv baadhi ya wabongo walianza kutoa maoni kwamba hiyo nyumba sio ya Wema, haiwezekani akamiliki nyumba ya namna hiyo.

Haikuishia hapo tu, hata baadhi ya magazeti yalifichua siri kwamba mmiliki wa hiyo nyumba sio Wema ni mama mmoja ambae ni mmiliki wa hospitali moja Dar es salaam.

Lawama za wachache pia zilitolewa kwa Zamaradi Mketema kwamba ameitoa hiyo stori huku akijua sio kweli inamilikiwa na Wema.

Zamaradi ameamplfy na millardayo.com kwa kusema “mimi ni Mwandishi, unapokwenda kufanya interview na mtu ninachotakiwa kusikiliza ni kile ninachoambiwa na mtoa habari lakini sio ninachokijua au kusikia kwa watu, nilimuuliza hii nyumba ni yako? akajibu kweli yeye ndio mmiliki sasa siwezi kubisha, magazeti yanakosea kusema mimi naipotosha jamii ya watanzania… sijaipotosha na kama kweli ile sio nyumba yake mimi sitakiwi kulaumiwa”

Kwenye sentensi nyingine Zamaradi amesema “kwenye show ya Take One ndani ya wiki mbili zijazo Wema amekubali kwamba atautoa uthibitisho kuonyesha kwamba ni mmiliki halali wa hiyo nyumba japo siwezi kuutaja ni uthibitisho gani”

source:millardayo.

Older Entries

%d bloggers like this: