Home

SIMBA SC YAIBUKA MABINGWA WA KOMBE LA URAFIKI.

Leave a comment


Waziri asiye na Wizara maalum Zanzibar Mh. Machano Othman Said akimkabidhi kombe la ubingwa wa michuano ya Urafiki nahodha wa timu ya Simba Juma K. Juma mara baada ya timu ya Simba kuifunga timu ya Azam FC magoli 5-3 kwa penati, baada ya kutoka suluhu magoli 2-2 katika kipindi cha dakika tisini, kwenye mchezo mzuri na wa kuvutia kwa timu zote na hivyo kuifanya Simba kuibuka mabingwa wa kombe hilo.(Picha na Fullshangwe Blog).

Mabingwa wa Tanzania Bara klabu ya Simba SC imeibuka bingwa wa kombe la Urafiki (ujirani mwema) baada ya kuifunga timu ngumu ya Azam FC kwa bao 4 – 3 kwa njia ya mikwaju ya penati.
Mchezo huo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ulikuwa wa vuta nikuvute ambapo hadi timu hizo zinakwenda mapumziko mabao yalikuwa ni 1-1, ambapo kwa upande wa Simba goli lilifungwa na Felix Sunzu na Khamis Mcha aliisawazishia Azam FC.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu hizo kushambuliana ambapo mchezaji John Boko aliipatia Azam FC goli la pili kabla ya ksawazishwa na kiungo bora wa Simba Mwinyi Kazimoto.
Baada ya mechi hiyo kumalizika timu hizo zikiwa sare ya bao 2-2 ndipo ilipotumika mikwaju ya penati kuamua nani atakuwa bingwa wa Kombe la Urafiki, ambapo Simba ilitawazwa kuwa bingwa kwa kupata penati 4 dhidi ya 3 za Azam.

source:/dewjiblog.

WEMA AITWA IKULU

2 Comments


Wema Isaac Sepetu.

WEMA Isaac Sepetu amelidokeza gazeti alipendalo la Ijumaa Wikienda kuwa ameitwa ikulu ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza kwa mwaliko maalum.
Wema alisema mwaliko huo aliupata mara tu baada ya kuzindua ile filamu yake ya Super Star wiki mbili zilizopita ambapo katika mwaliko huo wa ujumbe kutoka ikulu hiyo ulimuomba kutoisambaza kwanza kabla ya kwenda kuizindua nchini humo.
“Waliniambia juu ya mimi kuomba uraia wa nchi hiyo ili kukuza filamu zao. Kusema kweli nilikuwa nina ratiba ya kwenda kuizindua filamu yangu Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Yaani sijui hata walijuaje. Sijui ni nini kimetokea, nina wasiwasi. Hata sijui nitaongea nini na Rais wa Burundi,” alisema Wema na kuongeza kuwa maandalizi yakikamilika atatii wito huo muda wowote

source:globalpublishers.

Ziara ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Washington DC

Leave a comment


Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wameanza ziara ya siku mbili Washington DC, kuanzia tarehe 2 – 4 Julai 2012. Pichani, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowassa (Mb.) akiweka saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwneye ubalozi wa Tanzania Washington DC.

Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Lilly Munanka akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowassa (Mb.) kwenye ofisi za ubalozi

Kaimu Balozi wa Tanzania Mhe. Lilly Munanka akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama walioanza ziara ya siku mbili Washington DC

Baadhi ya wafanyakazi wa ubalozi wakipata picha ya pamoja na wajumbe wa kamati hiyo

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Edward Lowassa (Mb.)akifuatilia taarifa kutoka Ubalozi wa Tanzania Moscow, kutoka kwa mjumbe wa kamati hiyo Mhe. Vita Kawawa aliyejumuika na msafara huo akitokea Moscow.

source:father kidevu

Ray Azindua Filamu kwa Kutoa Msaada Kwa Yatima

Leave a comment


Kampuni ya usambazaji wa filamu za kitanzania Steps Entertainment ya Jijini Dar-Es-Salaam ikishirikiana na Msanii wa filamu wa Bongo Movies, Vincent Kigosi almaarufu kama Ray, wametoa Msaada wa vitu mbali mbali kwenye kituo cha watoto yatima cha Maunga Center kilichopo maeneo ya Kinondoni ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa filamu yake mpya.

Msaada huo ni sehemu ya mpango wa matukio ya uzinduzi wa filamu yake ‘Sobing Sound’ na pia kurudisha fadhila kwa jamii ambayo ndio wateja wakubwa wa filamu za kitanzania.

Filamu hiyo imezinduliwaa kwa staili tofauti ambapo badala ya kuzindua ukumbini kama ilivyozoeleka na wasanii wengi, msanii huyo ameamua kuzindua filamu hiyo katika kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh. Milioni 1.5.

Akizungumza na http://www.bongo5.com mara baada ya kuzindua filamu hiyo, akiwa pamoja na watoto yatima wa kituo hicho, Ray, ambaye pia aliongozana na afisa masoko wa kampuni ya steps,bwana Ignatusu Kambarage ,alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na ukweli kwamba watu wengi wamekuwa wakifurahia maisha huku wengine wakiendelea kutaabika, kitendo ambacho amesema, si kizuri.


Alisema ujio wa filamu hiyo ni kama azma yake aliyoipanga tangu awali kuhakikisha filamu zake zote zinafanya vizuri ,na atahakikisha japo kidogo,kwa namna yoyote anawakumbuka watoto yatima, kwani anawapenda.

“Hii ni filamu ya kwanza kutoa, tangu kifo cha mwigizaji mwenzangu Steven Kanumba alipofariki dunia, Aprili mwaka huu, na najisikia furaha kuja hapa na kutoa msaada kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu” alisema Ray

source:bongo5

NGORONGORO HEROES KUJIPIMA KWA MISRI, RWANDA

Leave a comment


Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) itacheza mechi nne za kirafiki na timu za Misri na Rwanda kabla ya kuivaa Nigeria kwenye mashindano ya Afrika.
Ngorongoro Heroes ambayo kwa mara ya kwanza itakuwa chini ya kocha mpya Jakob Michelsen itaanza kwa kucheza mechi mbili za Misri zitakazofanyika Julai 3 na 5 mwaka huu, na baadaye Julai 14 na 16 mwaka huu dhidi ya Rwanda.
Mechi zote zitachezwa nchini, na kama ilivyo Ngorongoro Heroes, Misri na Rwanda nazo ziko kwenye kinyang’anyiro cha kusaka tiketi za kucheza Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 zitakazofanyika mwakani nchini Algeria.
Katika raundi ya kwanza, Ngorongoro Heroes iliitoa Sudan ambapo katika raundi ya pili imepangiwa Nigeria, na mechi ya kwanza itafanyika jijini Dar es Salaam, Julai 29 mwaka huu. Timu hizo zitarudiana wiki mbili baadaye nchini Nigeria.
Iwapo Ngorongoro Heroes itafanikiwa kuitoa Nigeria, katika raundi ya mwisho itacheza na mshindi kati ya Congo Brazzaville na Afrika Kusini.

Kanumba apelekwa sabasaba

Leave a comment


FAMILIA ya msanii wa filamu za Swahiliwood, Steven Kanumba, imeamua kuuza bidhaa za marehemu katika uwanja wa maonyesho wa Sabasaba uliopo Temeke katika kujenga utaratibu wa kumbukumbu dhidi yake.

Bidhaa za marehemu Kanumba kama aina ya nguo alizokuwa akipenda kuvaa, filamu alizowahi kuigiza, picha zake zitaonyeshwa katika maonyesho ya Sabasaba mwaka huu, familia ya marehemu imechukua banda kwa ajili ya maonyesho hayo ambayo yatakuwa ya aina yake kufanyika katika uwanja huo, anasema Magulu.

Katika banda hilo pamoja na kuona bidhaa za msanii huyo lakini pia kwa wale watakaolitembelea, watapata fursa ya kuongea na wanafamilia kama Seth Bosco mdogo wa marehemu aliyekuwa naye karibu sana, Mama yake mzazi, wafanyakazi wa kampuni yake.

Alisema hiyo itakuwa fursa nzuri kwa watakaotaka kujua mengi yamhusuyo Kanumba.

Kanumba alifariki miezi miwili iliyopita katika kifo kilichojaa utata huku msanii mwingine, Elizabeth Michale ‘Lulu’ akikabiliwa na kesi inayomtuhumu kuhusika na kifo hicho kilichotokea mara baada ya wawili hao kuzozana chumbani kwa Kanumba.

Wezi wamfanyia kitu mbaya MwanaFA

Leave a comment


“Next time nikikuta watu wanapiga mwizi na mtu akanizuia nisishiriki ntaanza na yeye kwanza” ni tweet ya jana ya Hamisi Mwinjuma aka MwanaFA iliyokuwa imeambatanishwa na picha ya gari lake lenye namba T 809 PMB ikiwa imenyofolewa taa zote za mbele na nyuma.

Wizi huo umefanyika usiku wa kuamkia jana na inavyoekena ni kuwa wezi walipanda na kuvuka geti kimya kimya, kwa raha zao wakanyofoa taa na kuingia ndani kuchukua radio.

Ile MwanaFA kuamka asubuhi ndo akakuta tayari wajanja wameshamliza kiasi cha kuamua kutangaza vita na wezi. Hivyo kama ukikuta MwanaFA anashiriki kumponda ‘vitofa’ mwizi aliyekamatwa street baada ya kuiba, kamwe usishangae, usimuulize na usimzuie sababu ataanza na wewe! Pole sana Binamu!

Hata hivyo wezi hao hawaikuiharibu ratiba ya usiku wa kuamkia leo ya Binamu. Ratiba yake ilianzia pale the so-called ‘Uwanja wa taifa wa burudani’ Dar Live ambapo aliperform ngoma yake mpya Ameen kwa mara ya kwanza.

Baada ya Dar Live show ikahamia Maisha Club, “Dar Live Done..Beautiful..Maishani Sasa Kwa Ndege Mnana,” alitweet.

Huko New Maisha Club alienda kumpa support mwanadada Linah Sanga aliyekuwa akifanya show yake ya kwanza tangu arudi kutoka kwenye ziara ndefu ya nchini Marekani. “What a show..Maisha I Loooooooooved you tonite!” aliandika alfajiri hii.

source:bongo5

Older Entries

%d bloggers like this: