Home

RAIS WA ZAMANI WA MISRI HOSNI MUBARAK AREJESHWA GEREZANI.

Leave a commentRais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak amerejeshwa gerezani baada ya kupata matibabu hospitalini.
Mwendesha mashitaka wa umma nchini humo ameamuru kuwa afya ya Mubarak mwenye umri wa miaka 84 imeimarika na kwamba hapaswi tena kuendelea kuwa katika hospitali ya kijeshi.
Mubarak anatumikia kifungo cha maisha gerezani kutokana na mauaji ya waandamanaji wakati wa wimbi la mageuzi katika ulimwengu wa kiarabu ambalo lilianza mwezi wa Januari mwaka wa 2011.
Hosni Mubarak aliondolewa madarakani wakati wa vuguvugu hilo la umma na kuumaliza utawala wake wa miaka 30 nchini Misri.

POLISI YAMNASA MTU MMOJA RAIA WA KENYA KWA KUHUSIKA NA SHAMBULIO DHIDI YA DKT. ULIMBOKA.

1 Comment


Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linamshikilia mtu mmoja raia wa Kenya kwa tuhuma za kuteka nyara na shambulio la kudhuru mwili dhidi ya Dkt. Stephen Ulimboka lilifanyika tarehe 26 Juni 2012. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum Suleiman Kova amesema mtu huyo aitwaye Joshua Gitu Mhindi mwenye umri wa miaka 31, ana kitambulisho cha utaifa Na.29166938 kilichotolewa Nyeri na hati ya kusafiria ya dharura Na.0123431 iliyotolewa Namanga Kenya. Kamanda Kova amesema katika mahojiano na polisi mtu huyo alieza kwamba yeye ni mwanachama wa kikundi cha kihalifu kinachojulikana kama GUN STAR chenye makao yake eneo la RUIRU wilaya ya Thika nchini Kenya na kudai kuwa kinaongozwa na mtu mwenye jina la utani SILENCE akisaidiwa na PAST, ambao wamekuwa wakifanya matukio mengi ya kihalifu nchini Kenya.Mtu huyo alipohojiwa zaidi alisema alikuja Tanzania na wenzake 12 kwa lengo la kumdhuru Dkt. Stephen Ulimboka baaada ya kukodiwa na mtu ambaye hakumtaja jina, ambaye anaamini kuwa ni mtumishi wa serikali.Polisi inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini wengine waliohusika

Hasheem Thabeet kusaini na kucheza kesho na Thunder

Leave a comment


Mchezaji wa mpira wa kikapu cha kulipwa katika ligi ya NBA ya Marekani, mtanzania Hasheem Thabeet kesho Jumatano, anatarajiwa kusaini mkabata rasmi wa miaka miwili kukipiga na timu ya Oklahoma City Thunder.
Kama akisaini kesho anaweza kucheza kwenye mechi tatu za mwisho akiwa na timu yake mpya kwenye Orlando Pro Summer League.
Thabeet hawezi kusaini rasmi mkataba wake mpya na Thunder hadi kesho pindi msitisho rasmi wa free agent huyo ukitolewa. Kabla ya hayo kufanyika, bado sio mchezaji wa kimkataba na timu ya Thunder.
Hata hiyo haimkatazi Thabeet kucheza kwakuwa wachezaji kumi kati ya 14 wa OKC kwenye roster ya summer league hawana mkataba na Thunder.
Lakini wachezaji hao kumi hawana siku moja tu zilizosalia ili kusaini mkataba unaohusisha malipo kama Thabeet.
Wachambuzi wa masuala ya mchezo huo nchini Marekani wanasema kuwa Thabeet anaweza kusaini mkataba huo kesho asubuhi kwa saa za Marekani na kuingia uwanjani rasmi.
Thabeet anatarajiwa kujiunga na timu yake wiki hii mjini Orlando na anaweza kushiriki kwenye mazoezi wiki hii yote na kama kesho akisaini mkataba hakutakuwa na chochote tena cha kumzuia kucheza.
Ni wachezaji wachache wanaohitaji muda wa kucheza kumzidi Thabeet, na ndo maana ni lazima acheze wiki hii.
Kwa misimu miwili iliyopita Thabeet amecheza kwa dakika 512 tu.

BAADA YA Z ANTO KUACHANA NA HUYU BINTI, ASEMA YUKO TAYARI KUOA TENA.

Leave a comment


Z anto

Wote tunafahamu kwamba Z Anto star wa hits kama Binti Kiziwi na Mpenzi Jini, alioa akiwa na umri wa miaka 22 tu tena siku chache baada ya video ya Binti kiziwi ilipotoka ambapo alimuoa mrembo alieuza kwenye hiyo video. Walikaa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda wa mwaka mmoja na kuoana kwenye ndoa ambayo haikumaliza mwaka mmoja, ilivunjika Miaka mitatu iliyopita. Z Anto anasema “niliamua kumuoa kwa sababu pesa ninazo mali ninazo na nikawa sipendi kuendelea kutenda dhambi, lakini tuliachana kwa sababu ya tamaa zake za kibinaadamu”

Huyu ndio mrembo alieonekana kwenye video ya Binti Kiziwi ambae ndio Z Anto alimuoa na wakaachana baadae.

“Kwa sasa niko tayari kuoa tena manake dini yangu inanilazimisha mimi kuoa, nina mtu ambae bado sijamchumbia na kwa bahati nzuri nimebahatika kupata nae mtoto pia aliezaliwa miezi mitatu iliyopita, plan yangu ni lazima nioe maishani kwa sababu kosa la mtu mmoja haliwezi kunifanya niwaadhibu watu 100, yeye nilimuadhibu na nimeshasahau pia… wakati namuoa alikua na umri wa miaka 20 na mimi nilikua na kati ya 21 au 22″ – Z Anto

source:millardayo

Hizi ni Picha 7 za Mtoto wa miaka 12 kutokea Nigeria kupewa mkataba na Sony Music

Leave a comment


Sony Music Entertainment imemsainisha mtoto mwenye kipaji cha hali ya juu aitwaye Kamsee aliye na miaka 12 kwenye roster ya wasanii wake.
Kamsee anaungana na wasanii wakubwa kwenye kampuni hii ya muziki ya pili kwa ukubwa duniani ikiwa na wasanii kama Beyonce,Usher, Britney Spears, Celine Deon, Chris Brown, Jordin Sparks, John Legend, Madonna, R.Kelly na wengine kibao.
Staa huyo mtoto atakuwa chini ya uangalizi na utayarishaji wa timu ya utayarishaji wa muziki ya Afrika Kusini iliyowahi kushinda tuzo za SAMA Jax Panik, ambao watatengeneza nyimbo zilizotungwa na Kamsee zitakazotoka mwaka huu.
Umaarufu wa Kamsee Ekpenyong, mwanafunzi wa Trinity International College, ya Ofada, Nigeria, ulianza baada ya kuonekana kwenye mtandao kwa nyimbo zake ‘Friends’ na Father In Heaven’ zilizoonesha kipaji chake.
Mkataba huu wa kufanya albam kadhaa na Sony Music Entertainment, pamoja na kuhudumiwa kila kitu na Sony Music pamoja na ROCKSTAR4000, ni wa kwanza kwa msanii mwenye umri kama wake katika nchi yoyote barani Afrika.
Paul Thackwray, Meneja mkuu wa Columbia / Epic upande wa Sony Music Africa,alisema: “Tunafurahi kumuunganisha Kamsee kwenye line-up ya wasanii wenye vipaji vya hali ya juu na tunategemea kuiendeleza career yake.”
Mpaka sasa mtoto huyo ambaye alianza kupiga piano akiwa na miaka mitano, ameshafanya show na wasanii wakubwa kama Wizkid, 2face Idibia na Stella Damasus

source:bongo5.

MSANIFU MAARUFU WA MAGARI YA FERRARI ITALI PININFARINA AFARIKI.

Leave a comment


Msanifu maarufu wa utengenezaji wa magari ikiwemo miundo ya Ferrari na Fiat Sergio Pininfarina (pichani) wa nchini Italia amefariki dunia nyumbani kwake katika mji wa Turin baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Pininfarina alisanifu miundo maarufu ya magari ikiwa ni pamoja na Ferrari, Fiat na Maseratis na pia magari aina ya Peugeot na Mitsubishi.
Sergio Pininfarina pia alikuwa mbunge wa bunge la Ulaya hadi mwaka wa 1988 na baadaye kukiongoza Chama cha Wafanyabiashara wa Italia.
Waziri Mkuu wa Italia Mario Monti amesema kuwa Pininfarina alizaliwa na kipaji cha kuleta pamoja uzuri na ubora katika kazi yake.
Sergio Pininfarina alizaliwa katika mji wa viwanda wa Turin Kaskazini mwa Italia na amefariki akiwa na umri wa miaka 85.

Nadia Buari akataa uvumi wa kurudiana na Michael Essien

Leave a comment


Muigizaji wa filamu wa kike nchini Ghana Nadia Buari, amekanusha taarifa za udaku kuwa ana mpango wa kurudiana na mpenzi wake wa zamani, mchezaji wa klabu ya Chelsea, Michael Essien.
Habari za kuwa wapenzi hao huenda wamerudiana zilienea kwenye internet wiki iliyopita baada ya kuonekana kwa picha zao wakibusu kwenye birthday party ya mtangazaji maarufu nchini Ghana wa Diva’s Show, Nana Aba Anamoah.
Nadia ambaye kwa sasa amejiingiza pia kwenye muziki, amezieleleza picha hizo kwa “innocent pictures” zilizopigwa kwenye party hiyo.
“Hakukuwa na kupigana busu; Essien na mimi ni marafiki lakini, hatuna issue kubwa sana. Lakini kuhusiana na ripoti kuwa tumerudiana, hakuna kitu kama hicho,” alisema.
Nadia aliendelea kueleza kwamba “tulikuwa tunajaribu kupiga picha na mapaparazi nao walikuwa wakipiga picha zao. Tulikuwa tupige picha mbili tu lakini wao waliendelea kuchukua picha nyingi na niliona aibu sana hivyo nilijaribu kumwacha Essien, nilitaka kuficha uso wangu tu.
Nadia na Essien waliachana miaka miwili iliyopita.

source:ghanacelebrities

Older Entries

%d bloggers like this: