Home

AJALI MBAYA YA BASI LA BUNDA IMETOKEA GEITA,WATU 11 WAFARIKI PAPO HAPO NA 12 WAJERUHIWA.

Leave a comment


MKUU wa mkoa wa Geita Magalula Said Magalula akiangalia miili ya marehemu waliokufa katika ajali ya Gari leo mchana Wilayani Geita,miili hiyo ilikuwa imelazwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya hiyo.Picha na David Azaria. (Source http://www.hakingowi.com/)

Watu wamefariki Dunia Papo hapo hapo na wengine 12 wakijeruhiwa vibaya baada ya magari matatu mawili kati yao yakiwa ni ya abiria waliyokuwa wakisafiria kupata ajali na kupinduka wilayani Geita Mkoani Geita.

Tukio hilo limetokea leo Jumapili majira ya saa 8:30 katika kijiji cha Chibingo kata ya Katoro eneo ambalo mwaka jana kulitokea ajali ya basi la Bunda na kuua watu 14 papo hapo na kujeruhi wengine 28.

Katika tukio hilo watu 9 wakiwemo watoto watatu wamekufa papo hapo,huku wengine wawili mmoja akifariki njiani wakati wa kukimbizwa hospitalini huku mwingine akifariki wakati akipatiwa matibabu na madaktari katika chumba cha Upasuaji.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Geita Paul Kasabago amelithibitihishia gazeti hili kuwepo kwa tukio hilo,na kueleza kuwa ajali hiyo ni mbaya nay a kwanza kutokea katika kipindi cha mwaka huu huku akitaja magari yaliyopata ajali kuwa ni zenye namba T 344 AZE zote aina ya Toyota Corola,na T 421 BHS Toyota land Cruiser.

Aliwataja waliokufa papo hapo katika ajali hiyo kuwa ni Maria Elisante (18) mkazi wa Mganza wilayani Chato,Masasila Benjamin (17) mkazi wa Mkolani mjini Geita,James Ntungirwenge (36) Mkazi wa Nyankumbu Geita,na Eliud Ngovongo (36) pamoja na watoto wake watatu Amin (10),Emison(7),na Sara(4) wote wakazi wa Kalangalala mjini Geita.

Alisema bado majina ya marehemu watatu mpaka jioni ya jana yalikuwa bado hayajatambuliwa,huku akibainisha kwamba tayari marehemu saba kati ya 11 waliofariki wametambuliwa na ndugu zao.

Kamanda Kasabago alisema katika tukio hilo watu 12 wamejeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya wilaya ya Geita,huku wanne kati yao ambao hali zao ilionekana kuwa mbaya wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi.

Mganga mkuu wa Wilaya ya Geita Dk.Abdalah Dihenga jana aliwaongoza madaktari wengine kutoa huduma kwa majeruhi,ambapo mwandishi wa Gazeti hili aliwashuhudia wakitoa huduma kwa wagonjwa katika chumba cha upasuaji hospitalini hapo.

Akisimulia tukio kamanda Kasabago alisema chanzo cha ajli hiyo mbaya ni mwendo kasi wa magari mawili madogo ya abiria yajulikanayo kwa jina la ‘Michomoko’ ambayo yaligongana uso kwa uso na gari linguine aina ya Land Cruiser.

Kamanda Kasabago alisema magari hayo mawili yalikuwa yakifukuzana kutoka mjini Geita kwenda Katika mji mdogo wa katoro huku yakiwa na abiria,ambapo baada ya kufika katika eneo hilomoja liliamua kulipita lingine na ghafla likakutana na gari linguine mbele.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Said Magalula alifika katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Geita,na kushuhudia miili ya marehemu iliyokuwa imelazwa chini katika chumba hicho.

Akizungumza na mamia ya wananchi waliokuwa wamefurika nje ya Viwanja vya jingo hilo la kuhifadhia maiti katika hopspitali ya wilaya hiyo Mkuu huyo wa Mkoa alitoa pole kwa wafiwa,na kuwataka kuwa na moyo wa subira wakati wa maombolezo ya vifo vya ndugu jamaa na marafiki zao.

source:dewjiblog.

MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA CCM (UVCCM) AUAWA SINGIDA.

Leave a comment


Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,Linus Vicent Sinzumwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya mauaji yaliyofanywa na wafuasi wa CHADEMA. (Picha na Nathaniel Limu).

Jeshi la polisi mkoa wa Singida, linawashikilia wakazi 18 wa kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi,kwa tuhuma ya kumuua mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM (UVCCM),Yohana Mpinga (30) baada ya kumpiga kwa kutumia silaha za jadi.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Singida, Linus Vicent Sinzumwa alisema tukio hilo la kusikitisha limetokea julai 14 mwaka huu saa kumi alasiri huko katika kijiji cha Ndago.

Alisema siku ya tukio,Chama Cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) kilikuwa na kibali halali cha kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji hicho cha Ndago na mgeni rasmi katika mkutano huo,alikuwa mbunge wa jimbo la Ubungo jijini Dar-es-salaam.

Sinzumwa alisema mara baada ya CHADEMA kuanza mkutano huo,viongozi wake walianza kuporomosha mvua ya kashifa mbalimbali dhidi ya mbunge wa jimbo hilo Mwingullu Nchemba, kitendo ambacho kiliudhi baadha ya watu waliokuwa wamehudhuria mkutano huo.

“Wananchi hao ambao walichukizwa na kitendo cha kukashifiwa mbunge wao,walianza kupiga kelele kuwa hawataki mbunge wao akashifiwe na badala yake wanataka kusikia sera za CHADEMA tu na si vinginevyo.Hata hivyo,viongozi hao waliendelea tu kuporomosha kashifa dhidi ya Mwingullu na kusababisha kuanza kwa vurugu”,alisema.

Kamanda huyo alisema kuwa vurugu hizo zilihusisha kundi la wanachama wa CHADEMA na wa CCM na zilisambaa.Wanachama hao walianza kurusha mawe ovyo na askari wachache wa polisi waliokuwepo,walizidiwa nguvu na makundi hayo.

“Huyu mwenyekiti wa vijana CCM Yohana,yeye akikimbilia kwenye nyumba ya mwalimu Shume Manase Mpinga ili kuokoa maisha yake,lakini kundi la wananchama wa CHADEMA wakiwa wamebeba fimbo na mawe,walimpiga sehemu mbalimbali za mwili wake na kusbabisha kifo chake papo hapo”,alisema kamanda Sinzumwa kwa masikitiko makubwa.

source:dewjiblog.

Tamko Maalum Kutoka CHADEMA Kuhusu Yaliyojiri Katika Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA Uliofanyika Kata ya Ndago Siku ya Jumamosi Tarehe 14 Julai 2012

Leave a comment


Ofisa wa Sera na Utafiti CHADEMA Makao Makuu Bw. Waitara Mwita Mwikwabe


CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

Tamko Kuhusu Yaliyojiri Katika Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA  Uliofanyika Kata ya Ndago Siku ya Jumamosi Tarehe 14 Julai 2012

1. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliandaa mikutano ya  hadhara katika Jimbo la Iramba Magharibi. Mikutano hiyo ilitolewa taarifa polisi na jeshi hilo lilitoa baraka zake kama utaratibu wa sheria unavyotaka kwa barua yake ya tarehe 12 Julai 2012 Kumb. Na. KIO/ B1/1/VOL.V/268

2. Mkutano wa kwanza ulipangwa kufanyika katika Kata ya Ndago katika  viwanja vilivyo karibu na kituo cha mabasi ambapo pia ni hatua chache karibu kabisa na Kituo cha Polisi Ndago. Mkutano huu ulipangwa kuanza saa nane mchana.

3. Msafara wa kitaifa unaofanya ziara ya ukaguzi wa chama, katika mkoa  wa Singida chini ya uratibu wa Ofisa wa Sera na Utafiti Makao Makuu, Mwita Mwikwambe Waitara, (ikiwa ni maandalizi ya operesheni nyingine kubwa mkoani humo itakayofanyika baadae), uliwasili katika eneo la  Mkutano majira ya saa tisa na nusu alasiri. Tulikuta wananchi wengi
wakiwa wanatusubiri. Kabla ya Mkutano kuanza tulipewa taarifa kwamba kuna kikundi cha vijana kimeandaliwa kuvuruga mkutano wa CHADEMA kwa kufanya fujo, ikiwemo kurusha mawe ili mkutano huo usifanyike. Suala hilo lilielezwa mkutanoni mapema na Mheshimiwa Waitara, mbele ya askari polisi.

4. Wakati tukijiandaa kuanza hotuba, vijana wapatao wanane walianza chokochoko kwa kutoa matusi na punde mawe yakaanza kurushwa kutoka sehemu mbalimbali. Wakati fujo zinaanzishwa na kile kikundi, Mheshimiwa Waitara alikuwa bado anazungumza na wananchi kuwaandaa kusikiliza wazungumzaji wengine. Vurumai hiyo ilizimwa na wananchi
wenyewe wa Ndago waliokuwa na hamu ya kusikiliza ujumbe wa viongozi wa kitaifa wa CHADEMA.

5. Kwa kweli tunawashukuru wananchi wengi wa Ndago walioonesha ujasiri  mkubwa kuweza kuwaondoa vijana wale eneo la mkutano, kisha mkutano ukaendelea, huku wananchi wakionesha kila hamasa ya kufurahia hoja kutoka kwa wazungumzaji, akiwemo Mheshimiwa John Mnyika, ambaye aliombwa ahudhurie ziara hiyo kwa nafasi yake ya Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA.

6. Mpaka tunamaliza mkutano huo ambao wananchi waliufurahia sana kwa  namna ulivyohutubiwa kwa amani na utulivu huku wazungumzaji wakijenga hoja juu ya mstakabali wa jimbo na taifa lao kwa ujumla, mamia ya wananchi waliohudhuria walitaka tuendelea kuhutubia, lakini tulibanwa na ratiba ya kuwahi mkutano wa pili, eneo la Kinampanda.

7. Lakini kutokana na vurugu hizo zilizokuwa zikisababishwa na kikundi  cha vijana ambao tayari ilishatolewa taarifa yao kwenye mkutano huo, lakini askari waliokuwepo hawakuthubutu kuchukua hatua, tulilazimika kuomba msaada kutoka kwa OCD na R.P.C, ambapo baadae wakati mkutano unakaribia kuisha tuliona gari la polisi kutoka Mjini Singida likiwa na askari waliojipanga rasmi kwa ajili ya kuzuia vurugu likifika pale
eneo la mkutano, lakini wakati huo hali ilishatulia na hotuba zimetolewa vizuri.

8. Kutokana na hali hiyo ya vurugu, zilitolewa taarifa Kituo cha  Polisi cha Ndago, ambapo lilifunguliwa jalada NDG/RB/190/2012. Katika jalada hilo tulitaja baadhi ya majina ya watuhumiwa waliokuwa vinara wa kundi lililokuwa likifanya fujo kwenye mkutano mbele ya askari polisi. Majina hayo ni; 1. Daniel Sima, 2. Tito Nitwa, 3. Bakili Ayubu, 4. Yohana Makala Mpande, 5. Ernest Kadege, 6. Abel John, 7. Athuman Ntimbu, 8. Martin Manase, 9. James Ernest, 10. Simion Makacha, 11. Anton John, 12. Frank Yesaya

9. Kwa hakika askari polisi wa Ndago waliokuwepo mkutanoni mbali ya  kutochukua hatua yoyote dhidi ya fujo tulizofanyiwa ikiwemo kupondwa mawe na kikundi kidogo cha wahuni, fujo zilipozidi askari wote walikimbia eneo la mkutano, akabaki OCS pekee ambaye naye alionekana dhahiri kutotaka kuchukua hatua stahili. Hakuonekana kufanya juhudi zozote za kuhakikisha amani inalindwa na ulinzi unaimarishwa katika eneo la mkutano na hatua zinachukuliwa dhidi ya watu walioonekana kudhamiria kufanya fujo.

 Mtu yeyote makini angeweza kuona kuwa askari wale walikuwepo pale mkutanoni ‘almuradi’ tu lakini kama vile walikuwa na maelekezo maalum ya kuhakikisha hawachukui hatua yoyote katika kuzuia mpango wowote wa kusababisha vurugu na kuvunja amani.

10. Baada ya kumaliza mkutano wa Ndago kwa amani, tulikwenda  Kinampanda ambako tulifanya mkutano mwingine mzuri kwa amani kabisa, ambapo mbali ya wananchi kuwa wametusubiri kwa hamu kubwa na kutusikiliza kwa makini hoja zetu, polisi katika eneo hilo walitupatia ushirikiano mzuri tangu wakati tunafika mpaka tulipomaliza mkutano
huo.

11. Jioni wakati tumerudi hotelini, tukasikia kuna taarifa  zinasambazaa kuwa kuna mtu/watu wamekufa katika eneo la Ndago. Habari hizo zilikuwa zinakanganya kwa sababu zilikuwa zikitaja idadi tofauti tofauti. Lakini kwa vyovyote vile kama ni kweli kuna tukio la mtu
kufariki, CHADEMA tunasikitika sana kwa tukio hilo la uhai wa mtu.

12. Tunalaani taarifa zinazozidi kusambazwa ambazo zinawataja polisi  kuwa wanatuhusisha CHADEMA na tukio la mtu aliyefariki. Hii ni ajabu kubwa kwamba tumetoka kwenye mkutano ule kwa amani kabisa mpaka tumemaliza mkutano wa pili kwa amani na polisi wakiwepo sehemu zote mbili, kisha tunasingiziwa masuala ambayo wenyewe hatukuwa na habari nayo tangu mkutano wa kwanza ukiwa unaendelea mpaka mkutano wa mwisho
ulipomalizika.

13. Kutokana na habari hiyo ya kifo cha mtu inavyoenezwa kwa  kuihusisha CHADEMA, tumebaini kuwepo kwa mbinu na mikakati ya chama tawala pia vyombo vya dola vikihusika kutaka kuwatisha wananchi waSingida, Watanzania wote wapenda mabadiliko na viongozi wa CHADEMA katika mkoa huu, wasifanye kazi ya kisiasa kwa kuwabambikizia tuhuma
na kesi na pia kuwafanya waonekane ni watu wa vurugu.

14. Tunapenda kusema hapa kuwa njama hizo hazitafanikiwa. Zitashindwa  kama zilivyoshindwa njama zingine zote ambazo zimekuwa zikifanywa na vyombo vya dola, viongozi wa serikali na chama tawala dhidi ya CHADEMA na vuguvugu la mabadiliko nchini.

15. Tunawataarifu wananchi kuwa ratiba ya kufanya Operesheni nyingine  kubwa katika Mkoa wa Singida, ikiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Willibrod Slaa, itafanyika baadae kama ilivyoazimiwa na kikao cha Kamati Kuu.


Imetolewa leo Singida, Julai 15, 2012 na;
Waitara Mwita Mwikwabe
Ofisa wa Sera na Utafiti CHADEMA Makao Makuu

source:fatherkidevu

AMBAKA MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI

Leave a comment


Mwanafunzi wa darasa la pili (7) katika shule ya msingi Mkombozi amenajisiwa na baba yake wa kambo jana majira ya saa 5:00 usiku huko Shigamba, Mbalizi jijini Mbeya.
Maafisa wa Polisi wamesema mtoto huyo, ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiusalama ni mbena na mkazi wa Shigamba amebakwa na Josephat Mtawa (39), Mndali, mkulima na mkazi wa Shigamba ambaye ni baba wa kambo wa mtoto huyo na kumsababishia maumivu makali mwilini mwake.

Maafisa hao wameongeza kusema kitendo hicho cha kinyama kwa mtoto huyo kiligundulika na mama mzazi wa mtoto. Pia mbinu aliyoitumia mtuhumiwa ni kumvizia mtoto alipokuwa amelala sebuleni na kumtoa hadi nje hadi kwenye pagala na kumbaka. Mtuhumiwa yupo mahabusu na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea.

Kamishna msaidizi wa Polisi, mkoa wa Mbeya Diwani Athumani ametoa wito kwa jamii kujiepusha na matendo ya udhalilishaji yaliyo nje na kinyume na maadili kwani yeyote atakeye jihusisha nayo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
source:jaizmelaleo

MISS UTALII KAGERA KUFANYIKA JUMAMOSI 14-7-2012

Leave a comment


Shindano la kumsaka Miss Utalii mkoa wa Kagera 2012, litafanyika katika ukumbi wa Linas Club siku ya tarehe 14-7-2012 kuanzia saa, mbili usiku. Katika shindano hilo Warembo 15 watachuana kuwania taji la miss Utalii Tanzania 2012- Kagera, ambapo watapita jukwaani katika mavazi ya kitanzania ya Ubunifu,kitalii,kutokea na ya asili, huku wakitangaza Utalii, Utamaduni,urembo wa kitalii, ubunifu na vipaji vya kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za asili za makabila ya mkoa wa Kagera na Tanzania kwa ujumla. Burudani mbalimbali za Ngoma za asili, bendi na wasanii wa muziki wa kizazi kipya watakuwepo, wakiwemo Diamond Musica Band, Agcox Burchaman toka Uganda,Maua na BK Sunday. Shindano hilo limedhaminiwa na Cargo Star, Vodacom Tanzania,Kroyera Tours,Vission Radio,Kasibante Radio, prins Hotel,Paradise Hotel,Linas Club ,Mice and Lovely Salon,misstourismorganisation.blogspot.com na Amazing Tanzania Tours(Tours and Safaris) .
Washindi wa shindano hilo watawakilisha mkoa wa Kagera katika fainali za miss Utalii Tanzania 2012- Kanda ya Magharibi, na baadae katika fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2012 zitakazofanyika siku ya mkesha wa Uhuru wa Tanzania 8-12-2012.
Miss Tourism Tanzania Symbol Of National Heritage – Do Value Added Pageant
“Lets Visit & Promote Tanzania National Parks -Tourism is Life ,Culture is Lining”

BSS ARUSHA GUMZO NI MAJAJI ZAIDI YA WASHIRIKI

Leave a comment


Majaji wa shindano la BSS wakiwa katika ukumbi wa Triple A tayari kwaajili ya usahili wa kuwasaka washiriki wa shindano hilo kwaajili ya kuwakilisha Mkoa wa Arusha katika shindano litakalofanyika jijini Dar es Salaam, kutoka kushoto ni Master J, katikati Rita Paulsen na Salama Jabir

Washiriki wa shindano hilo wakisubiri kuingia ndani kwaajili ya Usahili wakiwa wameketi katika viwanja vya Triple A jijini Arusha

Kushoto ni Afisa Masoko kampuni ya simu ZANTEL kanda ya kaskazini Bw.Melitus Kimolo akizungumzia juu ya suala la uchangishaji damu ambapo yeye mwenyewe alichangia damu,,zoezi ambalo lilikuwa pia likiendelea katika viwanja hivyo,,,,Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko Bw.Deepak Kumar Gupta

Daktari akiwa anamtoa damu kijana aliyejitokeza kuchangia damu kwa hiari

source:father kidevu

Producer Ally Baucha afiwa na baba yake mzazi

Leave a comment


Producer mkongwe nchini wa studio za Baucha Records, Ally Baucha, amefiwa na baba yake mzazi usiku wa kuamkia leo.
Leo usiku muda wa saa 6:26, ametutumia ujumbe wa simu unaosema, “Mambo vp…? Nimefiwa na baba mzazi leo usiku huu. Najua wewe ni mtu muhimu kukutaarifu kwanza, nasubiri kuelekea Zanzibar kwa mazishi… Baucha.”
Baucha amesema kifo cha baba yake Mzee Mohamed Yussuf kimetokana na ugonjwa wa ini.
Mzee Yussuf aliyefariki akiwa na umri wa miaka 69,aliwahi kuwa mkuu wa polisi wa wanamaji mkoa wa Mwanza miaka ya 1980 kabla ya kuhamishiwa Zanzibar.

source:bongo5

Older Entries

%d bloggers like this: