Home

AFANDE SELE AKIFUNGUKA KUHUSU SHOW YA ZANZIBAR MUSIC AWARD

Leave a comment


Salaam Ndugu zangu wote mashabiki na wadau wa muziki wetu!!
Tamko langu kuhusiana na lugha zilizotolewa na Twent Percent kuhusiana na show yetu ya Zanzibar Music Award.
“Tulialikwa kwenye ZANZIBAR MUSIC AWARD, na kabla ya kazi makubaliano yote ya kazi kwa mujibu wa mkataba yalifuatwa, makubaliano hayo yalihusisha sisi kujigharamia gharama zote za nauli na Malazi (accomodation).
Tulifika Zanzibar salama, tulipokua Zanzibar twenty alitaka agharamiwe huduma zote ambazo ni nje ya mkataba wetu, nikamuomba na kumsihi sana Ndugu yangu aheshimu mkataba, asitafute matatizo kwani tayari mpaka wakati huu tuna kesi na Halmashauri ya Manispaa ya Moro ambayo kimsingi sikuhusika (nilishatolea ufafanuzi siku za nyuma).
Lakini yeye alipingana na mimi, akanibishia na kunisukuma Mbele ya wageni na wenyeji wetu, wakiwemo Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seiph Ali Idi, Waziri Seiph Khatibu.
Walikuwepo waadishi wa habari wa siku Nyingi Akiwemo Abubakari Liongo (idhaa ya kiswahili radio Ujerumani), Mkurugenzi wa ZENJI FM ndugu Tua Saidi Tua.
Mimi Selemani Abdallah Juma Msindi sihusiki kwa namna yoyote, na tabia zisizo za kuridhisha zinazoonyeshwa na Ndugu yangu Twenty Percent, ambae nimekua nae nyumbani kwangu hata kabla ya Tuzo zake Tano (Kili Music Award) ambazo kazi hizo zote hizo kaandikia nyumbani kwangu siwezi kuwa na tatizo nae ni ndugu yangu kiimani na kikazi, hata kazi yangu niliyofanya nae kabla siku za nyuma “MBELE YAKO NYUMA YANGU” .. Kuna mstari Nilisema ” ..Kuandika Rhyme kwenda Gym kimtindo kuonyesha Ugum, bado unatakiwa uwe na nidhamu ya kweli, sio ya kumzuga Mwalimu, utajihukumu”.
Nimekua nikisisitiza nidhamu kwa Ndugu zangu woote toka enzi za Ghetto BoyZ, Watupori na Mabwasha’Kingdom, ambao wengine hawafanyi sanaa, ila nipo nao kwenye Familia yetu kubwa hapa Tanzania. Nimesikitishwa na kitendo hicho. Siku zote nimekua mwenye kuhitaji suluhu kwa namna ya Amani.
Verry sorry kwa wote ambao mumefadhaika kwa hilo. Tuendelee kuwa pamoja na msisite kutoa ushauri wenu, maoni ili Game letu lisonge. MUNGU ATUBARIKI.
Asanteni sana.
Selemani Juma Abdallah Mutabhazi Msindi.
a.k.a Afande Sele (King of Rhymes)

source:

JINSI JOSE CHAMELEONE ALIVYOANZA KUPATA MAFANIKIO KWENYE MAISHA, HIVI NDIVYO ANAVYOPATA PESA.

Leave a comment


Jose Chameleone (katikati) akiwa kwenye shooting ya moja ya video zake.

Baada ya kukutana na staa wa muziki kutoka Uganda Jose Chameleone nimegundua kuna mambo mengi nilikua nayasikia tofauti na kuyasoma ambayo yeye ameyazungumza tofauti kabisa.
Nilikua sijui, kumbe Chameleone alianza kuenjoy kuwa staa kuanzia mwaka 2000 japo alianza muziki 1995, 2003/2004 ndio alianza kupata pesa na hapo ndipo maajabu yalianza kutokea kwa kuanza kutimiza ndoto.Chameleone amesema “nilijenga nyumba yangu kwa miaka miwili ambapo 2005 ilimalizika na ikawa imegharimu shilingi milioni 200 -300 za kitanzania, wakati nilikua naijenga hiyo ndio pesa niliyokua nayo na nikasema kabla sijaipoteza acha nifanye kitu muhimu lakini Mungu akanibariki tena baada ya kujenga hiyo nyumba nikapata bahati nyingine nikaendelea na vitu vingine”
Exclusive na millardayo.com Mwimbaji huyu staa kutoka Uganda amesema vyanzo vyake vikubwa vya mapato kwa sasa ni kununua na kuuza ardhi, kuuza simu za mkononi ziitwazo Chameleone anazozitengeza China, kununua nyumba na kuziuza pia kupangisha nyumba.
kuhusu vyanzo vingine vya mapato Chameleone amesema “show pia zinatulipa sana Uganda japo siwezi kukwambia nalipwa bei gani kwa sababu sipendi kuonekana mtu wa kujisifia lakini kwa wiki moja naweza kupiga show mbili Kampala au Uganda, na kingine kinachotulipa sana ni Kampuni kubwa za biashara ambazo zikikuona una nguvu zinakuchukua na kukulipa vizuri kwa kufanya nao promoshen au mambo mengine ya mkataba wa biashara”

source:millardayo

Breaking News: Mama yao P-Square (Peter na Paul Okoye) afariki dunia

Leave a comment


Mama mzazi wa wasanii mapacha wa Nigeria Peter na Paul Okoye wa kundi la Psquare amefariki dunia.
Mrs. Okoye amekuwa akiumwa kwa mrefu ugonjwa ambao bado haujajulikana.
Pamoja na Peter na Paul, watoto wake wengine Jude na Ajeh wana mchango mkubwa kwenye muziki wa Nigeria.
Wakati kila mtu anajiuliza nini chanzo cha kifo cha mama yao, mtandao wa niyitabiti.net umebaini kuwa baada ya kuanza kuumwa alipelekwa kwenye hospitali ya St. Nicholas Hospital, miongoni mwa hospitali ghali zaidi nchini Nigeria.Baadaye alipelekwa nchi za nje kwa matibabu zaidi. Bahati mbaya amefariki wakati akiendelea na matibabu hayo.
Muda mfupi baada ya habari hiyoi kujulikana, marafiki na jamaa walianza kutuma salamu za rambirambi kwa familia ya Psquare.Katika maisha yake, mama huyo anafahamika kwa mchango mkubwa kwa mafanikio ya watoto wake. Leo hii P-square ndo wanamuziki wanaolipwa pesa nyingi zaidi nchini Nigeria na barani Afrika kwa ujumla.

MISS UTALII KAGERA KUFANYIKA JUMAMOSI 14-7-2012

Leave a comment


Shindano la kumsaka Miss Utalii mkoa wa Kagera 2012, litafanyika katika ukumbi wa Linas Club siku ya tarehe 14-7-2012 kuanzia saa, mbili usiku. Katika shindano hilo Warembo 15 watachuana kuwania taji la miss Utalii Tanzania 2012- Kagera, ambapo watapita jukwaani katika mavazi ya kitanzania ya Ubunifu,kitalii,kutokea na ya asili, huku wakitangaza Utalii, Utamaduni,urembo wa kitalii, ubunifu na vipaji vya kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za asili za makabila ya mkoa wa Kagera na Tanzania kwa ujumla. Burudani mbalimbali za Ngoma za asili, bendi na wasanii wa muziki wa kizazi kipya watakuwepo, wakiwemo Diamond Musica Band, Agcox Burchaman toka Uganda,Maua na BK Sunday. Shindano hilo limedhaminiwa na Cargo Star, Vodacom Tanzania,Kroyera Tours,Vission Radio,Kasibante Radio, prins Hotel,Paradise Hotel,Linas Club ,Mice and Lovely Salon,misstourismorganisation.blogspot.com na Amazing Tanzania Tours(Tours and Safaris) .
Washindi wa shindano hilo watawakilisha mkoa wa Kagera katika fainali za miss Utalii Tanzania 2012- Kanda ya Magharibi, na baadae katika fainali za taifa za Miss Utalii Tanzania 2012 zitakazofanyika siku ya mkesha wa Uhuru wa Tanzania 8-12-2012.
Miss Tourism Tanzania Symbol Of National Heritage – Do Value Added Pageant
“Lets Visit & Promote Tanzania National Parks -Tourism is Life ,Culture is Lining”

WAJANJA WA BUSH WAMLIZA TIMBULO DOLA 800

Leave a comment


Nyota wa muziki wa kizazi kipya Bongo, ALLY Timbulo ‘Timbulo’ amepatwa na tukio la aina yake baada ya wajanja wa Bush kumliza kamera kubwa aina ya sonny wakati wa paty maalumu aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita kijijini kwao Riuwa, Wilayani Mbalali jijini Mbeya.

Akizunguma na Teentz mapema leo Timbulo amesema kuwa aligundua kupotea ghafla kwa kamera yake hiyo mara baada ya kumalizika kwa paty hiyo iliyokuwa imechangamka kupita kiasi huku vijana wengi aliokuwa wamefurika wakiwa hoi kwa mitungi.
“Nilipomaliza kuimba nikawa nimechili sehemu napumzika, lakini baada ya party kuisha nianza kukusanya vitu vyangu na baadae nikagundua kuwa kamera yangu haipo, kwa kweli nilichanganyikiwa kwa kuwa bado ni mpya kabisa na niliinunua kiasi cha dola 800 za Marekani” alisema Timbulo
Akiendelea zaidi timbulo amesema kuwa juhudi za kumsaka mtu aliyesepa na kamera hiyo ya kisa bado zinaendelea kwa kuwa sehemu kubwa ya watu waliofika siku hiyo wanafahamiana hivyo anaamini ndani ya siku chache zijazo atakuwa ameipata.
katika shoo hiyo Timbulo amerifu kuwa jukwaa alilokuwa analitumia kuwaburudisha mashabiki wake lilishindwa kuhimili vishondo na kuvunjika kufuatia watu kushindwa kuvumilia na kupanda juu alipokuwa yeye na hatimaye jukwaa hilo likasalimu amri.
“Hakika ilikuwa siku mbaya kwani kuna mambo mengi yalijitokeza ikiwamo shughuli yangu kucheleweshwa baada ya mchana na kuwa ucku kutokana na mtendaji wa kata kuzuia mpaka diwani alipoingilia kati na kuniruhusu” alimaliza

source:teentz

GODZILLA : MASHABIKI WALITAKA NIIMBE

Leave a comment


Staa wa hip hop Bongo, Godzilla amefunguka kuwa hatua ya kutoa wimbo ukiwa kwenye staili ya kuimba imekuja kufuatia maombi kibao aliyoyapata kutoka kwa fans wake.
Akizungumza na Teentz.com muda mfupi uliopita Godzilla anayesumbia kitaa na ngoma kali inayobeba jina la ‘La Kuchumpa’ amesema kuwa ameshangazwa na hataua ya wadau wa muziki wa kizazi kipya kuhoji juu ya uamuzi wake wa kutumia staili ya kuimba kwenye wimbo wake mpya uliopewa jina la ‘nataka’.
“Unajua mimi ni mwanamuziki na katika hilo ni lazima ujuwe kuwa nina mashabiki ambao kwa lolote wako nyuma yangu , hivyo basi walinifuata na kuniambia kuwa wanataka nijaribu kutoa wimbo kwenye staili ya kuimba soo kwakuwa ninatambua umuhimu wao nikaamua kutoa nyimbo mbili moja ikiwa kwenye mtindo huo na nyingine ikiwa kwenye hip hop kama kawaida” alisema Zilla na kuongeza kuwa nimeamu a kufanya hivyo ili kuwarizisha mashabiki wangu wote.

source:.teentz

Baada ya Diamond, Diva kumshirikisha Kabayser na Ommy Dimpoz

Leave a comment


Baada ya mtangazaji wa radio na msanii wa muziki Loveness aka Diva kuachia wimbo ‘Piga Simu’ aliomshirikisha Diamond, safari yake ya muziki haina dalili ya kusimama hivi karibuni kwakuwa ana mipango mikubwa na kufanya ngoma na ‘big cats’ in the game.
“Whatchu all think? Remix coming featuring Ommy Dimpoz na ndio video tutatoa sasa with the boys,Ommy Dimpoz and Diamond …all we need is something good not only a video but Diva kinda video …next level kabisa, the moment ntarelease remix and the video will continue sasa,” aliandika kwenye blog yake.
“Second song itakuja featuring Mr. Blue na ntaitoa after Diva Giving for charity event and namtafuta Blue for that muda si mrefu sana. He is the perfect feature for my second song, ana fit as in my verses are ready and the beat omg Fishcrab again as u know.”
Katika hatua nyingine baada ya kuongezeka kwa maswali mengi juu ya nani aliyemwimbia kwenye ‘Piga Simu’ mwezi uliopita na kuandikwa vibaya aliamua kufunguka na kutoa ufafanuzi.
‘Sijataja mtu jina …and are you sure huyo unaemuhisi au unayemtaja natoka nae? maana nilivyosema sina boyfriend for years mlisema Diva msagaji Diva this Diva that , nasema nina boyfriend nimemuimbia nyimbo mnaanza sasa kunitajia list ndefu , you guys got time I swear,you all don’t know a bit about me,” aliandika.
“Acheni kuzusha mambo ya ajabu na kusambaza,maana asilimia ya mambo ninayoandikwa na kuongelewa that’s so not me , nijueni basi kidogo ndo mnizungumzie.”
Aliendelea kuandika, “Tupeane break sasa, mjueni Mungu a bit maana it’s too much sasa. Next thing what???Diva freemason labda maana ndio zenu hizi mpya while am a very Good Christian and church is the right thing for me every sundays . Serious what next jamani??? What next?? Da! maana nimechoka sana sana

source:bongoflavortz

Older Entries

%d bloggers like this: