Home

HUYU NDIO MUHUBIRI ALIETABIRI AJALI NYINGINE YA NDEGE.

Leave a comment


Muhubiri TB Joshua wa Nigeria ametabiri tena kwamba kuna ajali nyingine mbaya ya ndege itakayotokea siku za karibuni kwenye nchi hiyo. Amesema kama hiyo ajali ya ndege haitotokea basi wanasiasa tisa mpaka 12 wa Nigeria watapoteza maisha yao kwenye ajali nyingine ya ndege, na hiyo itatokea wakati wakiwa wanarudi kutoka kwenye mkutano. Yani wote watapoteza maisha kwenye ndege itakayokua imewabeba wakiwa kuanzia 9 mpaka 12 kwa sababu shetani ana mipango ya kuwashambulia wote kwenye ndege hiyo moja. Amesema ili kuepuka hiyo ajali ni lazima wanasiasa hao waepuke kupanda ndege moja.
Mtandao wa Naija umeuliza, kama kweli huyu ni mtumishi wa Mungu na anaweza kutabiri mambo mabaya tu kutokea kwenye nchi hiyo, kwa nini asitumie nguvu yake kuomba neema na Nigeria kuepushwa na hayo majanga?

Hii ndio ajali maba ya ndege iliyotokea June 4 mwaka huu na kuua zaidi ya watu 153.

source:millardayo

SIMU ANAYOUZA JOSE CHAMELEONE WA UGANDA, ZIJUE BIASHARA ZAKE NYINGINE.

1 Comment


Millard Ayo na Jose Chameleone kwenye interview.

Kwa mara ya kwanza toka Show ya AMPLIFAYA ianzishwe zaidi ya siku 500 zilizopita, leo ndio interview ya kwanza na staa wa Afrika Mashariki Jose Chemeleone kutoka area 256 imesikika akiwa na Millard Ayo. Utazisikia Stori zake nyingi tu kwenye mfululizo wa show za AMPLIFAYA on super brand Clouds fm na hapa millardayo.com!!! kuhusu muziki wake najua hizo stori utakua umezisikia sana kwengine…. Ninachokifanya ni kwenda deep zaidi kwenye maisha yake, Navifata vyote vilivyotokana na jina lake. Huu ni mwaka wake wa 12 toka ameanza kuwa maarufu kwenye muziki, Jose Chameleone anaetajwa kuwa kwenye list ya wanamuziki watano matajiri wa muziki wa sasa Afrika Mashariki, leo amekubali macho yako yasome vitu atakavyovitaja vinavyompa pesa nyingi tofauti na muziki kwa sasa.

Hii ndio simu inaitwa CHEMELEONE ambayo inauzwa kwenye maduka mbalimbali Uganda, unaweza kuwaka line yoyote ya mtandao wa simu.


Amesema Moja kati ya ishu anazopiga ni “kununua nyumba na kuziuza, kukodisha, pia kununua mashamba na kuyauza huko Uganda, na kuna biashara nyingine nimeianza juzi juzi ya CHAMELEONE MOBILE, nilikwenda China na kuungana na kampuni moja ya China wakatengeneza simu inaitwa CHAMELEONE, hiyo ni moja kati ya kazi zangu kubwa… watu wanazinunua sana nyumbani Uganda, ni handset ambayo unaweza kuweka line ya mtandao wowote”

Kwenye line ya mwisho ChameleonE kasema “hii ni kujaribu kufikiria nje ya box pamoja na kujaribu kufanya mipango uliyokua nayo kichwani, na bado naendelea baada ya hizo simu nataka kutengeneza vitu vingi zaidi.. nataka jamii yangu inikumbuke kwa nilichowafanyia”

Hayo ndio aliyoyasema Staa wa muziki Jose Chameleone wa Uganda nchi inayotajwa kuwa na wasanii wanaoongoza kwa kuwa na pesa nyingi kuliko nchi yeyote Afrika Mashariki.

Tayari mpaka sasa kuna baadhi ya mastaa ambao wamejaribu kupiga dealz nyingine mbali na muziki akiwemo Lady JayDee ambae anamiliki Mgahawa, Jua Cali wa Kenya alitangaza kuanza kutengeneza headphone kama za Beat by Dre, Profesa Jay nae alitangaza kwamba ndoto zake hazipo kwenye magari ya kifahari sasa hivi au anasa nyingine, anajipanga kwa ajili ya kuinvest kwenye ardhi for now.

source:millardayo

WEMA AITWA IKULU

2 Comments


Wema Isaac Sepetu.

WEMA Isaac Sepetu amelidokeza gazeti alipendalo la Ijumaa Wikienda kuwa ameitwa ikulu ya Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza kwa mwaliko maalum.
Wema alisema mwaliko huo aliupata mara tu baada ya kuzindua ile filamu yake ya Super Star wiki mbili zilizopita ambapo katika mwaliko huo wa ujumbe kutoka ikulu hiyo ulimuomba kutoisambaza kwanza kabla ya kwenda kuizindua nchini humo.
“Waliniambia juu ya mimi kuomba uraia wa nchi hiyo ili kukuza filamu zao. Kusema kweli nilikuwa nina ratiba ya kwenda kuizindua filamu yangu Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Yaani sijui hata walijuaje. Sijui ni nini kimetokea, nina wasiwasi. Hata sijui nitaongea nini na Rais wa Burundi,” alisema Wema na kuongeza kuwa maandalizi yakikamilika atatii wito huo muda wowote

source:globalpublishers.

Sauti za Busara yajipanga kuleta wasanii wakubwa wa Congo mwakani

Leave a comment


Waandaji wa tamasha la Sauti za Busara ambalo hufanyika kila mwaka mwezi February visiwani Zanzibar, wamesema wanajitahidi katika tamasha la mwakani, 2013, kuleta wasanii wakubwa wa nchini DRC.
Extra musica, JB Mpiana, Werrason na Fally Ipupa ni miongoni mwa wasanii ambao wangependa kuwaona kwenye steji wakati tamasha hilo la kumi litakapofanyika tarehe 14 hadi 17 February, 2013 mjini Zanzibar.
Ni wasanii wachache sana kutoka Congo waliowahi kutumbuiza katika tamasha hilo kubwa wakiwemo Fredy Massamba, Samba Mapangala na orchestra Virunga and Super Mazembe.
Waandaji wa tamasha hilo wamesema lengo lake ni kupromote vikundi vya muziki vya Tanzania kwa walau asilimia 50 na asilimia zingine ni kwaajili ya wasanii kutoka nchi zingine za barani Afrika pamoja na waafrika waashio ugenini (Diaspora).
Wamesema awamu ijayo wangependa kuwaalika wanamuziki wanaojulikana zaidi wakiwemo Extra Musica, Fally Fally, Werra Son, JB Mpiana, Staff Benda Bilili, Konono No. 1, Kasai All Stars na wengine.
Wamesema wanamuziki hao watakonga nyoyo za wapenzi wa muziki na pia kuwabadilisha wasanii wa Tanzania katika kutengeneza muelekeo mpya kwa kufanya muziki halisi wa kitanzania.
Tamasha hilo ambalo hufanyika kwenye eneo la ‘Ngome Kongwe’ mjini Zanzibar huwakutanisha wasanii wakubwa wa Afrika, wapenzi wa muziki na waandishi wa habari kusherehekea utajiri wa muziki wa bara la Afrika.

source:bongo5

Fally na Mr. Flavour wafanya kazi Pamoja

Leave a comment


Mwanamuziki wa kizazi kipya cha lingala ya Congo, Fally Ipupa amezidi kuonesha ukaribu zaidi na wasanii wa Nigeria na kufanya nao ngoma.
Jana kupitia Facebook, alipost picha mbili akiwa kwenye ‘video shoot’ nchini Ufaransa na msanii wa Nigeria Flavour na kumaanisha kuwa wamefanya wimbo pamoja.
Wimbo huo mpya ni wa Flavour utakaokuwepo kwenye albam yake mpya.
Fally Ipupa amewahi pia kushirikishwa na Jay Martins katika remix ya wimbo wake uitwao Jukpa.
Jumamosi iliyopita, June 30, Flavour, kundi la Bracket na Dontom, walikuwa mjini Paris Ufaransa kwa mara yao ya kwanza na kutumbuiza mbele ye umati wa wapenzi wao wa muziki nchini humo.
Ziara hiyo ilimpa nafasi Flavour ya kumpata Fally Ipupa ambaye mara nyingi huwepo Paris na kufanya video yao jana.
Wasanii wa Afrika kutoka nchi zingine zisizozungumza kifaransa, wameanza kujipatia soko na umaarufu mkubwa nchini Ufaransa husasan wasanii wa Nigeria.
Mwezi March mwaka huu Flavour N’Abania alisaini mkataba na label kubwa ya muziki ya nchini Afrika Kusini iitwayo Sould Candi.
Mkataba huo ulifanikisha uuzwaji wa albam yake Uplifted, iliyokuwa na hit ‘Nwa Baby’ kuuzwa nchini Afrika Kusini.
Kwa upande wake Fally Ipupa, mwishoni mwa mwezi uliopita, aliungana na Ferre Gola mjini Paris kuimba wimbo wa kizalendo kwa nchi yao uitwao “Congo, my country.”
Wasanii wengine wa Congo walioshiriki kwenye wimbo huo ni Lokwa Kanza, Djessi Matador, Aimelia, Celeo Schramme na wengine ambapo jumla wapo wanamuziki 30.

NI LINI SERIKALI ITATIBU CHANZO CHA MGOMO WA MADAKTARI? – ANANILE NKYA

Leave a comment


Katika nchi  yeyote duniani serikali ndiyo  yenye  jukumu la kuweka mazingira mazuri katika hospitali za umma na kuhakikisha kuwamadaktari na wafanyakazi  wa afya  wanafanya kazi yao ya kutibu wagonjwa  kwa  furaha .

Hii  ni kwa sababu serikali  iliyowekwa  madarakani na wananchi moja ya kazi ya   kodi inayokusanya kutoka kwa wananchi   ni kuhakikisha kuwa  hospitali, vituo vya afya na zahanati za umma ziko katika mazingira mazuri na zinatoa huduma nzuri kwa wananchi.

Mazingira mazuri hospitalini ni pamoja na  kuwepo kwa vitanda vya kutosha kwa  wagonjwa,  madawa ya kutosha na ya viwango bora, vifaa kwa ajili ya kupima na kubaini magonjwa na vifaa  na vyumba maalum vya kusaidia watu  wanaofanyiwa upasuaji wasipoteze maisha.

Lakini hali ya hosipitali zetu za umma ni hairidhishi.   Kwa mfano hospitali ya taifa ya   Rufaa Muhimbili ni hospitali  madaktariwanalalamika kuwa hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinawafanya madaktari  kushindwa kutimiza wajibu wao wa  kuokoa maisha ya wagonjwa.

Kwa mfano  hospitali hiyo ina   mashine  ya MRI  ya kupima na kutambua ugonjwa  mbali mbali  kwenye mwili ikiwa ni pamoja na kwenye   ubongo, uti wa mgongo na kifua. 

Lakini  cha kushangaza mashine hiyo  iliyonunuliwa kwa  shilingi zisizopungua Bilioni mbili miaka michache iliyopita,  inapungukiwa kifaa cha bei ndogo  tu cha    kuwezesha  watoto kupimwa. 

Hivyo watoto wenye matatizo yanayohitaji kupimwa kwa mashine hiyo  wanalazimika kupelekwa India au Afrika ya Kusini kwa wale wenye uwezo  wa kujigharamia  vinginevyo kwa maskini walio wengi  huishia  watoto wenye matatizo makubwa yanayoitaji utambuzi wa mashine hiyo, huishia kufa.  

Aidha  madaktari wanalalamika   jinsi wanavyoshindwa kuokoa maisha ya watoto   wanaozaliwa na tatizo la koromeo  la chakula kuungana na koromeo la hewa. Mabingwa wa upasuaji  wa watoto katika hospitali hiyo  wanasema kwa upande wao wanajitahidi kuwafanyia  watoto hao upasuaji, lakini watoto hao huishia  hufariki dunia  kutokana na hospitali hiyo ya Rufaa kukosa  vifaa maalum vya kuhudumia watoto hao na vyumba maalumu vya kuwaweka  baada ya kufanyiwa operasheni.  

“Kinauma sana  na kinakatisha tamaa sana kuona kwamba mtoto anafanyiwa   upasuaji vizuri lakini anapoteza maisha siku chache baadaye kutokana na kukosekana kwa vifaa na mazingira ya kumwezesha  kupona baada ya upasuaji”, anasema  Dakta Catherine Mungo’ngo, Bingwa wa upasuaji wa watoto Hospitali ya Rufaa ya Taifa.

Kwa mujibu wa bingwa huyo kwa mwaka huu pekee watoto watatu  waliozaliwa na tatizo la la koromeo  la chakula kuungana na koromeo la hewa ambao  walifanyiwa upasuaji  Muhimbili,    baadaye  walikufa hospitalini hapo kutokana na kukosekana kwa vifaa vya kuwasaidia kupumulia na chumba maalumu  cha kuwafanyia uangalizi baada ya upasuaji.

Aidha anasema watoto  kati ya 6 hadi 8 wanaohitaji kufanyiwa upasuaji kwa siku, upasuaji huo huahirishwa kutokana na ukosefu wa vifaa , dawa na chumba maalum cha kuwatunzia baada ya upasuaji.

Ni mtu gani mwenye akili timamu  ambaye atafurahia  kuona kazi anayoifanya  haitoi  matunda yanayotarajiwa.?  Ni Daktari gani atakayeendelea kufurajhia kazi yake wakati lengo lake la kuokoa maisha ya watu  linakwamishwa  na  mambo yanayowezekana kurekebishwa?

Daktari furaha yake ni kutibu mgonjwa na kuona anapona. Lakini Daktari katika hospitali za  serikali  atafanyaje kazi yake kuepusha vifo  visivyo vya lazima kama hana vifaa vya kufanyia kazi ?   

Nionavyo mimi,  serikali yetu inapaswa kutafakari tena kwa utulivu na busara kubwa  na kuweka mikakati ya kupata suluhisho la kudumu la mgogoro  wake na madaktari. 

Vinginevyo hata kama wataagizwa  madaktari kutoka Ulaya, na wa hapa nchini kufukuzwa kazi au hata kama viongozi wao ‘watashughulikiwa’,  tatizo la  mazingira ya kazi  hospitalini ambalo ni moja  ya  mambo ya msingi   linalosababisha mgomo wamadaktari   litakuwa halijashughulikiwa  na litaendelea kujirudia  hata kama litapoozwa   kwa mbinu yoyote ile.

 Na ikumbukwe watakaoendelea kuumia zaidi hapa ni wananchi wengi  ambao maisha yao yanategemea uwajibikaji wa serikali yao.

Nijuavyo mimi, serikali  ya wananchi, madaktari wakiwa ni sehemu ya wananchi, husikiliza kero za wananchi na kuzishughulikia badala ya kutumia mabavu na vitisho. 

Mungu ibariki Tanzania.


Ananilea Nkya 

Executive Director 
Tanzania Media Women’s Association (TAMWA) 
P. O. Box 8981, Sinza-Mori 
Dar es Salaam, TANZANIA 
Tel: +255-22 2772681 
Fax +255 22 2772681 

E-mail: ananilea_nkya@yahoo.com
Cellphone:+255-754-464-368

Leave a comment


Klabu ya soka ya Arsenal ya nchini Uingereza, jana imesaini mkataba wa ushirikiano wa miaka mitatu na kampuni ya mawasiliano ya simu barani Afrika ya Airtel.
Mkataba huo unaipa fursa Airtel kutumia bidhaa za klabu hiyo kwenye nchi tano za barani Afrika: Nigeria, Zambia, Ghana, Uganda na Rwanda.
Makubaliano hayo yataisaidia klabu hiyo ya kaskazini mwa London kuwafikia mashabiki wake milionu 42 barani Afrika.
Wateja wa Airtel nchini Nigeria, Zambia, Ghana, Uganda na Rwanda wataweza kujishindia tiketi za mechi kushuhudia mechi zao na kupokea habari kuhusu klabu hiyo kwenye simu zao.
Pia makubaliano hayo yataifanya kampuni ya Airtel kuwa kampuni rasmi ya simu kwenye ziara ya mwaka huu ya Arsenal nchini Nigeria.
Arsenal pia itasupport program ya soka ya Airtel Rising Stars, mafunzo ya kila mwaka yanayowapa vijana wa Afrika fursa ya kucheza soka na kushindana kwenye mazingira salama.
Airtel huchangia fedha kwa kila goli linalofungwa kwenye shindano hilo kusaidia elimu ya wachezaji hao kuhakikisha kuwa wale wanaoshiriki hawapati tu mafunzo bora ya mchezo huo bali pia fursa za masomo zaidi ya darasani.Mkuu wa ushirikiano wa kimataifa wa Arsenal, Vinai Venkatesham alisema: “Nimefurahi kuwakaribisha Airtel kwenye familia ya washirika wa kibiashara. Haya ni makubaliano makubwa ya pili na marefu kutokea barani Afrika na tunaratajia kufanya masuala mengi na Airtel, tukianza na ziara ya Nigeria mwezi August.”

source:bongo5

Older Entries

%d bloggers like this: