Home

ALICHOKIANDIKA JOSE CHAMELEONE KUHUSU ERICK SHIGONGO KUENDELEA KUISHIKILIA PASSPORT YAKE.

Leave a comment


Kama kumbukumbu zako zipo fresh, muda mfupi baada ya Jose Chameleone kumaliza show yake Uwanja wa taifa July 7 2012 na kufanya kama walivyokubaliana kwenye mkataba, siku mbili baadae stori gazetini ziliandikwa kwamba mwimbaji huyu staa wa Uganda ameshindwa kurudi kwao kutokana na Passport yake ya kusafiria kushikiliwa na Eric Shigongo C.E.O wa Global Publishers walioandaa show hiyo kutokana na kumdai pesa ambazo ilidaiwa alishawahi kulipwa kipindi cha nyuma kuja kufanya show Tanzania lakini hakutokea.
Pamoja na hati yake ya kusafiria kuzuiliwa na Erick Shigongo, aliweza kusafiri kurudi kwao… sasa baada ya kuwa kimya kidogo…… hiki ndicho alichoandika kwenye ukurasa wake wa facebook kuhusu hiyo ishu.
Kwa ufupi ni kwamba Jose Chameleone amemlalamikia Big Boss Erick Shigongo kuhusu kuendelea kuishikilia Passport yake wakati meneja wake Chemeleone hakuhusika kuchukua hizo dola za Kimarekani 3500 zinazodaiwa kupokelewa na Meneja wa Chameleone kwa ajili ya show iliyopangwa siku nyingi kidogo.
Chameleone amesema aliporudi Uganda alifanikiwa kumkamata na kumpeleka polisi George, mtu ambae ndio anadaiwa kuzichukua hizo pesa akijidai ni meneja wa Chameleone lakini baadae akaachiwa huru ambapo baada ya kuona hivyo ilibidi Chemeleone aende kwa balozi wa Tanzania Uganda ili kupata msaada lakini hakufanikiwa.
Amesema wakati passport yake ilipozuiliwa na Erick Shigongo alikwenda kwenye ubalozi wa Uganda Tanzania na ndio uliomsaidia kumpa Document zilizomuwezesha kurudi nyumbani, kwa sasa amepata mialiko ya shows South Africa, England, Belgium, Norway, Sweeden, Canada n.k lakini hajui itakuaje na anahitaji ushauri kuhusu Erick Shigongo ambae ameshikilia Passport yake kwa zaidi ya mwezi mmoja.

source:millardayo

Maafa Ya Kuzama Kwa Meli, Watu 30 wa Fariki dunia mpaka Asubuhii!!

Leave a comment


Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia Julai 19 hadi Julai 21 kufuatia maafa ya ajali ya Meli ya Mv. Skagit iliyozama karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein akitangaza maombolezo hayo, alisema bendera zote zitapepea nusu mlingoti na kwamba shughuli za sherehe na burudani zimefutwa kwa muda wa siku tatu za maombolezo.

Dk. Shein alisema shughuli za Serikali zitaendelea kama kawaida. Katika taarifa yake aliyoitoa Ikulu usiku wa kuamkia Julai 19, Rais Dk Shein amewahakikishia wananchi na hasa waliopoteza jamaa zao kuwa Serikali itabeba gharama zote za mazishi na pia kugharamia huduma za matibabu kwa majeruhi.

“Nimesikitishwa sana na msiba huu, Katika wakati huu si vema tukaanza kulaumiana jambo la muhimu hivi sasa ni kuokoa maisha ya watu” Alisema Rais Dk. Shein.

Mbali ya taarifa hiyo, Rais Dk Shein aliungana na wananchi, viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, Viongozi wa dini katika kutambua maiti zilizofikishwa katika eneo maalum la viwanja vya Maisara Suleiman.

Mbali ya kwenda katika viwanja hivyo, pia alifika katika eneo la bandari ya Zanzibar kufuatilia taarifa za tukio hilo. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana lilisitisha shughuli zake kufuatia maafa hayo ambapo wakati wa jioni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Nchimbi alitarajiwa kufanya majumuisho ya bajeti yake.

Baadhi ya Wabunge wakiongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Jeshi la Polisi walitembelea majeruhi katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja pamoja na eneo la viwanja vya Maisara ambapo maiti hufikishwa kwa ajili ya utambuzi.

Mbali ya Bunge, pia Baraza la Wawakilishi Zanzibar jana lilisitisha kwa muda shughuli zake ili kutoa nafasi kwa Wawakilishi hao wa wananchi kushiriki katika shughuli za uokozi ambapo wengi walifika bandarini kusaidia kazi mbalimbali ikiwemo kuwafariji waliopoteza ndugu zao.

Taarifa kutoka Mamlaka za Serikali zinaeleza kwamba hadi asubuhi hii maiti 30 zilipatikana ambapo 20 kati ya hizo zimetambuliwa na kuchukuwa na jamaa zao huku wananchi wengine wakiendelea na kuzitambua maiti zinazofikishwa katika eneo la Maisara.

Aidha, katika taarifa hiyo, watu 145 wameokolewa wakiwa hai, wengi wao wapo katika hali nzuri wameruhusiwa kuungana na familia zao baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar.

Meli ya Mv. Skagit ilizama Julai 18,2012 saa 7:50 mchana ikitokea Bandari ya Dar es Salaam kwenda Zanzibar ikiwa imebeba abiria 250 watu wazima, watoto 31 na mabaharia 6.

Kazi ya utafutaji na uokoaji zinaendelea asubuhi hii katika eneo la tukio ilikozama meli hiyo umbali wa maili sita Kusini mwa Kisiwa cha Yasin karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.

Happy Birthday Mandiba “NELSON MANDELA”

Leave a comment


Nelson Rolihlahla Mandela alizaliwa tarehe 18 Julai, mwaka 1918. Ni rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini Afrika Kusini. Alikuwa mwanasheria na mwanachama wa ANC aliyepinga siasa ya Apartheid katika Afrika Kusini. Mandela alitumikia kifungo cha maisha kwa miaka 27 kutokana na harakati zake za kuupinga ubaguzi wa rangi. Alifungwa katika kisiwa cha Robben. Baada ya kuachiliwa huru mwaka 1990 alianzisha sera ya maridhiano. Mwaka wa 1993, pamoja na Frederik Willem de Klerk alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani.
Jumanne hii rais wa zamani Bill Clinton alienda nyumbani kwa Nelson Mandela Kumtakia kila la heri katika kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa. hata hivyo
Rais Barack Obama na Mke wake Michelle Obama, jana pia walimtumia salamu za pongezi kwa Mandiba kwa heshima ya juu zaidi. “ kwa niaba ya watu wa Marekani, Tungependa Kutoa pongezi zetu za dhati kwa siku ya kuzaliwa ya miaka 94 na mwaka wan ne wa kuadhimisha siku ya kimataifa ya nelson Mandela’s day”. Alisema Obama

ALICHOSEMA CHEGE KUHUSU USALAMA WAKE BAADA YA KUPATA AJALI USIKU.

Leave a comment


Inawezekana stori ya msanii CHege wa TMK WANAUME FAMILY kupata ajali umeshaisikia mpaka sasa, lakini na uhakika haujasikia kingine alichozungumza exclusive na AMPLIFAYA, nilifanya nae interview jana usiku saa tano na dakika 17 akiwa hospitali ya Temeke.Siku zote kuna maeneo ambayo huwa tunaonywa kwamba hata kama tairi la gari yako likiisha upepo usisimame, Temeke pia ni sehemu hatari kwenye ishu kama hizo… mi siku moja usiku nilishawahi kukutana na jamaa wamevaa sare alafu wanasema wanatengeneza taa kumbe sio, ni wakabaji.Pamoja na kwamba Temeke inatajwa kutokua nzuri kiusalama hasa linapotokea swala la ajali, Gari la Chege halijaibiwa hata kitu kimoja lilipopata ajali hiyo jana saa nne usiku, sababu kubwa na pekee ambayo imemuokoa chege ni kwa sababu ni mtoto wa kiumeni, mtu wa watu, umaarufu pia umemsaidia.Chege amesema watu waliosogelea eneo la ajali baada tu ya ajali kutokea na watu kukusanyika, baada tu ya kujua ni yeye ndio kwanza walianza kulilinda gari.. hakuna chochote kilichoibiwa.

source:millardayo

AJALI MBAYA YA BASI LA BUNDA IMETOKEA GEITA,WATU 11 WAFARIKI PAPO HAPO NA 12 WAJERUHIWA.

Leave a comment


MKUU wa mkoa wa Geita Magalula Said Magalula akiangalia miili ya marehemu waliokufa katika ajali ya Gari leo mchana Wilayani Geita,miili hiyo ilikuwa imelazwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya hiyo.Picha na David Azaria. (Source http://www.hakingowi.com/)

Watu wamefariki Dunia Papo hapo hapo na wengine 12 wakijeruhiwa vibaya baada ya magari matatu mawili kati yao yakiwa ni ya abiria waliyokuwa wakisafiria kupata ajali na kupinduka wilayani Geita Mkoani Geita.

Tukio hilo limetokea leo Jumapili majira ya saa 8:30 katika kijiji cha Chibingo kata ya Katoro eneo ambalo mwaka jana kulitokea ajali ya basi la Bunda na kuua watu 14 papo hapo na kujeruhi wengine 28.

Katika tukio hilo watu 9 wakiwemo watoto watatu wamekufa papo hapo,huku wengine wawili mmoja akifariki njiani wakati wa kukimbizwa hospitalini huku mwingine akifariki wakati akipatiwa matibabu na madaktari katika chumba cha Upasuaji.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Geita Paul Kasabago amelithibitihishia gazeti hili kuwepo kwa tukio hilo,na kueleza kuwa ajali hiyo ni mbaya nay a kwanza kutokea katika kipindi cha mwaka huu huku akitaja magari yaliyopata ajali kuwa ni zenye namba T 344 AZE zote aina ya Toyota Corola,na T 421 BHS Toyota land Cruiser.

Aliwataja waliokufa papo hapo katika ajali hiyo kuwa ni Maria Elisante (18) mkazi wa Mganza wilayani Chato,Masasila Benjamin (17) mkazi wa Mkolani mjini Geita,James Ntungirwenge (36) Mkazi wa Nyankumbu Geita,na Eliud Ngovongo (36) pamoja na watoto wake watatu Amin (10),Emison(7),na Sara(4) wote wakazi wa Kalangalala mjini Geita.

Alisema bado majina ya marehemu watatu mpaka jioni ya jana yalikuwa bado hayajatambuliwa,huku akibainisha kwamba tayari marehemu saba kati ya 11 waliofariki wametambuliwa na ndugu zao.

Kamanda Kasabago alisema katika tukio hilo watu 12 wamejeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya wilaya ya Geita,huku wanne kati yao ambao hali zao ilionekana kuwa mbaya wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando kwa matibabu zaidi.

Mganga mkuu wa Wilaya ya Geita Dk.Abdalah Dihenga jana aliwaongoza madaktari wengine kutoa huduma kwa majeruhi,ambapo mwandishi wa Gazeti hili aliwashuhudia wakitoa huduma kwa wagonjwa katika chumba cha upasuaji hospitalini hapo.

Akisimulia tukio kamanda Kasabago alisema chanzo cha ajli hiyo mbaya ni mwendo kasi wa magari mawili madogo ya abiria yajulikanayo kwa jina la ‘Michomoko’ ambayo yaligongana uso kwa uso na gari linguine aina ya Land Cruiser.

Kamanda Kasabago alisema magari hayo mawili yalikuwa yakifukuzana kutoka mjini Geita kwenda Katika mji mdogo wa katoro huku yakiwa na abiria,ambapo baada ya kufika katika eneo hilomoja liliamua kulipita lingine na ghafla likakutana na gari linguine mbele.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Said Magalula alifika katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Geita,na kushuhudia miili ya marehemu iliyokuwa imelazwa chini katika chumba hicho.

Akizungumza na mamia ya wananchi waliokuwa wamefurika nje ya Viwanja vya jingo hilo la kuhifadhia maiti katika hopspitali ya wilaya hiyo Mkuu huyo wa Mkoa alitoa pole kwa wafiwa,na kuwataka kuwa na moyo wa subira wakati wa maombolezo ya vifo vya ndugu jamaa na marafiki zao.

source:dewjiblog.

KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI TIGO YAKUTANA NA BLOGGERS JIJINI DAR.

Leave a comment


Meneja wa Promosheni na Matukio wa Kampuni ya simu za mkononi TIGO Bw. Allan Shilla akizungumza na Bloggers katika hafla fupi iliyoandaliwa na Kampuni hiyo katika hoteli ya Kebby’s jijini Dar yenye lengo la kufahamina na kubadilishana mawazo ambapo wameahidi kuwa karibu na mitandao ya Kijamii inayokua kwa kasi katika kupashana habari pamoja na kutoa offer kemkem zikiwemo line za simu bure, huduma ya Mega Box kwa bloggers wote waliohudhuria na vifurushi vya kutumia bure kwa mwezi mzima.

Blogger Rajabu Mhamila mmiliki wa http://burudan.blogspot.com/ akijitambulisha mbele wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi TIGO pamoja na Bloggers wenzake.

Mmiliki wa http://othmanmichuzi.blogspot.com/ na msaidizi wa http://www.issamichuzi.blogspot.com/ Othmani Michuzi akitiririka wakati wa hafla hiyo.

Mmiliki wa mtandao wa http://missiepopular.blogspot.com/ Mariam Ndabagenda wakati wa utambulisho.

Baadhi Wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi TIGO.

Baadhi ya Wamiliki na wasimamizi wa Mitandao mbali mbali nchini wakiwa kwenye picha ya Pamoja wakati wa Tafrija Fupi iliyoandaliwa na Kampuni ya simu za Mkononi Tigo ambapo yenye lengo la kufahamiana na kujenga mahusiano mazuri.

PR Agencies wa TIGO kutoka kampuni ya Trinity wakijitambulisha kwa Bloggers.

Bloggers http://missiepopular.blogspot.com/ (Kushoto) na Mwanzilishi wa http://www.jamiiforums.com/ wakibadilishana mawazo.

source:dewjiblog

Picha 26 za Pambano dhidi ya Bongo Movies na Bongo Fleva

Leave a comment


This slideshow requires JavaScript.

Mamia kwa maelfu ya wakazi wa jiji la Dar-Es-Salaam na vitongoji vyake walifurika katika uwanja mkuu wa taifa kushuhudia tamasha la burudani mbali mbali za kimuziki, Ndondi pamoja na mpira wa miguu uliohusisha wabunge wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania wanaoshabikia timu za Yanga na Simba, Bongo Flava dhidi ya Bongo Muvi, mpambano wa Wema na Jackline Wolper na mwisho kabisa Ngumi kati ya bondia Japhet Kaseba na Francis Cheka.
Tamasha hilo lililoandaliwa kwa pamoja baina ya Kampuni ya Global Publishers kupitia kitengo chake cha Burudani kwa kutumia platform yao ya ukumbi wa burudani Dar Live, pamoja na mfuko wa elimu na kulipa jina tukio hilo kuwa la Tamasha La Matumaini lilikuwa mahususi kuchangia mfuko wa elimu kwa wasichana katika ujenzi wa mabweni katika shule ya Kongwa mkoani Dodoma…
Watu wa marika mbali mbali walihudhuria tamasha hilo ambalo lilianza rasmi majira ya saa tisa kamili ambapo timu ya Bongo Fleva ilipambana na timu ya Bongo Muvi na timu ya Bongo Fleva kuondoka na ushindi wa goli moja dhidi ya Bongo Fleva katika pambano lililokuwa la kuvutia na vituko pamoja na vibweka kibao. Alikuwa… ambaye aliwainua mashabiki wa Bongo Muvi baada ya kufunga goli katika dakika ya 64 ya kipindi cha pili.
Mastaa kama Claude 112, Steve Nyerere, Abdul Kiba, H baba, TID, Inspector Harun, Vincent Ray kigosi na wengineo walitoa burudani ya kutosha kwa kucheza mpira uliofurahisha na kusisimua wengi. Aidha burudani kubwa ilikuwa baada ya kipyenga cha refa Othman kazi kupulizwa kuashiria mechi imeisha ambapo wachezaji wa Bongo muvi walikwenda kushangilia ushindi kwa mashabiki wao huku wakicheza kwaito na steve Nyerere kuvua jezi yake na kuonyesha maandishi ya “why Always Me? ”. kitendo kilichofanya wamfananishe na Balotelli

sourcebongo5

Older Entries

%d bloggers like this: