“Next time nikikuta watu wanapiga mwizi na mtu akanizuia nisishiriki ntaanza na yeye kwanza” ni tweet ya jana ya Hamisi Mwinjuma aka MwanaFA iliyokuwa imeambatanishwa na picha ya gari lake lenye namba T 809 PMB ikiwa imenyofolewa taa zote za mbele na nyuma.

Wizi huo umefanyika usiku wa kuamkia jana na inavyoekena ni kuwa wezi walipanda na kuvuka geti kimya kimya, kwa raha zao wakanyofoa taa na kuingia ndani kuchukua radio.

Ile MwanaFA kuamka asubuhi ndo akakuta tayari wajanja wameshamliza kiasi cha kuamua kutangaza vita na wezi. Hivyo kama ukikuta MwanaFA anashiriki kumponda ‘vitofa’ mwizi aliyekamatwa street baada ya kuiba, kamwe usishangae, usimuulize na usimzuie sababu ataanza na wewe! Pole sana Binamu!

Hata hivyo wezi hao hawaikuiharibu ratiba ya usiku wa kuamkia leo ya Binamu. Ratiba yake ilianzia pale the so-called ‘Uwanja wa taifa wa burudani’ Dar Live ambapo aliperform ngoma yake mpya Ameen kwa mara ya kwanza.

Baada ya Dar Live show ikahamia Maisha Club, “Dar Live Done..Beautiful..Maishani Sasa Kwa Ndege Mnana,” alitweet.

Huko New Maisha Club alienda kumpa support mwanadada Linah Sanga aliyekuwa akifanya show yake ya kwanza tangu arudi kutoka kwenye ziara ndefu ya nchini Marekani. “What a show..Maisha I Loooooooooved you tonite!” aliandika alfajiri hii.

source:bongo5