Home

ARSENAL IMESEMA HAITAMWACHIA Robin Van Persie

Leave a comment


Klabu ya Arsenal kamwe imesema haitamwachia Mshambuliaji wake Robin Van Persie kuihama klabu hiyo ya kaskazini mwa London licha ya kubakiza mwaka mmoja wa kukaa klabuni hapo.Mdachi huyo ameonekana dhahiri kutaka kuihama klabu hiyo kutokana na uhaba wa mataji na amekuwa katika mazungumzo na Kocha wake Arsena Wenger na Mwenyekiti wa Washika bunduki hao wa kaskazini mwa London, Ivan Gazidis. “We are going to keep him and hold him to his current contract,” a senior source told Goal.com. “When he is 30 it will be easier to re-sign him and in the last year (of his deal) we hope he will change his mind about wanting to leave.”

Aquilani kubaki Liverpool.

Leave a comment


Msemaji wa mchezaji Alberto Aquilani amesisitiza ya kuwa Aquaman (Aquilani) atakuwa mchezaji wa Liverpool msimu ujao na kuwa hatoondoka.
Mchezaji huyo mwenye asili ya kiitalia alisajiliwa na Liverpool mwaka 2009-10 kutoka klabu ya Roma lakini kutokana na majeruhi yaliyopoelekea kiwango chake kupungua alijikuta akitolewa kwa mkopo. Mchezaji huyo anamkataba na Liverpool mpaka mwaka 2014.
Akiongea na calciomercato.com, msemaji wa mchezaji huyo aitwaye Franco Zavaglia alisema,
“Atachezea Liverpool msimu ujao. Kuna machache ya kusema kuhusiana kilichotekea na AC Milan, msimu umeisha na nauhakika Aquilani atalitupia mbali swala hilo la AC Milan.
Alberto yupo Uingereza kwa sasa na bado ni mchezaji wa Liverpool. Ataichezea Liverpool msimu ujao”.

source:skysports

Hasheem Thabeet kusaini na kucheza kesho na Thunder

Leave a comment


Mchezaji wa mpira wa kikapu cha kulipwa katika ligi ya NBA ya Marekani, mtanzania Hasheem Thabeet kesho Jumatano, anatarajiwa kusaini mkabata rasmi wa miaka miwili kukipiga na timu ya Oklahoma City Thunder.
Kama akisaini kesho anaweza kucheza kwenye mechi tatu za mwisho akiwa na timu yake mpya kwenye Orlando Pro Summer League.
Thabeet hawezi kusaini rasmi mkataba wake mpya na Thunder hadi kesho pindi msitisho rasmi wa free agent huyo ukitolewa. Kabla ya hayo kufanyika, bado sio mchezaji wa kimkataba na timu ya Thunder.
Hata hiyo haimkatazi Thabeet kucheza kwakuwa wachezaji kumi kati ya 14 wa OKC kwenye roster ya summer league hawana mkataba na Thunder.
Lakini wachezaji hao kumi hawana siku moja tu zilizosalia ili kusaini mkataba unaohusisha malipo kama Thabeet.
Wachambuzi wa masuala ya mchezo huo nchini Marekani wanasema kuwa Thabeet anaweza kusaini mkataba huo kesho asubuhi kwa saa za Marekani na kuingia uwanjani rasmi.
Thabeet anatarajiwa kujiunga na timu yake wiki hii mjini Orlando na anaweza kushiriki kwenye mazoezi wiki hii yote na kama kesho akisaini mkataba hakutakuwa na chochote tena cha kumzuia kucheza.
Ni wachezaji wachache wanaohitaji muda wa kucheza kumzidi Thabeet, na ndo maana ni lazima acheze wiki hii.
Kwa misimu miwili iliyopita Thabeet amecheza kwa dakika 512 tu.

Mtandao wa Thunderumblings wampa ushauri Hasheem Thabeet

Leave a comment


Jana ilibainika wazi kuwa mtanzania Hasheem Thabeet amesaini mkataba wa kuichezea timu ya Oklahama City Thunder kwaajili ya misimu miwili ya ligi ya NBA ambapo kwa mwaka atakuwa akilipwa dola 880,000.
Hata hivyo tangu Hasheem aanze kucheza kwenye ligi ya NBA, hajawahi kuonesha kiwango cha kuridhisha na hivyo kujikuta akikoselewa mara nyingi na waandishi wa Marekani.
Hata hivyo mwandishi wa mtandao wa ThunderRumblings uliojikita katika kuandika habari za timu mpya ya Hasheem, Darnell Mayberry amempa ushauri wa kumsaidia mchezaji huyo kama anavyasema:
“Sio rahisi kwa Thabeet kuingia uwanjani mara nyingi msimu ujao. Kitu muhimu kwa Thunder, na Thabeet, ni kufocus kwenye maendeleo.
Ni wazi, kuna kipaji ndani ya urefu wa Thabeet wa 7-foot-3. Hakuwa mchezaji bora wa mwaka wa defense kwa misimu miwili na Co-Big East Player of the Year kwenye msimu wa mwisho wa UConn bure.
Lakini huu ni muda sasa wa kukitumia kipaji hicho. Ni muda wa Thabeet kufanya kazi.
Hii itakuwa ni timu ya nne kwa Thabeet ndani ya misimu minne baada ya kuwa drafted kama mchezaji wa pili kwenye usajili mwaka 2009. Tunaamini kuwa hii ndo itakuwa ni nafasi ya mwisho kuthibitisha kuwa anastahili kuwepo kwenye ligi ya NBA.
Lakini kitu cha kwanza ambacho Thabeet anatakiwa kufanya kuonesha kuwa muda huu, timu hii itakuwa tofauti na misimu mitatu iliyopita ni kwenda Orlando kuungana na wachezaji wenzake wapya kwenye summer league.
Mara nyingi wachezaji maarufu huwa hawashiriki kwenye ligi hii. Lakini katika mtu ambaye anatakiwa kujifanya mjinga ni Thabeet. Kama mimi ningekuwa Thabeet, ninajitolea kwenda na kushindana badala ya kusubiri kocha aniambie niende.

Ni kitu rahisi kuweka ‘good first impression’ na kuprove kuwa yaliyopita, yamepita. Uthibitisho kuwa sasa yupo tayari kufanya kazi kwa bidii na kufanya kinachotakiwa kustawi kuwa mchezaji ambaye wengi waliamini alikuwa na sifa za kuwa.

Iwapo hakuna kingine. Ni nafasi ya kucheza. Na Mungu anajua Thabeet anahitaji hilo.
Kwenye misimu minne iliyopita, Thabeet amecheza kwa dakika 512 pekee. Kwa kulinganisha, mchezaji (guard) chipukizi wa Thunder Reggie Jackson alicheza dakika 501 msimu huu. Ukitengenisha muda wake akiwa na Houston na Portland mwaka huu, Thabeet alicheza dakika 139 tu. Kevin Durant alicheza dakika 213 kwenye fainali za NBA dhidi ya Miami pekee.
Muda wa uwanjani ndicho kitu anahitaji Thabeet kuliko kingine chochote. Kama hatocheza, ama kutokuwa mchezaji aliyetegemewa kuwa defender mzuri, basi na iwe. Lakini kuna njia moja ya kutoka.
Thabeet anahitaji kuchukua hatua hiyo ya kwanza. Anahitajika kwenda Orlando.”

source:bongo5

Lets the Game beginning:Chris Brown akubali kuingia ulingoni na Drake kuzichapa

Leave a comment


Hatimaye Chris Brown ameizungumzia ofa iliyotolewa na tajiri wa Marekani Alki David ya kuingia ulingoni kuzichapa na adui yake Drake kwa malipo ya dola milioni 9 kwa mshindi na milioni moja kwa loser.
Pambano hilo litakuwa na raundi tatu zenye dakika moja.
Kwa mujibu wa mtandao wa RumorFix, miongoni mwa wapiga picha wa mtandao huo alionana na Chris Brown jana na kumuuliza kama anaweza kukubali ofa hiyo na yeye kujibu,”Yeah, I would. I would.”
Siku chache zilizopita Chris Brown ametoa wimbo wa kumdiss Drake na hivyo kuchochea zaidi beef lao.Drake amesema hatojibu diss hiyo.
Katika taarifa nyingine, wakati ambapo kila msanii amejaribu kuzungumzia beef inayoendelea kati ya Chris Brown na Drake, wapo ambao wameamua kuchukua upande mmoja.
Ukianzia kwa Gayle King ambaye alisema yupo kwenye timu ya rizzy hadi kwa Big Sean aliyesema Breezy ndio mwana wa ukweli zaidi.
Hata hivyo mwanadada Kelly Rowland amesema yeye anabaki neutral na kukubali kuwa anawazimia wote.
“Oh, huwezi kunifanya nichague. Ukweli ni kwamba nawapenda wote,” nyota huyo aliuambia mtandao wa Bossip.
“Ni wasanii wazuri. Sidhani kwamba mtu yeyote anatakiwa kuchagua kati yao.

Hii Ni kazi Mpya ya Fid Q Feat. Yvonne Mwale – Sihitaji Marafiki (Official Video)

Leave a comment


HII NDIO MANENO YA RAFAEL VAN DER VAART MPAKA SASA.

Leave a comment


Rafael van der Vaart amesisitiza kwamba hakuna mawasiliano yoyote yanayofanyika kati yake na club ya Hamburg japo bado kuna fununu kwamba club hiyo ina mpango wa kumpa mkataba mpya.
The Dutch midfielder bado ananyenyekewa na mashabiki kutokana na kazi nzuri aliyoifanya kwa miaka mitatu ambapo kwa mujibu wa skysports, Hamburg-based billionaire Klaus-Michael Kuehne yuko tayari kuisaidia club kumpa gamba jipya Tottenham playmaker Van der Vaart.

Older Entries

%d bloggers like this: