Home

HAWA NDIO WACHEZAJI WA SIMBA KOCHA ALIOSEMA HARIDHISHWI NA VIWANGO VYAO.

Leave a comment


KOCHA Mkuu wa Simba Milovan Cirkovic amesema kikosi chake hakipo imara katika kiwango kile anachokihitaji kwa ajili ya Michuano ya Kagame ambayo timu nyingi zinajiandaa vizuri.
Wachezaji ambao viwango vyao havijamridhisha ni Haruna Moshi ‘Bobani’, Mwinyi Kazimoto, Juma Nyosso na Amir Maftar na hivyo amepanga kuwapa mazoezi kuwarudisha kwenye line.
Simba inatarajiwa kucheza mechi yake ya kwanza Jumatatu ijayo na URA ya Uganda saa kumi jioni na mchezo mwingine utapigwa kati ya Villa Club na Ports saa 8:00 mchana kwenye Uwanja wa Taifa. (Stori imeandikwa na shaffihdauda.com)

Simba Fc Kumsajili MUSSA MUDDE KUTOKA UGANDA CRANES.

Leave a comment


Akiwa tayari amesign mkataba wa kuichezea Simba SC msimu huu, mchezaji kiungo Mussa Mudde (Pichani) kutoka timu ya taifa ya Uganda anatarajiwa kuwasili jijini Dar-es-salaam leo kwaajili ya kukamilisha taratibu mbalimbali za uhamisho.
Mzungumzaji wa Simba SC Ezekiel Kamwaga amesema tayari Mudde amesajiriwa kwa mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo ya Msimbazi.
Mudde ambaye ameichezea timu ya Sofapaka kutoka Kenya kwa kipindi cha miaka miwili na nusu, sasa anajiunga na Mganda mwenzie Emmanuel Okwi kuitumikia Simba SC.

chameleone kushuka Bongo kufanya show kwenye Uwanja wa Taifa

Leave a comment


Msanii wa muziki kutoka Uganda, Jose Chameleone Picha Juu akiwa anakamilisha taratibu zote za kusaini mkataba wa kufanya shoo kali Uwanja wa taifa , Jijini Dar es Salaam, Siku ya sabasaba baada ya meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho baada ya kutia timu Entebe

CHAMELEONE AKIJIGAMBA KUFANYA SHOO KALI BAADA YA KUSAINI MKATABA WA MWEISHO , CHAMELEONE AMETOA ONYO KWA DIAMOND ATAMCHAKAZA NA VALIVALU

source:issamichuzi

WAFANYAKAZI WA UN-WAGOMA

Leave a comment


Wafanyakazi katika ofisi ya Umoja wa Mataifa iliyoko mjini Entebe, Uganda wamefanya mgomo jana Jumatatu kulalamikia mazingira mabaya ya kufanyia kazi pamoja na kutaka nyongeza ya mishahara.

Wafanyakazi zaidi ya 120 walianza mgomo leo asubuhi na hivyo kukwamisha shughuli katika ofisi hiyo ya UN. Wafanyakazi hao wanasema kuwa Umoja wa Mataifa umeipa kampuni ya kibinafsi kandarasi ya kuendesha ofisi hiyo na kwamba kampuni hiyo sasa imekata mishahara yao kwa asilimia kubwa. Wameongeza kuwa hawana bima za afya wala barua za kuajiriwa na hivyo wanahisi kuwa UN inawafanya kuwa watumwa katika nchi yao. Wafanyakazi hao wamesisitiza kuwa hawatorudi kazini hadi pale mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Nchini Uganda atakapofika katika eneo hilo na kutatua matatizo yao.

MCHUNGAJI KIWEDDE ARUDISHWA RUMANDE KWA TUHUMA ZA KULA NJAMA ZA UBAKAJI.

Leave a comment


Mchungaji wa nchini Uganda William Muwanguzi a.k.a Pastor Kiwedde amerejeshwa rumande kwa tuhuma za kula njama na wenzie waliombaka mwanamke wa miaka 30.
Makamu mzungumzaji wa polisi, Judith Nabakooba amesema Kiwedde na wanaume wenzie watatu, wakisafiri katika gari binafsi waliwachukua wanawake wawili kutoka pub ya Kabuusu na kuwapa ofa ya kwenda kunywa.
Wanawake hao baadae walipatwa na wasiwasi na kujaribu kutoroka ambapo mmoja wao alifanikiwa, wakati aliebaki alibakwa na wanaume hao wawili.

%d bloggers like this: