Home

HAWA NDIO WANAUME WATATU WALIOPOTEZA MAISHA KWA KUWAKINGIA VIFUA WAPENZI WAO.

Leave a comment


Huyu ndio James Holmes mtuhumiwa wa mauaji ya watu 14 kwenye ukumbi huo wa Cinema, alijeruhi watu wengine 58 pia. hapa ni akiwa amefikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza

Imefahamika kwamba kuna wanaume watatu walipoteza maisha kati ya watu 12 waliofariki kwa kupigwa risasi wakati wakichek movie ijumaa iliyopita Century Cinemas in Aurora, Colorado Marekani, tukio ambalo limepata nafasi kubwa sana kwenye headlines Marekani na sehemu nyingine za dunia.

Hao wanaume watatu walipoteza maisha kwa kupigwa risasi na James Holmes mtu aliyeingia ghafla kwenye ukumbi wa cinema, akatupa mabomu ya machozi na kuanza kufyetua risasi ovyo.

Safari ya maisha ya hawa wanaume watatu ilifikia mwisho baada ya wote watatu kujitokeza na kuwakingia kifua wapenzi wao baada ya risasi kuanza kupigwa ovyo, ambapo girlfriends hao wote watatu waliepuka kifo.

source:millardayo

HICHI NDICHO ALIYOYASEMA DIAMOND PLATNUMS KUMALIZA MJADALA NA BABA YAKE.

Leave a comment


Baada ya stori kuandikwa kwenye magazeti kwamba Staa Diamond Platnums anadaiwa kumtelekeza baba yake na hamjali wala hataki kusikia stori zake, hii ndio kauli ya Diamond kuhusu hiyo ishu.

Amesema “kiukweli ni vitu ambavyo mimi vimenishangaza sana kwa sababu sijui chochote nakuja kukuta tu kwenye magazeti, na nisingependa nisikie swala la mzazi wangu kusema mimi ni mtoto wake sijui nini na nini kwamba mimi nafanya starehe sihusiki na yeye sio kauli nzuri kiukweli, ina maana ananijua kwamba mimi ni mwanae baada ya kuwa DIAMOND”

Kwenye line nyingine Diamond amesema “siku zote kama alijua mimi ni mtoto wake basi angenisomesha na kunipa elimu nzuri lakini siku zote nilihangaika na Mama yangu mzazi akanikuza na kunisomesha kwa shida na tabu zote mpaka leo nimekua hivi, nisingependa kumsikia mtu yeyote anaongea kwamba mimi ni mtoto wake au yeye ni nani kwa sababu siku zote hawakuonekana, wasitake kuonekana kipindi cha Maslahi mtu ndio anajifanya anahusika sana na mimi kama mtoto wake”

“Haya mambo nilianza kuyasema toka natoa single ya binaadam sikujua hata kama leo ningekuja kuwa na Prado, makazi au kuwa na haya mafanikio mengine, baba yangu ataendelea kuwa baba yangu tu ila siwezi kumpa kipaumbele kama ninachompa mama yangu kwa sababu kama angetaka hilo angenijali toka mapema” – DIAMOND.

Kwa kumalizia, Diamond ambae mpaka sasa ametumia zaidi ya milioni 69 kujenga Nyumba yake Tegeta Dar es salaam amesema “mimi nilikua napenda kusoma na nilikua nafanya vizuri kwenye masomo yangu lakini sikua na uwezo wa kifedha kuendelea kusoma, mzazi wangu alikua na pesa ina maana angenijua mimi angenisomesha leo ningekuja kuwa hata mbunge au hata waziri kwa sababu mi najua nina upeo mkubwa sana wa kielimu na vitu vingine, sasa nimesota na muziki alafu leo ndio wanajitokeza, SITAKI WANIACHE NA MAMA YANGU MZAZI”

Mnyika Kuwa Shahidi Kesi Ya Mauaji

Leave a comment


MBUNGE wa jimbo la Ubungo, John Mnyika atakuwa ni mmoja wa mashahidi wa Serikali watakaoithibitishia mahakama namna walivyohusika washtakiwa wanaotuhumiwa kumuua Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata ya Ndago, Yohana Mpinga (30).

Jeshi la Polisi mkoani Singida, limemefikia azimio hilo baada ya kumhoji Mnyika kwa saa tatu juzi usiku, kuhusiana na tukio hilo la mauaji lililotokea baada ya mkutano wake wa hadhara uliofanyika Julai 14 mwaka huu, majira ya jioni.

Mahojiano hayo yaliyoanza saa 11.53 jioni na kumalizika saa 3:15 usiku, yaliendeshwa chini ya kikosi maalum cha askari wa upelelezi kutoka jijini Dar es Salaam kwenye ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani hapa.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilithibitisha kwamba Jeshi la Polisi lilimtaka Mnyika awe tayari kuitwa wakati wowote ili kusaidia kwenye kesi hiyo ya mauaji.

Tayari watu 18 wametiwa mbaroni, miongoni wakiwemo wanachama wa Chadema, kwa tuhuma za kuhusika kwenye mauaji ya kijana huyo wa CCM.

Mnyika alihojiwa huku akiwa na wakili wa Chadema na mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Mauaji hayo ya mwenyekiti wa UVCCM yalifanyika Julai 14 mwaka huu saa 10 jioni huko katika kijiji cha Nguvumali kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi.

Mauaji hayo yanadaiwa kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na vurugu zilizotokea kwenye mkutano wa hadhara ambao Mnyika alikuwa mgeni rasmi.

Katika hatua nyingine, mshauri na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Kitila Mkumbo, ambaye alikuwa ameambatana na Mnyika, alitarajiwa pia kuhojiwa kuhusiana na mauaji hayo jana.
Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz

Ajali ya Boti yamletea Kasheshe Spika Makinda

Leave a comment


AJALI ya kuzama kwa Boti mali ya kampuni ya Seagull July 18, 2012 ilizua hali ya kwanini ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kukataa hoja ya kutaka kujadili suala la ajali hadi pale taarifa kamili zitakapotolewa hivyo mjadala wa Bajeti ya Wizara ya mambo ya Ndani uendelee.

Kutokana na ajali hiyo, muda mfupi baada ya kipindi cha jioni kuanza, Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed alisimama na kuomba mwongozo kwa kutumia Kanuni ya 47(3) kulitaka Bunge lipitishe Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mafungu bila ya kutolewa ufafanuzi ili wabunge waweze kupata muda wa kujadili tukio hilo.

Hata hivyo, Spika Anne Makinda alipinga hoja ya Hamad na kutaka Bunge liendelee akieleza kwamba kanuni hiyo imekuwa ikitumiwa vibaya na kwamba tayari ameshawasiliana na waziri husika na kwamba taarifa kamili zitakapopatikana angelitaarifu Bunge.

Baada ya kauli hiyo Spika Makinda aliruhusu shughuli za Bunge ziendelee na kumwita Silima kutoa ufafanuzi wa hoja za wabunge.

Lakini wakati Naibu Waziri huyo akielekea kutoa hotuba yake, wabunge wote wa CUF, Chadema na baadhi wa CCM walitoka nje na kwenda katika Ukumbi wa Msekwa ili kupeana taarifa za ajali hiyo na kupanga mikakati ya jinsi ya kutuma ujumbe wa haraka kwenda Zanzibar kushirikiana na waokoaji.
Ukumbi huo uligeuka kuwa wa maombolezo kwa muda baada ya wabunge wengi kuangua vilio pale walipopewa taarifa rasmi za ajali hiyo.

Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid alieleza kwa ufupi tukio lilivyo na kwamba wangemwomba Waziri Mkuu, Mizengo Pinda awasaidie ndege ya Serikali ili waweze kwenda Zanzibar kujumuika na wenzao katika tukio hilo.

Baada ya Hamad kumaliza alisimama Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia ambaye alijaribu kuwatuliza wabunge akisema kuwa, meli inaweza kuzama lakini watu wasipoteze maisha kutokana na kuchukua muda, kauli ambayo ilipingwa na wabunge wengi.
Mbunge wa Mji Mkongwe (CUF), Ibrahim Sanya alimshutumu Spika Makinda akisema, amekosa hisia na hajui kwamba kuzama kwa meli ni janga la kitaifa.
“Kwa hili hata nikikutana na Spika nitamwambia kweli ameniudhi. Sihitaji ubunge kama hali yenyewe ndiyo hii na tutapiga kura ya kutokuwa na imani na Spika,” alisema Sanya.

Wakati hayo yakitokea, katika Viwanja vya Bunge baadhi ya wabunge na mawaziri walionekana wakiwa katika vikundi wakijadili suala hilo, huku wengine wakipinga uamuzi huo wa Spika.

Wakati hayo yakiendelea katika Ukumbi wa Msekwa, Bunge lilikuwa likiendelea kumsikiliza Silima akijibu hoja za wabunge na baada ya kumaliza, Spika Makinda alimwita mtoa hoja, Waziri Nchimbi naye kujibu.
Lakini badala yake, alitumia fursa yake kuondoa hoja ya Makadirio ya Matumizi ya wizara yake ili kutoa fursa kwa Bunge kujadili ushiriki wake katika tukio la kuzama kwa boti hiyo.

Dk Nchimbi alitumia Kanuni ya 58 (5) ambayo inamtaka mtoa hoja kusimama na kutoa hoja ya kuondoa mezani hoja yake kama kuna jambo la dharura.

“Mheshimiwa Spika, natumia Kanuni ya 58 (5) ambayo inamtaka Waziri kusimama na kutoa hoja ya kuondoa mezani hoja yake kama kuna jambo la dharura,” alisema Dk Nchimbi.

Dk Nchimbi aliendelea: “Ikumbukwe Mheshimiwa Spika, muda mfupi kabla ya kuingia hapa ndani uliniita mimi na Naibu Waziri ukataka tukueleze hali ya ajali hiyo na kwa wakati huo Kamishna wa Matukio Zanzibar alikuwa eneo la tukio. Sasa basi, kutokana na agizo lako, ni imani yangu kwa muda aliotumia Naibu Waziri unatosha kuendelea kufuatilia jambo hilo.”

Baada ya kutoa maelezo hayo, Wabunge wote 49 waliokuwa wamebaki katika ukumbi walisimama kuunga mkono hoja.

Baada ya hapo, Spika Makinda aliwahoji na kwa kauli moja waliridhia kuahirishwa kwa kikao hicho wakati huo ikiwa saa 11:31 hadi leo saa 3.00 asubuhi, huku akiitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Uongozi ya Bunge jana hiyohiyo kujadili suala hilo.

Akizungumza baada ya kikao hicho cha Kamati ya Uongozi, Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel alisema, limeamua kufuta kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu na kwamba kikao cha Bunge kitaendelea leo asubuhi kuanzia saa 2:00 kupokea taarifa ya Serikali kisha watajadili mustakabali wa vikao vya Bunge.Kamati hiyo pia iliamua kutuma ujumbe wa wabunge kwenda Zanzibar kuwafarijiwa wale wote walioathiriwa na ajali hiyo.

Imeandikwa na Salma Said, Zanzibar, Neville Meena, Habel Chidawali na Boniface Meena, Dodoma; Raymond Kaminyoge, Aidan Mhando, Dar es Salaam. SOURCE: Mwananchi.co.tz

Wasio tambulika ajali ya Boti ya Skagit waanza kuzikwa na serikali

Leave a comment


Baadhi ya Maiti zilizookolewa kutoka katika Meli iliozama na kukosa watu wake zikipelekwa kuzikwa na Serikali katika Eneo la Kama lililotayarishwa makusudi kwa ajili hio.

source:father kidevu

WATANZANIA UJERUMANI WATOA POLE

Leave a comment


UMOJA WA WATANZANIA  UJERUMANI (UTU)

UNATOA MKONO WA POLE NA RAMBI RAMBI KWA NDUGU NA JAMAA WALIOPATWA NA MAAFA KUTOKANA NA AJALI YA MELI  MV SKAGIT ILIYOTOKEA ENEO LA CHUMBE  ZANZIBAR SIKU YA TAREHE 18.07.2012.

UMOJA WA WATANZANIA NCHINI UJERUMANI UMEPOKEA KWA MASIKITIKO MAKUBWA TAARIFA ZA AJALI MBAYA AMBAYO IMESABABISHA VIFO.
UMOJA WA WATANZANIA UNAUNGANA NA WATANZANIA WOTE NCHINI KATIKA

 KIPINDI HICHI CHA  MAOMBOLEZO.
MUNGU IBARIKI TANZANIA

MUNGU UBALIKI UMOJA WA KITAIFA

MFUNDO PETER MFUNDO
MWENYEKITI WA
UMOJA WA WATANZANIA UJERUMANI (UTU)
Email: kamati.utu@googlemail.com

TAARIFA YA SMZ KUHUSU AJALI YA MELI YA MV. SKAGIT ILIYOTOLEWA USIKU WA JULAI 19,2012

Leave a comment


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetoa taarifa usiku huu ikieleza idadi ya watu waliopatikana wakiwa hai ni 146 na kupata maiti 62.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari usiku leo,Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamuhuna alisema taarifa hiyo ndio sahihi na kuwataka wananchi kutoamini taarifa zinazotolewa na watu wengine zaidi ya Serikali.

Waziri Shamuhuna alisema kwamba maiti 62 walipatikana ambao kati ya maiti hizo watoto ni 9 na kuna raia mmoja wa kike wa kigeni ambaye hakuweza kutambulika Uraia wake,lakini umeonekana picha yake moja ndogo ya hati ya kusafiria.

Waziri Shamuhuna alisema meli hiyo ilibeba jumla ya abiria 290 kati ya hao watu wazima 250, watoto wadogo 31 na mabaharia 9.

Waziri huyo aliwataka wananchi katika sehemu mbalimbali hasa katika vijiji vilivyo kandokando ya bahari watakapoona maiti au mtu akiwa hai ambaye wanadhani ni wa ajali ya Meli yaSkagit.

Aidha, Waziri Shamuhuna alisema kwamba kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ambao watakuwa na wasiwasi wa kutowaona ndugu na jamaa zao amewataka kufika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili ya kupata taarifa zaidi au kuripoti habari za kupotelewa kwa ndugu au jamaa zao.

Kwa upande waZanzibar, Waziri huyo aliwataka wananchi kufika kwa Masheha wao kutoa taarifakamahizo.

Serikali imewashukuru makampuni binafsi za usafiri baharini kwa msaada wao na wasisite kutoa msaada katika kazi inayoendelea ya kutafuta watu au maiti wengine katika eneo la tukio.

Meli ya Mv. Skagit ilizama Julai 18,2012 karibu na Kisiwa cha Chumbe umbali wa maili sita kuelekea Kusini mwa Kisiwa kidogo cha Yasin Zanzibar ikitokea Bandari yaDar es Salaamilikoanza safari saa 5:30 asubuhi.

Meli hiyo inamilikiwa na Kampuni ya Sea Guall Sea Transport Ltd, Kampuni ambayo Meli yake nyengine ya Mv. Fatih ilizama ikiwa Bandarini Malindi Zanzibar na kufariki watu sita mwaka 2009.

Mwisho.

IMETOLEWA NA:

IDARA YA HABARI(MAELEZO)ZANZIBAR

ZANZIBAR,TANZANIA

JULAI 19,2012

TAARIFA MPYA KUHUSU AJALI YA MV SKAGIT ZANZIBAR, IDADI YA VIFO IMEONGEZEKA.

Leave a comment


Kwa mujibu wa TBC1 katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku leo July 19 2012, mpaka sasa idadi ya waliopoteza maisha kwenye ajali ya MV SKAGIT ni 68 ambapo baadhi ya maiti tayari zimetambuliwa na tayari majeruhi zaidi ya 100 walikua wamefikishwa hospitali huku watu ambao hawajaonekana wakiwa ni 91.
Mpaka jana usiku kwenye taarifa ya habari saa mbili usiku, ni watu saba pekee walioripotiwa kupoteza maisha kwenye ajali hiyo.
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano na Serikali ya Zanzibar zimetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia July 19 2012 ambapo kituo cha mawasiliano kwa ndugu wanaohitaji kujua habari za ndugu zao waliopata ajali kwa upande wa bara ni ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es salaam.
Kutoka bungeni ni kwamba wabunge wamekubaliana posho za leo (July19) hawatazipokea na badala yake zitapelekwa kama rambirambi kwenye ajali.
Spika wa bunge Anne Makinda ambae aliahirisha kikao cha bunge leo mpaka kesho amesema “tulikua tunaamini kwamba kutakua na mazishi ya halaiki lakini Serikali ya Mapinduzi imesema hapana mpaka sasa”
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini SUMATRA imesema cheti cha ubora cha meli hiyo kilianza tarehe 24 August 2011 na muda wake unaisha tarehe 23 2012 ambapo imefahamika kwamba meli hiyo ilisajiliwa na Mamlaka ya usafiri wa baharini Zanzibar (ZMA) na ilikua imepitishwa kubeba abiria 300 na mizigo isiyozidi tani 26 ambapo Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu na Bunge William Lukuvi amesema meli ilikua imebeba watu 290, watu wazima ni 250, watoto ni 31 na wafanyakazi 9 wa meli.

Maafa Ya Kuzama Kwa Meli, Watu 30 wa Fariki dunia mpaka Asubuhii!!

Leave a comment


Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia Julai 19 hadi Julai 21 kufuatia maafa ya ajali ya Meli ya Mv. Skagit iliyozama karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein akitangaza maombolezo hayo, alisema bendera zote zitapepea nusu mlingoti na kwamba shughuli za sherehe na burudani zimefutwa kwa muda wa siku tatu za maombolezo.

Dk. Shein alisema shughuli za Serikali zitaendelea kama kawaida. Katika taarifa yake aliyoitoa Ikulu usiku wa kuamkia Julai 19, Rais Dk Shein amewahakikishia wananchi na hasa waliopoteza jamaa zao kuwa Serikali itabeba gharama zote za mazishi na pia kugharamia huduma za matibabu kwa majeruhi.

“Nimesikitishwa sana na msiba huu, Katika wakati huu si vema tukaanza kulaumiana jambo la muhimu hivi sasa ni kuokoa maisha ya watu” Alisema Rais Dk. Shein.

Mbali ya taarifa hiyo, Rais Dk Shein aliungana na wananchi, viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, Viongozi wa dini katika kutambua maiti zilizofikishwa katika eneo maalum la viwanja vya Maisara Suleiman.

Mbali ya kwenda katika viwanja hivyo, pia alifika katika eneo la bandari ya Zanzibar kufuatilia taarifa za tukio hilo. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana lilisitisha shughuli zake kufuatia maafa hayo ambapo wakati wa jioni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Nchimbi alitarajiwa kufanya majumuisho ya bajeti yake.

Baadhi ya Wabunge wakiongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Jeshi la Polisi walitembelea majeruhi katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja pamoja na eneo la viwanja vya Maisara ambapo maiti hufikishwa kwa ajili ya utambuzi.

Mbali ya Bunge, pia Baraza la Wawakilishi Zanzibar jana lilisitisha kwa muda shughuli zake ili kutoa nafasi kwa Wawakilishi hao wa wananchi kushiriki katika shughuli za uokozi ambapo wengi walifika bandarini kusaidia kazi mbalimbali ikiwemo kuwafariji waliopoteza ndugu zao.

Taarifa kutoka Mamlaka za Serikali zinaeleza kwamba hadi asubuhi hii maiti 30 zilipatikana ambapo 20 kati ya hizo zimetambuliwa na kuchukuwa na jamaa zao huku wananchi wengine wakiendelea na kuzitambua maiti zinazofikishwa katika eneo la Maisara.

Aidha, katika taarifa hiyo, watu 145 wameokolewa wakiwa hai, wengi wao wapo katika hali nzuri wameruhusiwa kuungana na familia zao baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar.

Meli ya Mv. Skagit ilizama Julai 18,2012 saa 7:50 mchana ikitokea Bandari ya Dar es Salaam kwenda Zanzibar ikiwa imebeba abiria 250 watu wazima, watoto 31 na mabaharia 6.

Kazi ya utafutaji na uokoaji zinaendelea asubuhi hii katika eneo la tukio ilikozama meli hiyo umbali wa maili sita Kusini mwa Kisiwa cha Yasin karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.

PICHA ZA MATUKIO YA UOKOAJI WA ABIRIA WALIOZAMA KWENYE MELI YA MV STAR GATE.

Leave a comment


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akiwa katika Eneo la Bandari akishuhudia kuletwa kwa majeruhi mbalimbali waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Amer Kificho pamoja na mawaziri mbalimbali wakiwa katika Eneo la Bandari wakishuhudia kuletwa kwa majeruhi mbalimbali waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.

Majeruhi alieokolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.

Majeruhi wakipatiwa Mablangeti kwa ajili ya kujihifadhi baada ya kuokolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.

Raia wa kigeni waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.

Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Hamad Masoud Hamad akiwa katika hali ya huzuni Baada ya kushiriki katika uokoaji na kuwaona Majeruhi waliookolewa katika Meli iliozama ya Star Gate wakiteremka Bandarini Zanzibar.

Wananchi wakiwa wamekusanyika eneo la Bandari mjini Zanzibar kuona ndugu zao waliookolewa wakiwa hai na waliofariki katika ajali hiyo.

Askari wa Vikosi mbalimbali wakiwa katika kazi ya Uokozi kwa Abiria waliokuwa katika Meli ya Star Gate ambayo iliozama katika ikiwa imebeba abiria 250 huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar.

Daktari akitoa huduma ya kwanza kwa mmoja wa majeruhi wa boti iliozama ikiktokea Dar-es-Salaam kuelekea Zanzibar.

Abiria waliookolewa kutoka katika meli iliozama ya Star Gate katika bahari ya Chumbe Zanzibar.PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR

Older Entries Newer Entries