Home

UKWELI KUHUSU JOSE CHAMELEONE WAELEZWA

Leave a commentMkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo(kati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya msanii huyo na kushoto ni Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho

Baadhi ya wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza kwa makini Eric Shigongo.

JD akisisitiza jambo (kulia) Juma Mbizo, Mratibu wa Matamasha.

Eric Shigongo (kulia) akisikiliza maswali kutoka kwa waandishi wa habari.

MD wa Global Publishers Ltd, Eric Shigongo, mapema leo ameongea na media kuhusu madai ya Jose Chameleone kudai paspoti yake, ambaye jana alikwenda Ubalozi wa Tanzania nchini kwake Uganda kushinikiza kurejeshewa paspoti yake.

Eric amefunguka kwa kusema kuwa, kampuni yake na msanii huyo waliingia makubaliano ya kufanya shoo kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini, liliofanyika Uwanja wa Taifa Julai 7 mwaka huu, ambapo katika mazungumzo ya awali, msanii huyo aliomba kulipwa dola 5000 na kulipiwa tiketi 2 za ndege ili kuhudhuria tamasha hilo, masharti ambayo yalikubaliwa.

Mazungumzo hayo ya awali yalifanyika kati ya Global Publishers na agenti wa Chameleone ajuliikanae kwa jina la George. Kabla ya kutuma fedha hizo, kampuni yake ilihitaji kujiridhisha kama ajenti huyo alikuwa kweli anawasilina na kukubaliana na Chameleone kuhusu shoo ya Dar, ili kuepuka utapeli.

“Tulipokubaliana nae kupitia ajenti wake, tuliamua kwenda mbele zaidi ili kujiridhisha, ambapo tuliwasiliana na mwanamuziki Kidumu ambaye anamfahamu huyo George na kwenda mpaka Kampala kukutana ana kwa ana na wahusika, kwa niaba yetu”, alisema Shigongo.

Akielezea zaidi, Shigongo alisema kuwa Kidumu alikwenda Kampala na kukutana na George pamoja na Jose Chameleone, ambaye alikubali kuja kufanya shoo na kumruhusu Kidumu kusainishana mkataba na ajenti wake na kumpatia hizo fedha.

“Chameleone alitoa ruhusa kwa ajenti wake kusaini mkataba na kupokea advace ya dola 3,500 kwa niaba yake kwa madai kuwa yeye asingeweza kusubiri malipo wakati huo kwa sababu alikuwa anawahi sehemu nyingine.

“Baadae Jose alikuja kugeuka na kudai hakupewa hizo pesa na ajenti wake, kitu ambacho kilonekana kama mchezo wa kitapeli kati ya Chameleone na ajenti wake kwetu sisi.

“Kwa kuwa ujio wake Tanzania ulikuwa umeshatangazwa sana, uongozi wa Global Publishers, ulilazimika kufanya mazungumzo mengine na Chameleone na kumuomba sana kuja nchini kufanya shoo, ambapo this time akakubali kwa masharti ya kulipwa dola 8000 na tiketi nne za ndege.

“Ndugu zangu, sikua na jinsi, nililazimika kumkubalia na kumlipa dola 8000, kwa sababu tayari tamasha lilikuwa limeshatangazwa sana, billboards zimewekwa barabarani na promosheni kubwa ilikuwa inafanyika,” alisema Shigongo kwa uchungu.

Hivyo mara baada ya kukubaliana, safari hii akalazimika kumtuma meneja wake kwenda mpaka Kampala na kukutana na Chameleone ana kwa ana na kumpatia dola 8000 na kusaini mkataba mwingine wa pili.

“Ni dhahairi kabisa alichokifanya Chameleone kilikuwa ni utapeli kwa kushirikiana na ajenti wake, kwa sababu tunamuamini Kidumu ambaye tumeshafanya naye kazi mara Kadhaa kwa uaminifu mkubwa. Pia ni Chameleone ndiye aliyemuidhinisha ajenti wake kuchukua pesa hizo, hivyo ulikuwa ni mchezo wa pamoja,  na hiyo ni tabia ya Chameleone, kwani ameshawafanyia mapromota wengi kiasi kwamba hivi sasa hakanyagi nchini Kenya.

“Dola 3,500 siyo fedha nyingi, ningeweza kuzisamehe, lakini nimeamua kuzidai kwa manufaa ya watu wengine, Watanzania tusikubali kufanywa wajinga kwa sababu ya upole wetu, tutaendelea kudhauriwa na kufanywa wajinga mpaka lini,” alihoji Shigongo.

Mwisho Shigongo alitoa wito kwa Watanzania kuungana katika suala hili, kwani Chameleone ameonesha dharau kubwa kwa Watanzania kwa kumfuata balozi wetu nchini Uganda na kuondoka ofisi kwake huku akisonya na kubamiza mlango, akiendelea kuonesha dharau kwa Watanzania wote wapatao miloni 40!

 

 

PICHA: ISSA MNALLY/ GPL

source:globalpublishers

TAARIFA MPYA KUHUSU AJALI YA MV SKAGIT ZANZIBAR, IDADI YA VIFO IMEONGEZEKA.

Leave a comment


Kwa mujibu wa TBC1 katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku leo July 19 2012, mpaka sasa idadi ya waliopoteza maisha kwenye ajali ya MV SKAGIT ni 68 ambapo baadhi ya maiti tayari zimetambuliwa na tayari majeruhi zaidi ya 100 walikua wamefikishwa hospitali huku watu ambao hawajaonekana wakiwa ni 91.
Mpaka jana usiku kwenye taarifa ya habari saa mbili usiku, ni watu saba pekee walioripotiwa kupoteza maisha kwenye ajali hiyo.
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano na Serikali ya Zanzibar zimetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia July 19 2012 ambapo kituo cha mawasiliano kwa ndugu wanaohitaji kujua habari za ndugu zao waliopata ajali kwa upande wa bara ni ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es salaam.
Kutoka bungeni ni kwamba wabunge wamekubaliana posho za leo (July19) hawatazipokea na badala yake zitapelekwa kama rambirambi kwenye ajali.
Spika wa bunge Anne Makinda ambae aliahirisha kikao cha bunge leo mpaka kesho amesema “tulikua tunaamini kwamba kutakua na mazishi ya halaiki lakini Serikali ya Mapinduzi imesema hapana mpaka sasa”
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini SUMATRA imesema cheti cha ubora cha meli hiyo kilianza tarehe 24 August 2011 na muda wake unaisha tarehe 23 2012 ambapo imefahamika kwamba meli hiyo ilisajiliwa na Mamlaka ya usafiri wa baharini Zanzibar (ZMA) na ilikua imepitishwa kubeba abiria 300 na mizigo isiyozidi tani 26 ambapo Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu na Bunge William Lukuvi amesema meli ilikua imebeba watu 290, watu wazima ni 250, watoto ni 31 na wafanyakazi 9 wa meli.

Campmulla waomba kura kwenye Artist Of The Week ya MTV

Leave a comment


Kila wiki kituo cha MTV huwa na segment ya msanii bora wa wiki ambaye hupigiwa kura na watamazamaji.
Mpango huo uliowekwa na kituo hicho kwaajili ya kupromote wasanii wapya unaitwa MTV Iggy.
Kundi litakalopata kura nyingi zaidi litapewa shavu kwenye mtandao wa MTVIggy.com wiki hii pamoja na interview ndefu ( tell-all interview)
Wiki hii kundi la hip hop la nchini Kenya, Campmulla ni miongoni mwa wasanii/kundi lilitojwa kupigiwa kura.
Wasanii wengine ni pamoja na Leo Justi kutoka Brazil, Mario & Vidis wa Lithuania, Young Empires wa Canada na Fallulah wa Denmark.
Mpaka sasa Campmulla wanaongoza kwenye kura hizo.

Hawa ndio mastaa wa Hollywood wanaolipwa hela nyingi chini ya umri wa Miaka 30

Leave a comment


#1. Taylor Swift , 22
May 2011 to May 2012 Earnings: $57 million

#2. Justin Bieber, 18
May 2011 to May 2012 Earnings: $55 million

#3. Rihanna, 24
May 2011 to May 2012 Earnings: $53 million

#4. Lady Gaga, 26
May 2011 to May 2012 Earnings: $52 million

#5. Katy Perry, 27
May 2011 to May 2012 Earnings: $45 million

#6. Adele, 24
May 2011 to May 2012 Earnings: $35 million

#7. Kristen Stewart, 22
May 2011 to May 2012 Earnings: $34.5 million

#8. Lil Wayne, 29
May 2011 to May 2012 Earnings: $27 million

#9 = Taylor Lautner, 20
May 2011 to May 2012 Earnings: $26.5 million

#9 = Robert Pattinson, 26
May 2011 to May 2012 Earnings: $26.5 million

Enrique Iglesias & Jennifer Lopez Tour – Started on July 14th

1 Comment


Wasanii waige mfano wa website ya Diamond

Leave a comment


Katika jambo ambalo wabongo wanasema Diamond kapiga bao ni kuanzisha website yake mwenyewe. Website hiyo iitwayo Thisisdiomond.com imegeuka maarufu kwa mashabiki wake wanaotaka kujua yale ayafanyayo na waandishi wa habari wanaotaka kupata habari zake.
Tofauti na website za wasanii wengine nchini, yake Diamond tunathubutu kusema ndio personal website pekee inayoongoza kwa kuwa updated kila siku kwa matukio mapya. Diamond si mwandishi wa habari lakini anajua kuwa yeye ni mtengeneza habari (newsmaker). Katika uandishi wa habari yeye yupo kwenye ule ubora wa habari (news values) ambao kitaaluma unajulikana kama ‘Prominence’.
Yeye ni mtu maarufu kwahiyo chochote anachokisema ama kukiandika sehemu ni habari kwakuwa ni mtu maarufu. Hivyo ana mengi anayoyaandika kwenye website yake yanayotokana na kile akifanyacho kila siku, bila kusahau picha nzuri na nyingi ambazo huziweka mara kwa mara awapo kwenye ziara zake.
Hakuna show anayoenda na asichukue picha za kuja kuwaonesha mashabiki wake. Hakosi la kuandika kuwajuza mashabiki.
Kwanini tunasema wasanii wengine waige mfano wa website yake? Kwanza wasanii wachache ambao wana website ama blog zao wakumbuke kigezo hicho kuhusu ubora wa habari kuwa wao ni ‘newsworthy’ yaani wanatengeneza habari kwa mengi wanayosema ama kufanya.
Ni jambo la ajabu website ya msanii mkubwa inakuwa updated mara moja kwa mwezi tena kwa habari ya ajabu ajabu tu na wakati mwingine haimhusu yeye mwenyewe! Personal websites/blogs zinapaswa kutoa kwa asilimia kubwa habari kuhusu msanii mwenyewe.

Wasanii wengine wamezigeuza personal blogs zao kama blogs zingine za kawaida zinazotoa habari za watu wengine. Diamond anapaswa kusifiwa kwasababu website yake inamuangaza yeye zaidi. Wapi ameenda kufanya show, amekutana na nani, ana mipango gani n.k.
Ukiwa mtembeleaji mzuri wa website yake utayafahamu hayo. Iweje website binafsi ya msanii mkubwa nchini ijae mambo ya watu wengine tu wakati yeye mwenyewe kila siku kuna mambo anayoyafanya na ambayo kama angeyaandika kwa kuambatanisha na picha mashabiki wake wangefurahia!!
Hivyo wasanii wanaomiliki website/blog binafsi watambue kuwa sio fashion kuwa na website ambayo hubadilishwa habari mara moja ama mbili kwa mwezi. Huna haja ya kuwa na website binafsi wakati huna la kuandika. Inabaki kuwepo tu bila kitu chenye kumrudisha tena msomaji.
Kwa wale ambao hawana website/blog zao ni muda mzuri wa kufikiria kuwa nazo. Ni njia nzuri ya kujitangaza. Waandishi wa habari huzitumia kupata habari halisi na zenye ushahidi kutoka kwa msanii husika. Kumiliki tu akaunti ya Facebook na Twitter hakutoshi.

source:bongo5

The Game kuja na reality show yake

Leave a comment


Rapper The Game amepitia mengi ya hatari kama kupigana mtaani, kufungwa jela, kupigwa risasi na sasa yote hayo yanaweza kuonekana kwenye reality show yake itakayoonesha hadi pale atakapomuoa mpenzi wake wa siku nyingi Tiffany Cambridge.
Reality show hiyo inayotayarishwa na kampuni ya 51 Minds Entertainment itaonesha upande mwingine mpya wa rapper huyo.
Mtandao wa TMZ umesema kuwa katika show hiyo Game ataonekana jinsi anavyoijali familia yake na masuala mengine yahusuyo mipango ya ndoa..
Utayarishaji wa show hiyo ulianza mapema mwezi huu na tayari mazungumzo ya kuirusha show hiyo kwenye vituo vya runinga vya MTV na VH1 yameshafanyika.

Older Entries

%d bloggers like this: