Home

Maafa Ya Kuzama Kwa Meli, Watu 30 wa Fariki dunia mpaka Asubuhii!!

Leave a comment


Na Juma Mohammed,MAELEZO Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia Julai 19 hadi Julai 21 kufuatia maafa ya ajali ya Meli ya Mv. Skagit iliyozama karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk. Ali Mohammed Shein akitangaza maombolezo hayo, alisema bendera zote zitapepea nusu mlingoti na kwamba shughuli za sherehe na burudani zimefutwa kwa muda wa siku tatu za maombolezo.

Dk. Shein alisema shughuli za Serikali zitaendelea kama kawaida. Katika taarifa yake aliyoitoa Ikulu usiku wa kuamkia Julai 19, Rais Dk Shein amewahakikishia wananchi na hasa waliopoteza jamaa zao kuwa Serikali itabeba gharama zote za mazishi na pia kugharamia huduma za matibabu kwa majeruhi.

“Nimesikitishwa sana na msiba huu, Katika wakati huu si vema tukaanza kulaumiana jambo la muhimu hivi sasa ni kuokoa maisha ya watu” Alisema Rais Dk. Shein.

Mbali ya taarifa hiyo, Rais Dk Shein aliungana na wananchi, viongozi wa Serikali, vyama vya siasa, Viongozi wa dini katika kutambua maiti zilizofikishwa katika eneo maalum la viwanja vya Maisara Suleiman.

Mbali ya kwenda katika viwanja hivyo, pia alifika katika eneo la bandari ya Zanzibar kufuatilia taarifa za tukio hilo. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jana lilisitisha shughuli zake kufuatia maafa hayo ambapo wakati wa jioni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Nchimbi alitarajiwa kufanya majumuisho ya bajeti yake.

Baadhi ya Wabunge wakiongozwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Shamsi Vuai Nahodha, Mkuu wa Jeshi la Polisi walitembelea majeruhi katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja pamoja na eneo la viwanja vya Maisara ambapo maiti hufikishwa kwa ajili ya utambuzi.

Mbali ya Bunge, pia Baraza la Wawakilishi Zanzibar jana lilisitisha kwa muda shughuli zake ili kutoa nafasi kwa Wawakilishi hao wa wananchi kushiriki katika shughuli za uokozi ambapo wengi walifika bandarini kusaidia kazi mbalimbali ikiwemo kuwafariji waliopoteza ndugu zao.

Taarifa kutoka Mamlaka za Serikali zinaeleza kwamba hadi asubuhi hii maiti 30 zilipatikana ambapo 20 kati ya hizo zimetambuliwa na kuchukuwa na jamaa zao huku wananchi wengine wakiendelea na kuzitambua maiti zinazofikishwa katika eneo la Maisara.

Aidha, katika taarifa hiyo, watu 145 wameokolewa wakiwa hai, wengi wao wapo katika hali nzuri wameruhusiwa kuungana na familia zao baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar.

Meli ya Mv. Skagit ilizama Julai 18,2012 saa 7:50 mchana ikitokea Bandari ya Dar es Salaam kwenda Zanzibar ikiwa imebeba abiria 250 watu wazima, watoto 31 na mabaharia 6.

Kazi ya utafutaji na uokoaji zinaendelea asubuhi hii katika eneo la tukio ilikozama meli hiyo umbali wa maili sita Kusini mwa Kisiwa cha Yasin karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.

PICHA ZA MATUKIO YA UOKOAJI WA ABIRIA WALIOZAMA KWENYE MELI YA MV STAR GATE.

Leave a comment


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi akiwa katika Eneo la Bandari akishuhudia kuletwa kwa majeruhi mbalimbali waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.

Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Amer Kificho pamoja na mawaziri mbalimbali wakiwa katika Eneo la Bandari wakishuhudia kuletwa kwa majeruhi mbalimbali waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.

Majeruhi alieokolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.

Majeruhi wakipatiwa Mablangeti kwa ajili ya kujihifadhi baada ya kuokolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.

Raia wa kigeni waliookolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.

Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Hamad Masoud Hamad akiwa katika hali ya huzuni Baada ya kushiriki katika uokoaji na kuwaona Majeruhi waliookolewa katika Meli iliozama ya Star Gate wakiteremka Bandarini Zanzibar.

Wananchi wakiwa wamekusanyika eneo la Bandari mjini Zanzibar kuona ndugu zao waliookolewa wakiwa hai na waliofariki katika ajali hiyo.

Askari wa Vikosi mbalimbali wakiwa katika kazi ya Uokozi kwa Abiria waliokuwa katika Meli ya Star Gate ambayo iliozama katika ikiwa imebeba abiria 250 huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar.

Daktari akitoa huduma ya kwanza kwa mmoja wa majeruhi wa boti iliozama ikiktokea Dar-es-Salaam kuelekea Zanzibar.

Abiria waliookolewa kutoka katika meli iliozama ya Star Gate katika bahari ya Chumbe Zanzibar.PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR

MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA CCM (UVCCM) AUAWA SINGIDA.

Leave a comment


Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,Linus Vicent Sinzumwa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya mauaji yaliyofanywa na wafuasi wa CHADEMA. (Picha na Nathaniel Limu).

Jeshi la polisi mkoa wa Singida, linawashikilia wakazi 18 wa kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi,kwa tuhuma ya kumuua mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM (UVCCM),Yohana Mpinga (30) baada ya kumpiga kwa kutumia silaha za jadi.

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Singida, Linus Vicent Sinzumwa alisema tukio hilo la kusikitisha limetokea julai 14 mwaka huu saa kumi alasiri huko katika kijiji cha Ndago.

Alisema siku ya tukio,Chama Cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) kilikuwa na kibali halali cha kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji hicho cha Ndago na mgeni rasmi katika mkutano huo,alikuwa mbunge wa jimbo la Ubungo jijini Dar-es-salaam.

Sinzumwa alisema mara baada ya CHADEMA kuanza mkutano huo,viongozi wake walianza kuporomosha mvua ya kashifa mbalimbali dhidi ya mbunge wa jimbo hilo Mwingullu Nchemba, kitendo ambacho kiliudhi baadha ya watu waliokuwa wamehudhuria mkutano huo.

“Wananchi hao ambao walichukizwa na kitendo cha kukashifiwa mbunge wao,walianza kupiga kelele kuwa hawataki mbunge wao akashifiwe na badala yake wanataka kusikia sera za CHADEMA tu na si vinginevyo.Hata hivyo,viongozi hao waliendelea tu kuporomosha kashifa dhidi ya Mwingullu na kusababisha kuanza kwa vurugu”,alisema.

Kamanda huyo alisema kuwa vurugu hizo zilihusisha kundi la wanachama wa CHADEMA na wa CCM na zilisambaa.Wanachama hao walianza kurusha mawe ovyo na askari wachache wa polisi waliokuwepo,walizidiwa nguvu na makundi hayo.

“Huyu mwenyekiti wa vijana CCM Yohana,yeye akikimbilia kwenye nyumba ya mwalimu Shume Manase Mpinga ili kuokoa maisha yake,lakini kundi la wananchama wa CHADEMA wakiwa wamebeba fimbo na mawe,walimpiga sehemu mbalimbali za mwili wake na kusbabisha kifo chake papo hapo”,alisema kamanda Sinzumwa kwa masikitiko makubwa.

source:dewjiblog.

Mtanzania aliyepotea Norway; Polisi wanaomba msaada

Leave a comment


Tromøy, Arendal (Norway).
Mwanamke mwenye asili ya Tanzania anatafutwa, ametoweka nyumbani baada ya kudai kudundwa na mmewe tangu Jumatatu .

Huyu ndiye dada wa Kitanzania aliyepotea toka Jumatatu hajaonekana mpaka leo. Bado anatafutwa! Polisi wanaomba msaada wa wananchi kwa yeyote anayefahamu lolote kuhusu huyu dada.
Mbwa wa polisi wakisaidia kwenye msako wa kumtafuta mwanamke mwenye asili ya Tanzania aliyepotea Tromøy, Arendal. Picha na Anne Karin Andersen (Agderposten)
Jana saa moja mwanamke mmoja alipiga simu polisi na kusema kuwa amepigwa nyumbani kwake. Baada muda mfupi, akaonekana ametoka nyumbani kwake, maeneo ya Tromøy, Arendal. Ametoweka na hajaonekana tokea jana. Mwanamke huyo ana asili ya Tanzania.
Mumewe alitoa taarifa polisi baada ya kutoonekana kwa muda mrefu. Tokea jana amekuwa akitafutwa na helikopta, boti za polisi, polisi wenye mambwa, jamaa wa msalaba mwekundu na watu wa kujitolea.
Source: watanzaniaoslo

Mapenzi ndani ya Big Brother yajenga uadui ‘mkali’ kati ya Kenya na Nigeria.

Leave a comment


Jana wapenzi katika jumba la Big Brother Africa, Prezzo na Goldie wamezinguana tena baada ya Prezzo kumwambia Goldie, “you are a quitter, you are a runner, run away like you always do.” Pia alimwambia kuwa hakukuwa na haja Goldie kumwokoa na eviction.
Ugomvi huo wa Prezzo kutoka Kenya na Goldie kutoka Nigeria umenunuliwa na wananchi wa Kenya na wale wa Nigeria. Vita vya maneno na matusi vimetawala ukurasa maalumu wa Big Brother Africa wenye ‘fans’ 859,622 mpaka sasa.
Wakenya na wanaijeria wamejikuta katika vita nzito ya maneno kiasi cha kuhatarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Kenya, I don’t remember u winning BB, by the look of things u r not going to win not anytime soon… Sit ur asses down for a minute and watch the game, always insulting that’s what u knw best. Last time u were busy with SA now is Nigeria?” aliandika Nonhlanhla Sambo.
Grace Wanjiku wa Kenya aliandika, “si wakenya mwajua we are a working nation! Hawa waoga na sa hawana kazi,they eat /sleep bba!24/7 nendeni mkachape kazi.”
Mkenya mmoja aitwaye John Kisindai Kulundu aliamua kuziponda filamu za wanaijeria kwa kusema, “Only retarded villagers watch those predictable naija movies.lol.”
Kulundu hakukomea hapo, aliwaangushia wanaijeria bomu jingine, “nigerians have invaded africans cities because of insecurity and poverty in there country,we shall kick u back 2 die in your country,kaa mbali na sisi msituambukize ujinga.”
Kitendo cha wakenya kuchanganya Kiswahili kwenye comments zao zilimkera Mary Esosuota aliyesema, “Only cowards murmur so dey wont be heard…anyone bold enough shud write boldly and air their views for others to understand.”
Wanaijeria hawakukubali kushindwa, Maureen Eboh alitupa bomu kwa wakenya, “What a shame kenyans, c as dem dey wash una wif soda soap nd water, chai c poverty, not even detegent soap buh soda, una own don finish b dat oh.”
Mnaijeria mwingine Tunde Olawole aliandika, “Foolish kenyans they are all affected by meningitis which is a mentor to their mental image u will alwayz be our wast.teamnaija.”
Kama desturi ya watanzania wasiopenda makuu, mtanzania Koli Collins hakupendezwa na vita hiyo ya maneno kati ya wanaijeria na wakenya kwa kuwaambia, “Wakenya nawaomba,acheni matusi ili tusiwakwaze watu wa nchi zingine,tusije tukachimbia Prezzo kaburi kama vile watu wa Afrika kusini walivyomchimbia bibi kizee wao almaarufu barbs….sababu ya kujigamba na matusi,tusome funzo kutoka kwao, Proudly Tanzanian.”
Unadhani vita hii ya maneno kati ya wanaijeria na wakenya kutokana na Big Brother inaweza kuleta uadui kati ya nchi hizo baadaye?

source:bongo5

Wadau Kumradhi kwa picha hizi:lori laua wawili na kujeruhi vibaya wengine nane kibaoni-tegeta jijini Dar jana.

Leave a comment


Wananchi wa eneo la Tegeta Kibaoni, jijini Dar es Salaam wakisaidiani na polisi kuupakiza mwili wa mmoja wa mwananchi kwenye gari kati ya watu waliokufa katika ajali iliyotokea baada ya Lori la mchanga kupata hitilafu ya breki na kuacha barabara na kugonga Daladala kabla ya kuvamia baa na kusababisha vifo vya watu wawili papo hapo na wengine nane kujeruhiwa jana


Wananchi wa eneo la Tegeta Kibaoni, jijini Dar es Salaam wakijaribu kutoa mwili wa mmoja wa mwananchi kati ya watu waliokufa katika ajali iliyotokea baada ya Lori la mchanga kupata hitilafu ya breki na kuacha barabara na kugonga Daladala kabla ya kuvamia baa na kusababisha vifo vya watu wawili papo hapo na wengine nane kujeruhiwa jana

TCRA yawaasa Watanzania kuhamia Digitali

Leave a commentWaanzania wametakiwa kujiandaa kuhama katika mfumo wa mabadiliko ya anaelojia kwenda katika mfumo wa digital ambao hadi ifikapo Desemba 31 mwaka huu matangazo ya anaelojia yatazimwa rasmi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa Naibu Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Bw. Frederick Ntobi amesema kuwa kuanzia Januari 2013 wananchi hawataweza tena kutumia mfumo uliopo wa
sasa wa anaelojia.

Amesema kuwa ili kwenda na utandawazi uliopo hadi ifikapo januari 2013 dunia nzima itakuwa imehama katika mfumo wa kutumia anaelojia katika luninga zao hivyo ni vema wananchi wakaanza kujipanga mapema ili kuhakikisha kuwa kila mtu anafikiwa na huduma hiyo.

Amengeza kusema ku wa ili mfumo huoi ukamilike ni vema jamii ikahakikisha kuwa lazima inakuwa na kifaa kiitwacho kingamuzi ambacho ndicho kinatumika katika kubadilisha mfumo ili kuweza kufanikiwa katika ubadilishaji huo.

Bw Ntobi ametaja faidsa ya kutumia mfumo huo kuwa ni pamoja kuwa na matumizi bora ya masafa ,kupata huduma bora za ziada mfano kulipia bili ya umeme,kutuma pesa pamoja na kupata intenet pindi uwapo kwenye luininga zao.

Pia alitaja faida ingine kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa ajira kwa kuwa mfumo utachangia kuongezeka kwa makampuni nmengi ya utangazaji.

Older Entries

%d bloggers like this: