Home

GODZILLA : MASHABIKI WALITAKA NIIMBE

Leave a comment


Staa wa hip hop Bongo, Godzilla amefunguka kuwa hatua ya kutoa wimbo ukiwa kwenye staili ya kuimba imekuja kufuatia maombi kibao aliyoyapata kutoka kwa fans wake.
Akizungumza na Teentz.com muda mfupi uliopita Godzilla anayesumbia kitaa na ngoma kali inayobeba jina la ‘La Kuchumpa’ amesema kuwa ameshangazwa na hataua ya wadau wa muziki wa kizazi kipya kuhoji juu ya uamuzi wake wa kutumia staili ya kuimba kwenye wimbo wake mpya uliopewa jina la ‘nataka’.
“Unajua mimi ni mwanamuziki na katika hilo ni lazima ujuwe kuwa nina mashabiki ambao kwa lolote wako nyuma yangu , hivyo basi walinifuata na kuniambia kuwa wanataka nijaribu kutoa wimbo kwenye staili ya kuimba soo kwakuwa ninatambua umuhimu wao nikaamua kutoa nyimbo mbili moja ikiwa kwenye mtindo huo na nyingine ikiwa kwenye hip hop kama kawaida” alisema Zilla na kuongeza kuwa nimeamu a kufanya hivyo ili kuwarizisha mashabiki wangu wote.

source:.teentz

Nadia Buari akataa uvumi wa kurudiana na Michael Essien

Leave a comment


Muigizaji wa filamu wa kike nchini Ghana Nadia Buari, amekanusha taarifa za udaku kuwa ana mpango wa kurudiana na mpenzi wake wa zamani, mchezaji wa klabu ya Chelsea, Michael Essien.
Habari za kuwa wapenzi hao huenda wamerudiana zilienea kwenye internet wiki iliyopita baada ya kuonekana kwa picha zao wakibusu kwenye birthday party ya mtangazaji maarufu nchini Ghana wa Diva’s Show, Nana Aba Anamoah.
Nadia ambaye kwa sasa amejiingiza pia kwenye muziki, amezieleleza picha hizo kwa “innocent pictures” zilizopigwa kwenye party hiyo.
“Hakukuwa na kupigana busu; Essien na mimi ni marafiki lakini, hatuna issue kubwa sana. Lakini kuhusiana na ripoti kuwa tumerudiana, hakuna kitu kama hicho,” alisema.
Nadia aliendelea kueleza kwamba “tulikuwa tunajaribu kupiga picha na mapaparazi nao walikuwa wakipiga picha zao. Tulikuwa tupige picha mbili tu lakini wao waliendelea kuchukua picha nyingi na niliona aibu sana hivyo nilijaribu kumwacha Essien, nilitaka kuficha uso wangu tu.
Nadia na Essien waliachana miaka miwili iliyopita.

source:ghanacelebrities

MUME WA JACK PATRICK AHENYA KORTINI

Leave a comment


MUME wa mwanamitindo maarufu Bongo, Jacqueline Patrick, Abdulatif Fundukira (pichani katikati), Jumatatu iliyopita alihenya kusaka dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na ombi lake kutupiliwa mbali, Risasi Mchanganyiko linahabarisha.
Abdulatif alifikishwa mahakamani hapo akitokea mahabusu katika Gereza la Segerea jijini Dar es Salaam kutokana na tuhuma za kuhusika katika biashara ya madawa ya kulevya.
Mtuhumiwa huyo akiwa na wenzake watano baada ya kupandishwa kizimbani, aliiomba mahakama hiyo impatie dhamana lakini hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Riyad Chamshama alimwambia kuwa kulingana na uzito wa kesi yake hawezi kupata dhamana na kumtaka kupeleka madai yake mbele ya sheria kama ataona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.
Baada ya kupewa jibu hilo Abdulatif aliiomba mahakama hiyo impatie nakala ya mwenendo wa kesi hiyo kwa ajili ya matayarisho ya kulipeleka shauri hilo mbele ya sheria ili kupata dhamana ambapo aliambiwa atapatiwa wakati kesi hiyo itakapotajwa tena.
Hakimu Chamshama aliihairisha kesi hiyo hadi Julai 16, mwaka huu itakapotajwa tena Mahakamani hapo.
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki waliofika mahakamani hapo walisikika wakijadili kitendo cha mke wa Abdulatif, Jack Patrick ambaye aliwahi kuingia katika kinyang’anyiro cha kumsaka Miss Tanzania miaka ya nyuma kutoonekana mahakamani hapo.
“Inawezekana kuwa ameamua kumtosa mume wake?” alihoji mmoja wao huku wengine wakisema huenda mlimbwende huyo ametingwa na mambo muhimu.

source:globalpublishers.

KUONDOKA KWA KALALA JR BENDI YA MAPACHA 3 HAITAYUMBA.!

Leave a comment


Pichani kati ni Mwanamuziki mahiri Josee Mara akifafanua kuhusiana na mikakati yao waliyonayo kwa sasa mara baada ya mwanamuziki mwenzao mmoja,Kalala Jr kutimka na kuwaacha wakiwa wawili badala ya watatu.Josee Mara amesema wao wako fiti na hakuna kilichoharibika,kwani kuna wanamuziki wengine kadhaa ambao ni wazuri na watafanya nao kazi kama ilivyokuwa kwa Kalala Jr.”Na sasa hivi nakuhakikishia Da’Suzzy tutapiga kazi ile mbaya,kwa sababu hao vijana tunaowaongeza ni wanamuziki wazuri na tunawahamu toka kitambo,kwa hivyo naamini mambo yatakuwa sawa na washabiki wetu wasivunjike moyo,waendelee kutuunga mkono tu,sisi ni wapambanaji kwa hiyo ni lazima tupambane”amesema Josee Mara.Aidha Khalid Chokoraa ameongeza kuwa katika kuonesha bado wako fiti wamekwisharekodi singo yao moja iitwayo ONA NAONEWA,ambayo wataitambulisha hivi karibuni kwa mashabiki wa muziki wa dansiMmoja wa watangazaji wa Clouds FM,kupitia kipindi cha Wikend Bonanza,Da’ Suzzy akizungumza na wanamuziki mahiri wa dansi hapa nchini waliokuwa wakijiita Mapacha 3,ambapo kwa sasa mmoja wao Kalala Jr ameamua kuachia ngazi na kuwaacaha wenzake Khalid Chokoraa na Josee Mara kama uwaonavyo pichani wakiwa na Meneja wao Hamis Dacota pichani kulia.Da’Suzzy alikuwa akitaka kujua kwanini msanii mwenzao Kalala Jr ameamua kutimka kwenye bendi yao na kwamba wana mikakati gani ya kuliziba pengo la mwanamuziki huyo aliyetimka.Kwa mujibu wa Meneja wa bendi hiyo ya Mapacha 3,Hamis Dacota amebainisha kuwa Kalala Jr aliamua kuondoka mwenyewe bila kuwepo na ugomvi wowote baina yao,”hivyo kama mwanamuziki mwenzetu,kijana mwenzetu tunamtakia kila kheri huko aendako,lakini kama akitaka kurudi pia milango iko wazi anakaribishwa sana,kwa sababu yeye ni mmoja wa waasisi wa bendi ya mapacha 3″,alisema Dacota.

source:dewjiblog.

Fally na Mr. Flavour wafanya kazi Pamoja

Leave a comment


Mwanamuziki wa kizazi kipya cha lingala ya Congo, Fally Ipupa amezidi kuonesha ukaribu zaidi na wasanii wa Nigeria na kufanya nao ngoma.
Jana kupitia Facebook, alipost picha mbili akiwa kwenye ‘video shoot’ nchini Ufaransa na msanii wa Nigeria Flavour na kumaanisha kuwa wamefanya wimbo pamoja.
Wimbo huo mpya ni wa Flavour utakaokuwepo kwenye albam yake mpya.
Fally Ipupa amewahi pia kushirikishwa na Jay Martins katika remix ya wimbo wake uitwao Jukpa.
Jumamosi iliyopita, June 30, Flavour, kundi la Bracket na Dontom, walikuwa mjini Paris Ufaransa kwa mara yao ya kwanza na kutumbuiza mbele ye umati wa wapenzi wao wa muziki nchini humo.
Ziara hiyo ilimpa nafasi Flavour ya kumpata Fally Ipupa ambaye mara nyingi huwepo Paris na kufanya video yao jana.
Wasanii wa Afrika kutoka nchi zingine zisizozungumza kifaransa, wameanza kujipatia soko na umaarufu mkubwa nchini Ufaransa husasan wasanii wa Nigeria.
Mwezi March mwaka huu Flavour N’Abania alisaini mkataba na label kubwa ya muziki ya nchini Afrika Kusini iitwayo Sould Candi.
Mkataba huo ulifanikisha uuzwaji wa albam yake Uplifted, iliyokuwa na hit ‘Nwa Baby’ kuuzwa nchini Afrika Kusini.
Kwa upande wake Fally Ipupa, mwishoni mwa mwezi uliopita, aliungana na Ferre Gola mjini Paris kuimba wimbo wa kizalendo kwa nchi yao uitwao “Congo, my country.”
Wasanii wengine wa Congo walioshiriki kwenye wimbo huo ni Lokwa Kanza, Djessi Matador, Aimelia, Celeo Schramme na wengine ambapo jumla wapo wanamuziki 30.

Adele: Kupata ujauzito wa Simon Konecki!!

Leave a comment


Adele na Simon Konecki wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza. Ijumaa hii Adele mwenyewe alikiri kuwa wanatarajia kupata mtoto wao wakwanza na Simon Konecki, dada huyo ambaye ni mshindi wa Grammy aliwaambia mashabiki wake kwenye website yake kwa kuwa andikia habari kuhusu ujauzito huo na kutumia kichwa cha habari kinacho sema “I’ve Got Some News”
Simon Konecki ambaye ana umri wamiaka 38, ambaye ana mtoto wakike na vilevile yeye na mkewe wazamani walitalakiana January. Febuary Simon alimsindikiza Adele kwenye tuzo za Grammys ambapo kipindi hicho adele Mwenye umri wa miaka 24 alisema malengo yake nikuwa na watoto wa kiume watatu kabla hajafikia umri wa miaka 30. Na ujauzito huu unaonyesha kweli kuwa yupo tayari kutimiza malengo yake.
Adele “I really want to be a mum,” she said. “I better start getting on with it!”

source:thehollywoodgossip

NI LINI SERIKALI ITATIBU CHANZO CHA MGOMO WA MADAKTARI? – ANANILE NKYA

Leave a comment


Katika nchi  yeyote duniani serikali ndiyo  yenye  jukumu la kuweka mazingira mazuri katika hospitali za umma na kuhakikisha kuwamadaktari na wafanyakazi  wa afya  wanafanya kazi yao ya kutibu wagonjwa  kwa  furaha .

Hii  ni kwa sababu serikali  iliyowekwa  madarakani na wananchi moja ya kazi ya   kodi inayokusanya kutoka kwa wananchi   ni kuhakikisha kuwa  hospitali, vituo vya afya na zahanati za umma ziko katika mazingira mazuri na zinatoa huduma nzuri kwa wananchi.

Mazingira mazuri hospitalini ni pamoja na  kuwepo kwa vitanda vya kutosha kwa  wagonjwa,  madawa ya kutosha na ya viwango bora, vifaa kwa ajili ya kupima na kubaini magonjwa na vifaa  na vyumba maalum vya kusaidia watu  wanaofanyiwa upasuaji wasipoteze maisha.

Lakini hali ya hosipitali zetu za umma ni hairidhishi.   Kwa mfano hospitali ya taifa ya   Rufaa Muhimbili ni hospitali  madaktariwanalalamika kuwa hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinawafanya madaktari  kushindwa kutimiza wajibu wao wa  kuokoa maisha ya wagonjwa.

Kwa mfano  hospitali hiyo ina   mashine  ya MRI  ya kupima na kutambua ugonjwa  mbali mbali  kwenye mwili ikiwa ni pamoja na kwenye   ubongo, uti wa mgongo na kifua. 

Lakini  cha kushangaza mashine hiyo  iliyonunuliwa kwa  shilingi zisizopungua Bilioni mbili miaka michache iliyopita,  inapungukiwa kifaa cha bei ndogo  tu cha    kuwezesha  watoto kupimwa. 

Hivyo watoto wenye matatizo yanayohitaji kupimwa kwa mashine hiyo  wanalazimika kupelekwa India au Afrika ya Kusini kwa wale wenye uwezo  wa kujigharamia  vinginevyo kwa maskini walio wengi  huishia  watoto wenye matatizo makubwa yanayoitaji utambuzi wa mashine hiyo, huishia kufa.  

Aidha  madaktari wanalalamika   jinsi wanavyoshindwa kuokoa maisha ya watoto   wanaozaliwa na tatizo la koromeo  la chakula kuungana na koromeo la hewa. Mabingwa wa upasuaji  wa watoto katika hospitali hiyo  wanasema kwa upande wao wanajitahidi kuwafanyia  watoto hao upasuaji, lakini watoto hao huishia  hufariki dunia  kutokana na hospitali hiyo ya Rufaa kukosa  vifaa maalum vya kuhudumia watoto hao na vyumba maalumu vya kuwaweka  baada ya kufanyiwa operasheni.  

“Kinauma sana  na kinakatisha tamaa sana kuona kwamba mtoto anafanyiwa   upasuaji vizuri lakini anapoteza maisha siku chache baadaye kutokana na kukosekana kwa vifaa na mazingira ya kumwezesha  kupona baada ya upasuaji”, anasema  Dakta Catherine Mungo’ngo, Bingwa wa upasuaji wa watoto Hospitali ya Rufaa ya Taifa.

Kwa mujibu wa bingwa huyo kwa mwaka huu pekee watoto watatu  waliozaliwa na tatizo la la koromeo  la chakula kuungana na koromeo la hewa ambao  walifanyiwa upasuaji  Muhimbili,    baadaye  walikufa hospitalini hapo kutokana na kukosekana kwa vifaa vya kuwasaidia kupumulia na chumba maalumu  cha kuwafanyia uangalizi baada ya upasuaji.

Aidha anasema watoto  kati ya 6 hadi 8 wanaohitaji kufanyiwa upasuaji kwa siku, upasuaji huo huahirishwa kutokana na ukosefu wa vifaa , dawa na chumba maalum cha kuwatunzia baada ya upasuaji.

Ni mtu gani mwenye akili timamu  ambaye atafurahia  kuona kazi anayoifanya  haitoi  matunda yanayotarajiwa.?  Ni Daktari gani atakayeendelea kufurajhia kazi yake wakati lengo lake la kuokoa maisha ya watu  linakwamishwa  na  mambo yanayowezekana kurekebishwa?

Daktari furaha yake ni kutibu mgonjwa na kuona anapona. Lakini Daktari katika hospitali za  serikali  atafanyaje kazi yake kuepusha vifo  visivyo vya lazima kama hana vifaa vya kufanyia kazi ?   

Nionavyo mimi,  serikali yetu inapaswa kutafakari tena kwa utulivu na busara kubwa  na kuweka mikakati ya kupata suluhisho la kudumu la mgogoro  wake na madaktari. 

Vinginevyo hata kama wataagizwa  madaktari kutoka Ulaya, na wa hapa nchini kufukuzwa kazi au hata kama viongozi wao ‘watashughulikiwa’,  tatizo la  mazingira ya kazi  hospitalini ambalo ni moja  ya  mambo ya msingi   linalosababisha mgomo wamadaktari   litakuwa halijashughulikiwa  na litaendelea kujirudia  hata kama litapoozwa   kwa mbinu yoyote ile.

 Na ikumbukwe watakaoendelea kuumia zaidi hapa ni wananchi wengi  ambao maisha yao yanategemea uwajibikaji wa serikali yao.

Nijuavyo mimi, serikali  ya wananchi, madaktari wakiwa ni sehemu ya wananchi, husikiliza kero za wananchi na kuzishughulikia badala ya kutumia mabavu na vitisho. 

Mungu ibariki Tanzania.


Ananilea Nkya 

Executive Director 
Tanzania Media Women’s Association (TAMWA) 
P. O. Box 8981, Sinza-Mori 
Dar es Salaam, TANZANIA 
Tel: +255-22 2772681 
Fax +255 22 2772681 

E-mail: ananilea_nkya@yahoo.com
Cellphone:+255-754-464-368

Older Entries

%d bloggers like this: