Home

Wema Sepetu na Diva waingia kwenye orodha ya kusaidia wasiojiweza

Leave a comment


Ray Kigosi akitoa msaada

Lady Jay Dee akitoa msaada

Lady Jay Dee

Wema Sepetu

Diva Loveness Love

Muigizaji wa filamu nchini na Miss Tanzania wa zamani (2006),Wema Sepetu anatarajiwa kwenda jijini Arusha mwezi huu na kushiriki uoashaji wa magari ili kukusanya fedha za kusaidia watu wasiojiweza jijini humo.
“On 14th July I will be in Arusha with manager kushiriki uoshaji wa magari ili kuchangia fedha za kusaidia wasiojiweza in Arusha,” alitweet jana.
Mwingine aliyeamua kujitolea nguvu na mali kuchangisha fedha kwaajili ya kuwasaidia watoto yatima ni mtangazaji wa Clouds Fm, Loveness aka Diva.
Kupitia website yake, Diva amesema, “So nimeamua kwa muda mrefu sana kutoa for charity and right now am too busy organizing this charity event inayoitwa Diva giving for charity. Aim is raising much needed funds to support orphans.
June na July imekuwa miezi iliyotumiwa zaidi na mastaa wa hapa nchini kusaidia vituo vya watoto yatima.
June 30, mwanamuziki Lady Jaydee pamoja na familia yake walikitembelea kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre kilichopo Kinondoni jijini Dar es Salaam na kutoa misaada mbalimbali ikiwa pamoja na kushiriki chakula cha mchana na watoto hao.
Katika hotuba yake, kituo hicho kilisema kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo ni pamoja na kukosa fedha za kuwalipa wahudumu, Kukosa eneo kubwa la kujenga kituo, Kukosa wafadhili, watoto kutokuwa na sare za shule na kukosa gharama za kuwasomesha (michango ya shule).
Lady Jaydee aliwaahidi kuwatafutia kiwanja kikubwa kwaajili ya kujenga kituo kingine na kusema kuwa iwapo akitokea mtu wa kuwasaidia kiwanja, watachangisha fedha za kuanza ujenzi huo.
Naye muigizaji wa filamu mwenye mafanikio makubwa nchini Raymond Kigosi aka Ray The Greatest, weekend iliyopita alikitembelea kituo hicho cha Maungo na kutoa msaada sambamba na uzinduzi wa filamu yake mpya ya Sobbing Sound.
Kupitia blog yake Ray alisema: “Hili ni jukumu la watanzania wote kuanza kuguswa katika hili maana hapa duniani sisi ni wapangaji tu makazi yetu ni kwa Mungu Baba, sasa unapopata kidogo jaribu kuwafikiria na wale waliokuwa na maisha magumu, yaani tugawane umasikini.”

source:

Fally na Mr. Flavour wafanya kazi Pamoja

Leave a comment


Mwanamuziki wa kizazi kipya cha lingala ya Congo, Fally Ipupa amezidi kuonesha ukaribu zaidi na wasanii wa Nigeria na kufanya nao ngoma.
Jana kupitia Facebook, alipost picha mbili akiwa kwenye ‘video shoot’ nchini Ufaransa na msanii wa Nigeria Flavour na kumaanisha kuwa wamefanya wimbo pamoja.
Wimbo huo mpya ni wa Flavour utakaokuwepo kwenye albam yake mpya.
Fally Ipupa amewahi pia kushirikishwa na Jay Martins katika remix ya wimbo wake uitwao Jukpa.
Jumamosi iliyopita, June 30, Flavour, kundi la Bracket na Dontom, walikuwa mjini Paris Ufaransa kwa mara yao ya kwanza na kutumbuiza mbele ye umati wa wapenzi wao wa muziki nchini humo.
Ziara hiyo ilimpa nafasi Flavour ya kumpata Fally Ipupa ambaye mara nyingi huwepo Paris na kufanya video yao jana.
Wasanii wa Afrika kutoka nchi zingine zisizozungumza kifaransa, wameanza kujipatia soko na umaarufu mkubwa nchini Ufaransa husasan wasanii wa Nigeria.
Mwezi March mwaka huu Flavour N’Abania alisaini mkataba na label kubwa ya muziki ya nchini Afrika Kusini iitwayo Sould Candi.
Mkataba huo ulifanikisha uuzwaji wa albam yake Uplifted, iliyokuwa na hit ‘Nwa Baby’ kuuzwa nchini Afrika Kusini.
Kwa upande wake Fally Ipupa, mwishoni mwa mwezi uliopita, aliungana na Ferre Gola mjini Paris kuimba wimbo wa kizalendo kwa nchi yao uitwao “Congo, my country.”
Wasanii wengine wa Congo walioshiriki kwenye wimbo huo ni Lokwa Kanza, Djessi Matador, Aimelia, Celeo Schramme na wengine ambapo jumla wapo wanamuziki 30.

Madaktari 72 wasimamishwa kazi kwa Mgomo

Leave a comment


Mwenyekiti wa Bodi Kaimu [caption id="attachment_3013" align="alignleft" width="500"] Mkurugenzi wa wa hospitali ya rufaa Mbeya Dr E. Sankey akimsikiliza kwa makini kaimu mkuu wa mkoa Mbeya.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman Sigara Aikzungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu kusimamishwa kazi kwa madaktari hao.[/caption]BODI ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, imewasimamisha kazi madaktari 72 kwa kosa la kutoingia kazini kwa siku tano jambo ambalo ni kinyume cha makubaliano ya mkataba.

Imeelezwa kuwa madaktari hao ambao 54 ni wale wa mafunzo ambao waliingia mkataba wa miaka miwili na hospitali ya Rufaa na madaktari 18 ni wale walioajiriwa na Wizara ya afya.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Norman Sigara, alisema kitendo cha madaktari kutoripoti kazini kwa siku tano ni ukiukwaji wa kanuni za utumisha wa umma toleo la 2009 kifungu namba F.16-F17 na F. 27.

“Hivyo kupitia kanuni hiyo madaktari hao wamesimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa hatua zaidi za kinidhamu,”alisema Sigara.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa Bodi, imeelezwa kuwa siku ya tarehe 23/6/2012 wafanyakazi 15 waliokuwa zamu(Intern Doctors 12 na Registrars3) hawakufika kazini na tarehe 24/6/2012 wafanyakazi 19(Intern doctors 15 na Registrars 4) hawakufika kazini.

Alisema, kuanzia tarehe 25/6/2012 hadi leo imethibitika kuwa Interns doctor 54 na Registrars 18 hawakufika kazini hadi leo tarehe 28/6/2012 ambapo tarehe 25/6/2012 bodi ya hospitali ilifanya kikao cha dharura kujadili hali ya utendaji kazi na utoaji huduma hospitalini na kutoa uamuzi.

Sigara, aliyataja maamuzi hayo kuwa ni Mwenyekiti wa Bodi akutane na madaktari ambao hawakufika kazini ili awasikilize sababu za kutofika na kujadili namna ya kumaliza matatizo hayo jambo ambalo madaktari hao waligoma.

Alisema, baada ya madaktari hao kukaidi ombi hilo, Bodi ya hospitali ili waandikia barua za kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuvunja mkataba walioingia na hospitali na pia kukiuka
kanuni za kudumu za utumishi wa umma nalo walilikaidi

“Iwapo madaktari ambao hawakuripoti au kueleza sababu za kuridhisha ifikapo tarehe 28/6/2012. Kwa kuzingatia kanuni za utumishi wa Umma, madaktari hao watasimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,”alisema.

Aidha, alisema kuwa kwa ujumala madaktari hao waligomea barua zote mbili yaani ya kuitwa kwenye kikao pamoja na ile ya kuwataka kujieleza hivyo Bodi imechukua hatua za kisheria za kuwafukuza kazi.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo wa bodi, alisema kuwa tayari hospitali ya Rufaa kwa ushirikiano wa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, madaktari watano wamepatikana ili kusaidia huduma kwa hospitali hiyo.

Huyu ndiye Mwigizaji anayelipwa hela nyingi Nchini Ghana kwa sasa

Leave a comment


Yvonne Nelson on Cover Page

Muigizaji mwenye scandal kibao lakini mwenye kipaji cha hali ya juu nchini Ghana, Yvonne Nelson ameibuka kuwa muigizaji anayelipwa mkwanja mrefu zaidi nchini humo na kuwashinda wengine kama Jackie Appiah na Nadia Buari.
Waigizaji hao watatu kwa mujibu wa utafiti walikuwa ‘madiva’ wanaotafutwa zaidi huko Ghollywood na sasa Yvonne ambaye amekuwa akihusika na scandal kibao amekamata nafasi ya kwanza katika list hiyo.
Yvonne, model, designer,mfanyabiashara na muigizaji aliyeshirikishwa kwenye filamu lukuki za kimataifa huku mpya akiwa ameigiza kama Halima Abubakar kwenye ‘Mistress’ hafanyi mazungumzo kwa ‘madafu’ ya Nigeria (naira) bali ni kwa dola ya Marekani tu.
Na sasa bila dola 10,000 mezani ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 15 za Tanzania hawezi kufanya movie.
Bei yake hiyo kubwa tayari imewafanya baadhi ya waandaji wenye bajeti ndogo kusitisha mipango yao ya kumtumia kwenye filamu zao.
Pamoja na kumlipa $10,000, kuna masharti na vigezo vingine vinapaswa kuzingatiwa na kama asipoviona, bado producer anaweza kuondoka na hela zake.
Kwa sasa mrembo huyo amelamba mkataba mnono wa matangazo na kampuni ya Vodafone

source:.bongo5

Chris Brown alaumu media (vyombo vya Habari)

Leave a comment
STAA Chris Brown amesema vyombo vya habari vimekuwa vikipotosha ukweli kuhusu ugomvi uliotokea hivi karibuni kati yake na rapa Drake.
Brown alisema vyombo vya habari vimekuwa vikielemea upande mmoja bila kutaka kuchunguza ukweli wa ugomvi huo.
“Ninasikitishwa na jinsi vyombo vya habari vinavyoripoti hili jambo, hakuna anayejua ukweli wa ugomvi ule zaidi yangu mimi na Drake, kwanini hamuulizi mnaandika tu?” Alihoji Brown katika mtandao wa twitter.
Pamoja na kuvilaumu vyombo hivyo, pia anamtupia lawama, Drake, kuwa ndiye aliyeanzisha ugomvi huo kwa kurusha chupa hewani.

Keko ‘kuchana’ mbele ya rais Museveni

Leave a comment


Msanii wa kwanza wa kike wa hip hop kuwahi kufanikiwa nchini Uganda Keko, leo anatarajiwa kutumbuiza mbele ya rais Yoweri Museven na mke wake. Rais huyo atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa MaryHill High School Mbarara.

Mke wa rais Museveni, Janet Museveni alisoma katika shule hiyo ambapo Keko naye alisoma.
Asubuhi ya leo (June 23) ametweet, “MARYHILL High School Golden Jubilee Celebration Today ‪#CatchMeInYourCity‬ MBARARA HERE I COME ‪#KekonianArmy‬ Goodmorning.”

Msanii huyo kwa sasa wimbo ana wimbo aliomshirikisha Madtraxx wa Kenya uitwao “Make You Dance” unaofanya vizuri barani Afrika na Ulaya. Rapper huyo kwa sasa ni miongoni mwa wasanii wa kike wanaofanya hip hop waliofanikiwa zaidi barani Afrika

Mcheza sinema wa Marekani, Deidre Lorenz atua mjini Moshi na shauku kubwa ya kuona kama kweli mlima Kilimanjaro uko Tanzania!

Leave a comment


Deidre Lorenz na Rais wa IBF-USBA bala la Africa, Masharini ya Kati na Ghuba ya Uajemi Onesmo Ngowi.


Mcheza sinema toka Marekani Deidre Lorenz amewasili mjini Moshi tayari kushiriki kwenye mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika juni 24. Lorenz amwasili leo na ndege ya Ethiopian Airlines ambao ndio wafadhali wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zinazofanyika jumapili ya mwisho ya mwezi wa sita kila mwaka.

Ujio wa Lorenz ambaye amecheza sinema nyingi zikiwamo Santorini Bule, Perfect Strangers, The Big Fight umeleta msisimko mkubwa katika mji huu mkuu wa Kilimanjaro. Ujio wake umefuatia matayarisho ya muda mrefu ambayo yanaendana na hadhi yake.

Akizungumza na waandishi wa habari waliofika kumshuhudia mcheza sinema huyu, Lorenz alisema kuwa ameisikia kuwa mlima wa Kilimanjaro uko Kenya kwa kwa muda mrefu na ana furaha kubwa sana ya kufika ili kushughudia kuwa mlima huu maarufu duniani uko Tanzania. “Nimekuwa nautangaza sana ujio wangu kwenye blog na tovuti yangu, wapenzi wangu pamoja na watu wengi wanangojea kurudi kwangu nikawaambie niliyoyashughudia” alisema Deidre Lorenz ambaye ameshawahi kuteuliwa zaidi ya mara tatu kwa tuzo za Oscar. Lorenz alisema kuwa kwa miaka mingi alifikiri kuwa mlima Kiliamnjaro uko Kenya kwa jinsi nchi hiyo jiraniminavyoutangaza nchini Marekani.

“Sasa nimeona mwenyewe kwa macho yangu kuwa kweli mlima (Kilimanjaro) huu maarufu duniani uko Tanzania na sio Kenya” alisema Deidre Lorenz ambaye anaishi kwenye jiji la New York City linalofahamika kama jiji la pesa (International Financial Capital) la kimataifa. Lorenz ameshukia katika hoteli ya Bristol Cottages iliyopo karibu na benki ya Standard Chattered mkabala na bustani ya Manispaa ya Uhuru Park.

Older Entries

%d bloggers like this: